JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,112
- 3,536
Wanabodi salamu!
Kwa muda mrefu watu wengi wamekuwa wakilalamika kuwa tatizo la Nchi hii siyo ccm bali ni mfumo wa kitawala lakini hawatoi nini kifanyike.Nchi ina kila kitu kizuri kwa ustawi wa Nchi lakini tatizo kubwa ni kwamba mambo mengi yamebaki aidha kwenye katiba au maelekezo mengine bila kufanyiwa kazi.Utaratibu wa uendeshaji wa Nchi yetu ni sawasawa kabisa na wa Uingereza au Nchi nyingine zilizo kuwa chini ya himaya ya Uingereza.Tatizo ni kwamba watendaji wengi hawjui wajibu wao au au kwasababu ya umasikin wanafanya mambo kwa kuto jiamini kwa kuhofia kuwakwaza wakubwa! MKUBWA NI KATIBA na siyo binadamu, na ndio maana nikasema ni vizuri nikabainisha kwenye andiko langu hili nani hasa wanao takiwa kupewa semina elekezi.wafuatao wanatakiwa kupewa semina elekezi kwanza:
1.IGP NA JESHI LA POLISI
2.MWENDESHA MASHITAKA, DPP.
3.WABUNGE
4.MAHAKIMU NA MAJAJI WOTE
5.WATUMISHI WA UMMA.
IGP NA JESHI LA POLISI
Tunaposema tunataka Nchi iongozwe kwa kufuata utawala wa sheria (rule of law) jeshi la polisi ni chombo muhimu sana.Kikatiba ndio wenye mamlaka ya kuchunguza, kupeleleza na kuandaa mashitaka.jeshi la polisi ndio wenye jukumu la kuona SHERIA ZOTE zinatekelezwa ipasavyo.Hapa tulipo fika yaani watu kuvuta sigara ovyo na kila mahali, kujenga kiholela, kufanyia biashara maeneo yasiyo ruhusiwa, watu kutokufuata taratibu hizi au zile ni matokeo ya jeshi la polisi kutokujua wajibu wao.Jeshi la polisi ni Law enforcers kisheria.Kama mtu ana vibali vya kujenga mahali pasipo ruhusiwa, polisi wana wajibu wa kuchunguza kuona nani amekiuka kanun,taratibu na sheria ili aliyeisababishia serikali hasara achukuliwe hatua.
Fikiria mtu au kikundi cha watu wametuhumiwa kwa wizi kama ule wa EPA, TEGETA ESCROW, WANYAMA HAI KUUZWA n.k lakini polisi hawajanzisha uchunguzi ni kwasababu aidha hawajui sheria au wanawaogopa wathumiwa kwa sababu za kisiasa.WANATAKIWA WAPATE SEMINA ELEKEZI.
MKURUGENZI WA MASHITAKA.
Kimsingi hakuna mtu aliye juu ya SHERIA. Mtu yeyote akitenda kosa taratibu za kumchunguza kubaini kama kuna jinai amefanya au amevunja katiba zianze na hatimae mashitaka dhidi yake yafunguliwe.Sheria haibagi mtu wote wako sawa mbele ya sheria tofauti ni process za kumfikisha mahakamani. kuna wengi bunge lazima likubali waondolewe kinga ndio washitakiwe, MKURUGENZI WA MASHITAKA hatakiwi kupata kigugumizi lazima sheria itawale. hawa wanatakiwa wapate semina elekezi.
WABUNGE.
Wabunge ni muhimu wakapewa semina elekezi ili wajue maslahi ya Nchi ni yapi na maslahi ya vyama ni yepi. Katika mambo yenye masilahi ya Nchi ni muhimu wakawa kitu kimoja.Kamwe wasitunge sheria zinazo kinzana na katibu kwasababu ya kulinda vyama vyao.
WATUMISHI WA UMMA
Watumishi wa umma wamefika hapa kwasababu mahali fulani serikali ililegea katika kuwawajibisha wanapo kosea.kuna mkorea mmoja aliwahi kusema ili mtumishi wa umma Tanzania afukuzwe kazi labda auwe vinginevyo atafanyakazi mpaka asitaafu.WATU WAPEWE SEMINA ELEKEZI NA UKURASA MPYA WA UWAJIBIKAJI UFUNGULIWE.
MAHAKAMA.
Haki hainunuliwi. Ila kwa miaka ya karibuni mwenye pesa huwezi kumshinda. Jambo hili ni baya.watumishi wa idara hii wakitenda haki, dhuruma na vitendo viovu na waovu wenyewe watapungua