Sengerema: Fransico Kimasa Shejamabu ajiunga CHADEMA, Kugombea Ubunge

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,798

Mapokezi ya Fransico Kimasa Shejamabu (mwenye gwanda) akielekea katika viwanja vya shule ya msingi Pambalu wilayani Sengerema kuhutubia wananchi. (picha zote na Daniel Makaka wa MOblog, Sengerema).

Na Daniel Makaka, Sengerema.Aliyekuwa kada wa wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya Sengerema mkoani Mwanza Bw. Fransico Kimasa Shejamabu ametangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)ambacho amejiunga nacho.

Kauli hiyo ameitoa mjini hapa alipokuwa akiwahutubia maelfu ya wakazi wa wilaya Sengerema waliofika katika viwanja vya shule ya msingi Pambalu.Alisema yeye si mwanachama tena wa CCM na kwamba amekihama chama hicho kutokana na kukosa mvuto kwa kutokana na viongozi wake kuhusishwa na mambo ya kifisadi .

Bw. Shejamabu huku akishangiliwa aliwatangazia wananchi kuwa amekwisha weka nia ya kugombea ubunge jimbo la Sengerema kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hivyo kuwaomba wanasengerema kumuunga mkono yeye na chama chake ili kiwaletee maendeleo jimboni humo.

Mwanachama mmoja wa CHADEMA Bw. James Ndahihya alisema wanamshukuru Mungu kwa kumuelekeza kada huyo wa CCM kujiunga na chama cha ukombozi wa watanzania kwani sasa jimbo la Sengerema limepata mgombea ubunge.Bw. Shejamabu amesema ameingia Chadema kulikomboa jimbo la Sengerema .

 
Tuko naye kwa jicho la tatu. Tunamkaribisha si yeye tu hata wengine wakitaka. Hawajachelewa sana, tunawahitaji wao pamoja na wanachama wengine kutoka ccm. Wakubaliane na masharti ya chadema kukijenga chama.
 
hawa wengine wanaangalia upepo ndio wanaleta vurugu kwenye vyama kwani ameshwinda nini kugombea ubunge kupitia ccm ningemuelewa kama angesema amechoshwa na ufisadi wa ccm
 
Wale wanaojitoa dakika za mwisho na kuruhusu mafisadi kupita bila kupingwa
 
Huyo apigwe chini.... Sasa kipindi Alphonse mawazo amekuja huko kukampeni alishindwa nn kujiunga? Na kwann atangaze ubunge wakat ss ndo tulojenga miziz ya chama letu huko?
 
Huyo apigwe chini.... Sasa kipindi Alphonse mawazo amekuja huko kukampeni alishindwa nn kujiunga? Na kwann atangaze ubunge wakat ss ndo tulojenga miziz ya chama letu huko?
 
yaelekea makapi yote yatakimbilia huko. chadema na wengineo andaeni watu mnaowaamini na sio kusubiri makapi ya ccm dakika za mwizho.
 
Anataka kugombea ubunge kwani hakuna watu wenye sifa waliokitumikia Chama kwa muda mrefu?
 
Mh.... mbona ana kasi sana! Ndio ameambiwa karibu hata kigoda hajapewa tayari anafikiria ubunge? Na asipopitishwa si atahamia kwingine!
CHADEMA haitaki hawa sampuli za Shibuda. Asipewe cheo chochote ndani wala nje ya chama bali apimwe kwa kazi za kukijenga chama kwa miaka minne kwanza!
 
Hskika 100% ni pandikizi chili. Alelewe akomae miaka 5 kwanza. Huyu ni mithili ya John shibuda
 
Geita Mkuu

Thanks for the Update. Kuna kamanda nilipekua naye Chuo anaitwa Rogers nimesikia ni katibu wa chama cha ukombozi wa Mtanzania wilaya ya Geita...Ama kweli vijana ni chachu ya mabadiliko.
 
Swali langu wakati wa uchaguzi wa serekali za mitaa alikuwa upande gani alikuwa keshahamia cdm au ni baada ya uchaguzi .Kama ni baada awe mwanachama wa kawaida kugombea no Kama alishiriki kikamilifu upande wa cdm yes
 
Kama anasifa za kuwa mbunge tunamkaribisha na ajue kuwa kuwa mwanachadema Si lelema nilAzima aJiToe muhaNga.
ahi
 
Back
Top Bottom