Kumekuwa na tabia ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga Vyuo Vikuu kwa Mwaka wa masomo 2015/2016 kuweka Thread zao na kuanza kuuliza taarifa za Vyuo husika. Hii ni nzuri kwa kuwa unajaribu kupata updates na uzoefu kabla hujaenda Chuoni. Nawaomba wote mliochaguliwa Vyuo Vikuu tembeleeni Website za Vyuo mlivyopangwa na Kudownload PROSPECTUS ya CHUO ambayo hutoa information zote pamoja na Masomo utakayoyasoma kutoka unapoanza chuo mpaka unatakapohitimu. Inatoa taswira nzima ya mazingira ya Chuo kitaaluma na nje ya taaluma. Utajua Idara ya Program uliyochaguliwa. Inatoa mwelekeo mzima wa maisha ya chuo kiafya na hata kwa malazi na chakula. Jengeni utamaduni wa kuanza kusoma PROSPECTUS. Pia kuna vyuo vina UNIVERSITY POLICIES, UNIVERSITY BY LAWS, EXAMINATION BY LAWS Anzeni kuzisoma mapema ili kuondoa sintofahamu iliyojengeka ndani ya mioyo yenu. Nawatakieni kila la heri,. Kumbukeni Kumtangulizeni MUNGU katika masomo yenu..