Sema,"Ahsante Mungu"

Peculiar

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2015
Posts
821
Reaction score
689
TAJIRI aliamka asubuhi, akachungulia dirishani akamuona MASIKINI anaokota chakula jalalani. Tajiri akajisemea moyoni ,ASANTE MUNGU mimi si masikini.

Masikini nae alipogeuka nyuma, akamuona kichaa kavua nguo zote, masikini akajisemea,"ASANTE MUNGU mimi sio KICHAA.

Kichaa naye alipoangalia barabarani akaona ambulance ikipeleka mgonjwa hospitali... Kichaa pia akajisemea... "ASANTE MUNGU" mimi sio MGONJWA.

Mgonjwa naye alipoangalia nje akaona watu wamebeba MAITI wanaenda kuzika. Mgonjwa pia akajisemea, "ASANTE MUNGU" mimi sijafa.

Mshukuru Mungu ikiwa bado unapumua na kuvuta pumzi yake...

Sema... Asante Mungu.
 
Kwa mwenye kujitambua inatakiwa ajifunze kitu hapa.

Tuwe tunashukuru kwa kila hali tunayokutana nayo kwenye maisha yetu ya kila siku
 
aliye kufa nae alipofika mbinguni akaona wengine wakiteketea kweny moto wa milele akasema asante mungu me nilikuwa mtenda zambi
 
Aika ruwa...
Kwa kikongo hiyo uitwa vita, ! Unajua uwa sipendi mashinikizo ya namna hii...!!! Etu tuma sms kwa watu kumi kwa ajiri ya hili ama lile , au ...sema Asante....! Lazima Asante itoke kwa moyo mkunjufu bila shinikizo....!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…