Selelii agoma kurudi Bungeni!?

Status
Not open for further replies.

Zyansiku

Member
Joined
Jul 27, 2009
Posts
49
Reaction score
10
Wana JF,

Ni muda mrefu kidogo sijawa na mawsiliano na mtandao huu hii ni kutokana na shughuli nzito ya kuvuna mpunga inayonikabili hapa tongi (Nzega) nimeamua kuandika hili ili basi tuendelee kupata wasaa mzuri wa kutafakari mengi ambayo tumekuwa tukiyajadili kuhusiana na siasa.

Ikiwa ni wiki moja sasa imekatika toka bunge letu tukufu lianze vikao vyake mjini Dodoma katika hali ya kushangaza bado namuona Mh Selelii akiendelea kuhangaika katika jimbo la Nzega na hasa vijijini akiomba msaada wa watu kumuunga mkono ili aweze kurudi mjengoni huku akiwaomba radhi baadhi ya watu ambao anadhani wamemuhama katika kumpigia debe tena mwaka huu.

Mh yupo bize kweli kweli jimboni japo hali yake inazidi kuwa mbaya kila kukicha na katika hali ya kushangaza amekuwa akitoa lugha mbaya za matusi kwa baadhi ya viongozi wa CCM hasa anapogungundua kuwa hawamuungi mkono.

Naomba wote walio karibu na Mh Selelii mshaurini arudi mjengoni tunamuhitaji sana lakini pia nitoe pongezi kwa Dr Kigwangala mbunge mtarajiwa wa Nzega maana amembana kweli kweli Selelii
 
Zyansiku
10th August 2009 09:18 PM
Jamani simuelewi SS na sitamuelewa kabisa! simuelewi kwa sababu amekuwa akilalamika sana kuwa kundi la mafisadi linamwaga misaada majimboni ili kuwaangusha wale wanaopambana na ufisadi,

Mwenye macho haiambiwi ona, mkuu una post 41 zote zinamponda au mkejeli Samwel Sitta na Lucas Seleli. Mwenye macho anaona na kuujua ukweli, fisadis at work!.
 

Mijitu mingine sijui ikoje, inakuhusu nini? wewe nenda kawaambie waliokutuma kiama chao kipo karibu
 

Zyansiku wewe ndio huyu Dr Kigwangala! Unafaa kuogopwa kama ukimwi! Selelii ni mpiganaji wetu. Ameendika historia Tz. Wewe pamoja na hao waliokutuma hatukutaki!
 
haha ha ha JF mpo makini sana kumbe. Nemesis hahaha asante
 
Huyu mtu vipi? Mbona humsemi Rostam unayeonekana kumpigia debe -- kwa kukosa vikao vingi tu vya Bunge, na pia huwa hachangii katika mijadala wala kuuliza maswali?
 
Mwenye macho haiambiwi ona, mkuu una post 41 zote zinamponda au mkejeli Samwel Sitta na Lucas Seleli. Mwenye macho anaona na kuujua ukweli, fisadis at work!.

Hapo mkuu umemkamulia ndimu kwenye kidonda! Bravo!
 
Unajua wakati nasoma heading ya posts nilipoiuona hii nilishtuka sana nikawaza inamaana selelii ametangaza kutogombea? haraka nikaingia kuona kulikoni loooh bora ningeendelea na posts zingine kuliko kukutana na huyu kibaraka wa mafisadi

wewe unajua kazi ya kuvuna mpunga lakini ilivyo ngumu? usingepata hata muda wa kuona selelii anazungumza nini na watu hao ....wewe hauko shambani upo nyuma ya selelii unamfuatilia
Halafu waliokutuma watakudai hela yao huwezi kuandika post ki bias kiasi hili ukadhani wasomi wa JF hawatakung'amua....yani unamponda selelii halafu unasema siju Dr nani mbunge wetu mtarajiwa!!!! rudi shule ukasome zaidi itakusaidia zaidi kujua namna ya kuzunguka mbuyu
Mix with yours
 
namfananisha zyansiku na kibwengo!!!
 
Zyansiku wewe ndio huyu Dr Kigwangala! Unafaa kuogopwa kama ukimwi! Selelii ni mpiganaji wetu. Ameendika historia Tz. Wewe pamoja na hao waliokutuma hatukutaki!
Mmmmmmmhhhhhh umeamua kumpa ya uchi uchi isiyo na nguo huyu fisadi?
Hutamuona tena hapa. Kesha kimbia kivuli chake.
 
Mwenye macho haiambiwi ona, mkuu una post 41 zote zinamponda au mkejeli Samwel Sitta na Lucas Seleli. Mwenye macho anaona na kuujua ukweli, fisadis at work!.

Mkuu thanks for doing the needful, this person deserves to be in our ignore list!!!
 
Right on Guys....Tuna watu makini sana hapa....now we know who are the hyenas in sheep's skin..
 
Mwenye macho haiambiwi ona, mkuu una post 41 zote zinamponda au mkejeli Samwel Sitta na Lucas Seleli. Mwenye macho anaona na kuujua ukweli, fisadis at work!.


Mkuu upo makini, i like it
 
uyo anaweza kuwa ni Rostam azizi, manji, kundi la el etc....si unaona argument zake zilivyo cheap!
 
Kaacha mpunga unaliwa na ndege kaleta umbea! Utakufa njaa
 
Ahsante sana Zyansiku kwa kunifagilia na kunipa pongezi.
Wengine wanadhani mimi na wewe tuna ubia, naomba tu kusema hapa kwamba sikufahamu wala sijawahi kuwasiliana na wewe wala kujadili lolote lile kuhusu azma yangu ya kuwania Ubunge Nzega! Naomba tu pia niwataarifu ndugu zangu wanaJF kwamba mimi sina ubia na mtu yeyote yule katika harakati zangu za kuwania Ubunge, sijaombwa na wazee, sijatumwa na mtu yeyote yule - ila ni nafsi na dhamira yangu pekee iliyonituma kuutafuta Ubunge wa Nzega!

Jimbo la Nzega lina mtego tu kwamba yeyote atakayejitokeza kugombea basi atadhaniwa kuwa ametumwa na mtu, hususan akiwa na ushawishi na anakubalika zaidi ya Selelii! Hili lilijitokeza hata pale nilipoamua kutangaza nia yangu kwa umma kupitia vyombo vya habari, pale Habari maelezo! Hili linakuja kutokana na Selelii kujipambanua kama ni mbunge shupavu anayepambana na ufisadi! Wengi wanakuja kufikiri kwamba jimbo la Nzega lina maslahi ya watu fulani wanaoitwa mafisadi...na kwamba yeyote anayempinga Selelii basi anaungwa mkono na au ametumwa na hawa watu.....and this is a big misnomer! Kugombea Uongozi ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania, na hatuwezi kuliacha jimbo chini ya Selelii kwa kuhofia kusemwa tumetumwa! Tayari kuna watu zaidi ya watano wamekwishatangaza nia ya kuwania Jimbo la Nzega. Hivi wote hawa ni vibaraka wa mafisadi?

Regards,
Dr. Hamisi Kigwangalla.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…