SENGEREMA : Mgambo akaimu ofisi ya ofisa mtendaji kwa miaka minane

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mkazi kijiji cha Nyancheche, Kata ya Kagunga wilayani hapa, Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mgambo, Faustine Njingo amekaimishwa ofisi ya ofisa mtendaji wa kijiji hicho kwa zaidi ya miaka minane bila kuwa na taaluma hiyo

Suala hilo liliibuka wakati wajumbe wa kamati ya mfuko wa Jimbo la Sengerema walipofika kijijini hapo kutoa msaada wa madawati na kukuta ofisi imefungwa bila mtumishi wa Serikali kuwapo, kitendo kilichowashangaza

Baada ya nusu saa kupita, alitokea mkazi mmoja wa kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina la Makoye Masaga na kuwaeleza kuwa watumishi wote wa ofisi hiyo wameitwa ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema

Makamu mwenyekiti wa mfuko huo, Rachel Mabihya alimuuliza mwananchi huyo kama Mtendaji wa kata hayupo, ofisa Mtendaji wa kijiji yuko wapi..!? alijibu kuwa ofisi hiyo haina Mtendaji bali anayekaimu ni Mgambo ambaye naye ameelekea huko

Mratibu elimu Kata ya Kagunga, Maxmiliani Shija ambaye pia alipita ofisini hapo akitokea kwenye shughuli zake alithibitisha pia ofisi hiyo kukaimiwa na mgambo

Alipopigiwa simu ili athibitishe kama anakaimu ofisi hiyo, Njingo alikiri na kusema,"Mimi sasa hivi siyo mgambo naitwa ofisa mtendaji kwa sababu nimekaimu nafasi hii kwa zaidi ya miaka minane sasa."

Alisema alikabidhiwa ofisi hiyo na mjumbe wa Serikali ya kijiji aliyemtaja kwa jina la Daudi Kisinza "Kisinza naye alipewa barua na mkurugenzi ya kukaimu ofisi hiyo lakini alishindwa kufanya hivyo na kusababisha wananchi kukosa kazi hiyo na nitaendelea kuifanya," alisema Njingo

Diwani wa Kagunga, Michael Masunzu alipoulizwa juu ya mgambo huyo kukaimu ofisi alisema anastahiki kwa kuwa ni mtu mwema na anahudumia wananchi vizuri.


Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom