Selective Prosecution AU PERSECUTION: Takukuru na rushwa

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
52,980
Reaction score
104,399
Jana nimeona video clip ya Mwanajeshi (afisa Takukuru?????) akimtafuta Hans Pope na Lawuo.... kwa tuhuma za rushwa huko Simba S.C na TRA in connection with kukwepa kodi!
Najiuliza Makonda na makonteina si alikuwa na nia ya kukwepa kodi au amekwepa kodi tayari; na ni jinai, mbona haguswi? mbona hajatafutwa?
SELECTIVE PROSECUTION OR PERSECUTION?
 
Una update jambo lililoongelewa na kufikiwa uamzi?

Labda nikusaidie kuhusu sheria inavyotaka: Hauwezi kufanya kosa kwa kisingizio cha kosa jingine! Ama ukafanya kosa kwa kutumia utetezi wa kosa jingine.

Kwa mfano: mnaweza kutenda makosa ya wizi katika matukio mawili tofauti, kisha katika utetezi wako, ukasema 'mimi mnanitia hatiani na kunifunga kwa kosa la wizi, mbona fulani naye aliiba tena zaidi yangu, lakini akaachiwa huru?

Kama ni makontena, jadili makontena, kama ni utakatishaji fedha ama ukwepa kodi wa viongozi wa simba, basi jadili hilo.

Siyo mada ya issue 'A' unaipeleka kwenye mada ya issue 'B', jikite kwenye issue uliyoiweka mezani.
 
Nadhani katiba yetu inasisitizia haki sawa kwa kila mwananchi.
 
Reactions: Auz
Hakuna haki sawa kwenye kesi mzee!
Hujaelewa hoja.Wanachosema hapa ni kuwa kuna wengine walighushi vyeti wakaambiwa wapige kazi wakati wengine wamefukuzwa kazi na mafao wamenyimwa.Kuna wengine wamekwepa kodi ya TRA na bado wanatembea vifua mbele na wengine wanatafutwa
 
umenifilisi mkuu' huyo alichokifanya inaitwa fallacy in reasoning, attaching irrelevant issue to main topic
 
Hujaelewa hoja.Wanachosema hapa ni kuwa kuna wengine walighushi vyeti wakaambiwa wapige kazi wakati wengine wamefukuzwa kazi na mafao wamenyimwa.Kuna wengine wamekwepa kodi ya TRA na bado wanatembea vifua mbele na wengine wanatafutwa
Mkuu nimeelewa vizuri sana.
Lakini wewe ndiye haujanielewa nadhani ni jinsi ya uandishi nilioutumia.
Nimemaanisha kuwa hakuna usawa katika masuala yahusuyo sheria. Mwaweza kutenda kosa lilelile la aina moja navkatika tukio moja, lakini wewe ukafungwa na mwenziyo akaonywa ama kushinda kesi.
Huo mfano uliotolea wa vyeti ghushi, usidhani ulipukutisha waajiriwa wote serikalini, hakuna.
Linapokuja suala la kisheria katika kutafuta haki huwa haliwekwi kiujumlajumla kama siasa.
 
Hapo sawa.Hatujasema kuwa Dkt.Hans Pope hajafanya kosa.Tunachokemea ni double standard katika kusimamia sheria.Wanasheria wanamsemo kuwa haitoshi haki kutendeka bali ionekane kutendeka pia.
 
La Makonda sio ukwepaji kodi. Nakonda alikuwa anaomba msamaha wa kodi. Akanyimwa. Hilo sio kosa. Mtu yeyote, kwa kujua au kutojua sheria anaweza kuandika barua tra kuomba atendewe jambo lolote kuhusu kodi. Kama sheria hairuhusu atakataliwa. Na atalazimika kulipia kodi mzigo wake. Ndio kilichotokea kwa Makonda.
Angekwepa kodi kama angesamehewa halafu akatoa mzigo na kuupeleka kuuza.
 
Halafu mjue .mmoja ni msukuma (kanda ya ziwa) mwingine( MHEHE nyanda za juu kusini) hivyo ni vitu viwili tofauti
 
Nafikiri tukubali tu kuwa katika nchi yetu, hakuna haki, hakuna utawala wa sheria.
Utapata haki kutegemeana na nafasi yako katika siasa ndani ya ccm
Sheria itafuatwa na hasa kutumiwa kukukandamiza, unapokuwa ama ndani au nje ya siasa, lakini zaidi ukiwa nje ya ccm.
 
Never, alidanganya kuwa ni furniture za walimu while it was not! What was the motive behind? Barua yake ilisemaje anaomba msamaa wa kodi kwa ajili ya furniure za walimu! Alisema ni misaada toka USA, while hakuna uthibitisho wowote, NO iota of any cogent evidence kuwa ilikuwa misaada ya walimu!
 
Go deep and get the main take home msg from my thread.... we conderm selective prosecution and I am not saying Hans Pope should be spared, NEVER! . Nadhani kuna mtu kakujibu vizuri!
 
Makonda kakoswa vyeti feki kwa sababu zoezi lilihusu watumishi na yeye ni kiongozi wa kuteuliwa,
Saivi unaambiwa eti hana hatia kwa sababu ni kama mtu aliyeomba kusamehewa ila hajakubaliwa na hapa unaweza jiuliza ni kwa nini mpaka mzigo ufike? kuna bla bla nyiiiiiiing ila wengine wakihisiwa jambo utashangaa wanapimwa mkono ndo ujue kuna double standard kwenye utekelezaji wa sheria
 
Simtetei ila nilijikita kweywe sual la kodi. Kwamba maadam barua yake ilikataliwa bado huo sio ukwepaji kodi.
 
Deadly wrong!!! Huyo amedanganya kuwa ni vifaa vya shule wakati ni masofa na hili hata rais alilisema openly.
 
Hujaelewa hoja.Wanachosema hapa ni kuwa kuna wengine walighushi vyeti wakaambiwa wapige kazi wakati wengine wamefukuzwa kazi na mafao wamenyimwa.Kuna wengine wamekwepa kodi ya TRA na bado wanatembea vifua mbele na wengine wanatafutwa
asante, that is my essential take home message!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…