jamani nawapinga kwa 100%. Binafsi naikubali sana hospital ya ALMC kuliko hospital yoyote ile Arusha, kwangu mimi mimi imekuwa msaada mkubwa sana kwangu. sababu zifuatazo.
1. dada yangu alikuwa na tatizo la kutopata mimba, alianzia Mt. Meru kama mienzi 4 bila kujua tatizo, then tukaagizwa kwenda AICC kulikuwa na Dr. wa wanawake pale amehudhuria zaidi ya mwaka bila msaada, mwisho tukaagizwa kumtafuta Dr. msuya yeye alimfanyia baadhi ya vipimo (vingine tulivifanya kwa Dr.mohamed) havikuwepo pale hospital yake, mwisho alimwambia kuwa mirija yake imeziba na hawezi kupata mtoto kwa njia ya kawaida mpaka apandikizwe. tukiwa katika process ya kutaka afanyiwe hivyo tulikutana na mama mmoja ambaye alitushauri tunde ALMC, kweli tulienda, tulipewa appointment ya kumuona Dr. wa wanawake, kwa kweli alimsaidia leo ana watoto 2 bila kupandikiziwa mbegu. Hapo nilianza kuiamini ALMC sababa dadangu alitafuta mtoto wa muda mrefu sana.
2. Nilimpeleka mtoto wangu wa miaka 2 kutahiriwa pale, nikaonana na Dr. anayehusika na upasuaji wa watoto, yeye alinishauri lazima mtoto afanyiwe uchunguzi kabla ya kutahiriwa, kwanza nilipinga sababu niliona kama ni gharama za bure, baada ya Dr. kunieleza umuhimu nilikubali mtoto wangu afanyiwe check up kwanza. Yaaani ilikuwa kama bahati mwanangu alikuta na appendix, ni muda mrefu alikuwa akilalamika maumivu ya tumbo, nimeshampeleka hospital nyingi kila akipimwa hakuonekana ugonjwa ikafika wakati nikaona ni jambo la kawaida, kumbe mwanangu alikuwa na kidole tumbo (appendix) namshukuru Mungu alifanyiwa operation zote yaani tohara na kidole tumbo na sasa ni mzima wa afya.
3. Binamu yangu alipata ajali mwaka jana, akavunjika miguu yote miwili, alilazwa Mt. meru, Dr pale alisema mguu mmoja unafaa kuwekwa POP ila huo mwingine lazima ukatwe, tulipopata hiyo taarifa ilitusikitisha sana sababu ni kijana wa miaka 20 tu tena yatima, nilikumbuka ALMC hospital nikashauri familia tujichange akajaribu huko, jamani sijui nimrudishie Mungu nini kwa ajili yake. Dr wa mfupa pale alishangaa sana kusikia kuu mguu ule ulitakiwa kukatwa, hakuamini, alituambia mguu ule ni wa kuwekewa chuma na mgonjwa atakuwa na uwezo wa kutembea kama zamani baada ya muda. Mungu mkubwa kijana sasa ni mzima na anaendelea na masomo yake.
4. Mwaka jana nafikiri mwenzi wa 8 or 9, nilikwenda kumsalimia ndugu yangu. kufika kwake nilimkuta jirani yake ana mtoto mgonjwa. alikuwa na miaka 4, katika kuongea nae alinieleza jinsi mtoto wake anavyoumwa, ni kama vile mwanangu alivyokuwa anaumwa na tumbo, alikuwa anahudhuria kwa Dr mariamu na yeye alisema mtoto ana UTI, kila mara alimrudisha hospital Pale AICC na kupewa dawa ila tumbo liliendelea kuuma na mwisho mtoto alianza kunya damu ila docta, tena specialist hakujua tatizo la mtoto, nilimshauri aende seliani (ALMC) kweli kesho yake alienda pale, mtoto alijulikana ana appendix, alifanyiwa operation na sasa ni mzima. mtoto huyu alianza kuuwa akiwa na miaka 2 pasipo kujulikana tatizo.
Sipendi uswahili, kiukweli naipenda sana ile hospital, nawaamini madaktari wake, wanajituma, wanaweza na wana moyo. Kwangu ndiyo changuo langu ninapofikiria swala la matibabu, sasa nikuulize wewe mtoa mada hivi kweli umewai kutibiwa ALMC???????????????????????? Hayo madirisha manne uliyopita kabla ya kumuona Dr. ni yapi????????????????????????????? me najua unaanzia reception, cashier, nurce. na kila kimoja kina umuhimu wake
1. Reception - lazima ukatoe namba ya file ili utafutiwe file or kama ni mara ya kwanza uandikishwe, bila kupitia reception sidhani kama kuna mtu ataona kuwa kuna mtu amefika na anahitaji huduma, labda mganga wa kienyeji.
2. Cashier - ukalipe ela, hiyo ni kawaida kwa hospital zote kulipa ela ya kumuona docta hakuna private hospital hata moja duniani utaingia kwa Dr. bila kulipa consulatation fees, kama huwezi nenda govement hospital, unafiriki gharama za kulipa wafanyakazi utalipa kwa maneno???????????????????
3. Nurce - yaani hapo me ndio napapenda huwezi nipeleka kwa docta bila kujua uzito wangu na pressure, napenda sana jinsi ALMC wanavyozingatia huu utaratibu.
Nimalize kwa kusema, naipenda sana ALMC, nafurahi huduma zake, ingawa mimi siyo mlutheran, nawapongeza sana KKKT kwa kufungua hospital kama hiyo ambayo imekuwa mkombozi wa wakazi wa Arusha.