Sikonge tunaweza kukufuata lakini inabidi utueleze jinsi gani ya kufuata hiyo njia yako, na imebidii nikuulize hivi kutokana na maandishi yako ya jana ambayo nilikueleza faida za kupigania tunachopigania ni Sikonge na maeneo mengine ya njii hii, tusije tukalaumiana ooh kwetu hakuna umeme, ohh hakuna barabara, umeme au investor or sisi tunalima tumbakuu , watu wamechongeka nk nk . hatuna wasomi nk nk.Nafikiri hapa tukubali tumeguke.
Vyama vingi vya upinzani au wapigania uhuru walikuwa wanagawanyika katika makundi mawili. Moja ni lle la military wings na jingine ni Political Wings.
Kuna wengine mnaona kuwa mabadiliko ya kweli yataletwa kwa KUPIGA sana kelele. Haya makele wengine yametuchosha na tunasema sasa inabidi kubadilisha mwelekeo wa mapambano. Nyie mnaamini kuwa hii njia inafanya kazi ila wengine tunaona kama vile Fisi anaumezea na kuupigia makelele mkono wa binadamu ukatike.
Inawezekana mko sawa, na endeleeni kupiga kelele. Mie najipelekeka kwenye kundi la watu wanaosema 'imetosha' na sasa ni kuanza kupambana nao direct. Kama ni maandamo au chama cha upinzani. Hakuna haja ya wenyewe kwa wenyewe kuanza kutukanana. Kama unafanya hivyo basi uko kwenye pay roll ya RA.
tkKupiga kelele?? Kelele zitasaidia nini!! Nilidhani ungesema zichukuliwe hatua fulani ili kuzuia. Lakini kelele tu mtapiga wee usiku na mchana na hakuna kitachotendeka. Si umeona mwenyewe kelele za wabunge zilipolifikisha suala la Richmond!! Waliapa kuwa ikiwa serikali haitokuja na majibu ya kueleweka kwenye kikao cha Bunge lililopita wangepiga vote of no confidence kwa serikali. Mbonan hawakufanya hivyo na imo ndani ya uwezo wao? Wamebaki kulalamika tu.. Hebu jamani tuwe realistic for once..Watu wote wamo katika maslahi tu. Hakuna cha utaifa hapa..
Hao Lowassa na papa fisadi ni wapambe wako maana wanakupamba kwa kila namna ili ukamuondoe mbaya wao kule Kyela.
Mimi sijakulink kabisa na hao mafisadi bali kilichokulink na hao mafisadi ni unachoandika hapa cha kuwatetea kwa nguvu zako zote bila kujali maslahi ya nchi yetu na kuthubutu kusema eti tufukie mashimo na kusonga mbele bila kutafutia ufumbuzi madudu chungu nzima ambayo yanaitafuna nchi yetu kila kukicha. Unayoyaandika yanaonyesha kabisa hufai kupewa wadhifa wowote ndani ya nchi yetu hata ujumbe wa nyumba 10 haukufai.
Katika kipindi hiki ambacho nchi yetu inapita katika wakati mgumu kuliko wowote ule hatuhitaji Wabunge wa kufukia mashimo ili tu tusonge mbele wakati huko mbele kuna kiza cha kutisha na nyuma pia kuna madudu ya kutisha. Hatuwahitaji kabisa ndani ya Bunge letu Wabunge wenye kutaka kufukia mashimo kama wewe utakavyo.
Mkuu BUBU ATAKA KUSEMA, achana na MTANZANIA, tumemwelewa! He is simply stupid! Anataka kutatua matatizo ya Tanzania kwa remote control, akiwa London na kwa maelekezo ya mafisadi!
tk
Hayo uliyosema ni kweli, Hatua zinahitajika dhidi ya haya yanayolalamikiwa, je unaweza kupendekeza hatua yoyote mbali na zile zinazogusiwa na baadhi ya Wachangiaji; za kuanzisha vurugu, Kuchukua Ikulu au Kuingia Msituni?
Mkuu BUBU ATAKA KUSEMA, achana na MTANZANIA, tumemwelewa! He is simply stupid! Anataka kutatua matatizo ya Tanzania kwa remote control, akiwa London na kwa maelekezo ya mafisadi!
Duh leo tangu asubuhi nilikuwa naipitia hii thread kwa makini sana sikupenda kuchangia ila kufyonza elimu taratibu.
Napenda kuwapongeza wachangiaji wafuatao.
[1] Bubu Ataka kusema
[2] Masanilo
[3] mzee Mwanakijiji
[4] Mkandara
[5] Steve D
Naomba tusikate tamaa tuendelee kupiga kelele kwa nguvu zetu zote hadi kieleweke.
Tungeenda hatua kwa hatua.
1. Kila mass action lazima iwe na maandalizi na uongozi. Kwa kawaida haya hufanywa na vyama vya upinzani. Kwa kuwa nchini kwetu vyama hivyo ni dhaifu sana na haviwezi kutoa uongozi huo, inabidi tutegemee muungano wa wana harakati na wasomi ambao watatakiwa waunde forum maalum kwa ajili ya kutekeleza mass action hizo. Njia hii itaondoa zile shutuma za kawaida kuwa chochote kitachofanyika ni kutokana na mbinu za wapinzani.
2. Baada ya kupata chombo hicho, yaanze kufanyanyika maandamano ya amani. Kila panapotokea jambo ambalo linaenda kinyume na maslahi ya taifa watu washawishiwe kujitokeza na kuandama. Hatua hii itatatanguliwa na intensive education campaing kuuelimisha umma kuhusu haki zao za msingi na jinsi ya kuzidai.
3. Ikiwa serikali itajaribu kupinga au kuzuia maandamano hayo, au ikiwa yatafanyika kwa muda mrefu bila kutoa results, hapo ndio gear ya pili itatumika ya maandamano yatayoambatana na kuingia mitaani.
4. Ikiwa mpaka hapo bado mambo yatakuwa si shwari basi yaanze mapambano ya dhahiri. Kwa hali ilivyo sasa hata askari nao wanaweza kushawishiwa kuunga mkono umma kwani wengi wao pia nao wanakerwa na matokeo ya uhalifu unaoendelea.