Sensa ingefanyika hivi - it could have been cheaper and time saving

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
1,222
764
Naambiwa budget ya sensa ya mwaka huu ni Tshs160 Billion. Jana nikakutana na Mwenyekiti na Katibu Mtendaji wakaniambia mpaka sasa hawajalipwa na hata wakilipwa haitazidi shs 150,000 kwa mtu. Najaribu kupiga hesabu na kugundua kwamba hela nyingi imetumika katika administration and logistics. Na siku ya mwisho anaehesabu watu ni watu wa chini kabisa. Mimi leo nimehasabiwa na sijaona hata swali moja ambalo ni very technical kumshinda balozi kuniuliza.

JE? Ni kwanini Sensa isingerudishwa kwa Mkurugezi wa maendeleo wa wilaya na yeye aka delegate kwa WEO na kufika mpaka kwa mabalozi? Je isingetumia muda mdogo na pesa kidogo?
 
Nimewasikia watu wengine leo wakizungumzia pia kuwatumia maafisa watendaji wa kijiji na wenyeviti wa mitaa badala ya makarani wanaotumika sasa.
 
mimi nahisi ni maandalizi ya kutohoa pesa za uchaguzi wa 2015,
ukizingatia mradi wa ujenzi wa bot na epa pesa zilitumika ktk kampeni za 2005,kuna miradi kama ya mabasi ya kasi dsm,ujenzi wa kigamboni city,upanuzi wa bandari,na hili la sensa yote ni kwa ajili ya lengo la kukusanya na kuhalalisha matumizi makubwa yasiyo ya lazima. SEnza ingefanywa kwa mfumo wa wtu kujitolea ,i.e volunteers wapo wengi tu na kila mjumbe wa mtaa angeweza kupata japo watu watatu kujitolea ktk mtaa wao
 
Tanzania bhana, we acha tu! Tunajua tuna walimu wangapi na tumeshindwa kuwahudumia, tukijua watanzania wote halafu iweje?
 
Ili pesa iliwe inabidi ujustify,AG aanze kufanya uchunguzi maana naona ambao ujenzi ulikuwa umekwama sasa majengo yanaenda kwa kasi,watu wanajua kuila nchi.
 
serikali inasema inafanya sensa ili kuiwezesha kupanga mipango ya maendeleo na kutoa huduma kwa wananchi, naomba niulize tangu uhuru hadi leo bado wanafunzi
mashuleni wanakaa chini. je serikali haijui idadi ya wanafunzi ili kutengeneza madawati yakutosheleza wote? me naona sanaa imetawala
 
Naambiwa budget ya sensa ya mwaka huu ni Tshs160 Billion. Jana nikakutana na Mwenyekiti na Katibu Mtendaji wakaniambia mpaka sasa hawajalipwa na hata wakilipwa haitazidi shs 150,000 kwa mtu. Najaribu kupiga hesabu na kugundua kwamba hela nyingi imetumika katika administration and logistics. Na siku ya mwisho anaehesabu watu ni watu wa chini kabisa. Mimi leo nimehasabiwa na sijaona hata swali moja ambalo ni very technical kumshinda balozi kuniuliza.

JE? Ni kwanini Sensa isingerudishwa kwa Mkurugezi wa maendeleo wa wilaya na yeye aka delegate kwa WEO na kufika mpaka kwa mabalozi? Je isingetumia muda mdogo na pesa kidogo?

upo sahihi mkubwa
 
Tanzania bhana, we acha tu! Tunajua tuna walimu wangapi na tumeshindwa kuwahudumia, tukijua watanzania wote halafu iweje?

wakijua idadi ya watu wote wataweza kujua wanahitajika walimu wangapi na watazalisha walimu wangapi baadae?
 
Mojawapo ya maoni yangu kwenye katiba mpya ni kuwepo kwa wajumbe wa kaya 20 ambao watakuwa viongozi wa kiserikali na wala sio wa kichama. Hawa watachaguliwa kwa kura na watawajibika kuhakikisha usalama ktk maeneo yao pamoja na majukumu mengine. Mazoezi yote ya kitaifa mf. sensa, chanjo, uandikishaji wapiga kura n.k. watahusika moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom