Sensa ya tembo: Tembo wazidi kuangamia tanzania

Mlachake

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2009
Posts
4,451
Reaction score
4,655
Wizara ya Maliasili na utalii imetangaza matokeo ya sensa ya Tembo ambayo yanaonesha kuwa kati ya mwaka 2009 na 2013, Tembo wamepungua kwa 66% katika maeneo ya mfumo ikolojia wa SELOUS–MIKUMI na 36.5% katika maeneo ya mfumo ikolojia wa RUAHA–RUNGWA.

Jumla ya mizoga 6,516 ya Tembo imepatikana Selous–Mikumi na mizoga 3,496 imepatikana Ruaha–Rungwa na jumla ya meno ya Tembo yenye uzito wa Kilogramu 32,987 yamekamatwa ndani na nje ya nchi kati ya mwaka 2008 hadi Septemba 2013.

Nini maoni yako juu ya kuokoa rasilimali hii ya Tembo kwa ajili ya Tanzania ijayo?
 
Ni hali ya kusikitisha sana kuwa wahusika wameshindwa kutekeleza kwa ufanisi mipango na mikakati ya kulinda maliasili hii
 
Wizara ya Maliasili na utalii imetangaza matokeo ya sensa ya Tembo ambayo yanaonesha kuwa kati ya mwaka 2009 na 2013, Tembo wamepungua kwa 66% katika maeneo ya mfumo ikolojia wa SELOUS–MIKUMI na 36.5% katika maeneo ya mfumo ikolojia wa RUAHA–RUNGWA.

Jumla ya mizoga 6,516 ya Tembo imepatikana Selous–Mikumi na mizoga 3,496 imepatikana Ruaha–Rungwa na jumla ya meno ya Tembo yenye uzito wa Kilogramu 32,987 yamekamatwa ndani na nje ya nchi kati ya mwaka 2008 hadi Septemba 2013.

Nini maoni yako juu ya kuokoa rasilimali hii ya Tembo kwa ajili ya Tanzania ijayo?

kachukueni takwimu sahihi ofisini kwa katibu mkuu
 
Dah! Inasikitisha sana ila serikali inachangia hili sababu hata hao wanaopewa mamlaka ya kulinda hifadhi za wanyama ndo wa kwanza kufanya ujangili>>>>>>> yaan nomaaa sanaa!!!!
 
Wachina acheni Mara moja kutuongezea umaskini kwa huu ujambazi,tutawapiga ban msije kabisa
 
Back
Top Bottom