maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,345
- 15,852
Selcom kama kazi ya kuhudumia watanzania imewashinda mtafute kazi nyingine. Haiwezekani nifanye muamala tangu jana na pesa isiingie kwenye simu badala yake mnasema funds will be credited within 30 minutes wakati my bank account has been debited with the same.
Hii si mara ya kwanza kutokea na mbaya zaidi ni hadi mtu aende bank kujaza form. Sasa mimi niko safarini vijijini kufuata mzigo na nimeshindwa kulipa kwa sababu yenu.. Mtanilipa fidia? Nimeingia hadi kwenye website yenu kuangalia namna ya kuwapigia baada ya mtandao wangu kudai pesa mmeishikilia ninyi lakini ajabu hakuna sehemu mmeandika namba ya kuwasiliana nanyi kutatua matatizo kama haya. Mbona mnafanya kazi kama mnahudumia ng'ombe?
Last time mmenirudishia pesa baada ya mhudumu wa benki kusumbuana sana nanyi kwa email na kwa simu. Sasa kwa tunaokua mbali na bank tushindwe kuhudumiwa kwa sababu ya utaratibu wenu mbovu? Kwani hamjui bank zipo sehemu chache sana kwa nchi hii na tulitegemea ninyi ndio mtakua mkombozi wa matatizo haya?
Tafadhali tafadhali naomba mamlaka husika iwamulike hawa. Haiwezekani system zenu zisiwe na uwezo wa kujua pending transactions.. Au ni hujuma tu?