Wont be the same
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,564
- 2,483
Chama cha NCCR Mageuzi kimeeleza kuwa hakitasusia uchaguzi Mkuu wa baadae mwaka huu, wakieleza wazi pia mpango wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kutaka kuzuia uchaguzi ni suala ambalo haliwezekani.
Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Joseph Selasini amekiri kusema kuwa kuzuia uchaguzi ni ndoto za mchana zisizoweza kutimia, akisema Chadema pia imeshindwa kuwa na mkakati wa wazi katika kueleza ni namna gani watazuia uchaguzi, akisisitiza umuhimu wa kujiepusha na baadhi ya maneno nyakati hizi za maandalizi ya uchaguzi kwani zitakiweka Chama na Wanasiasa wao kwenye nafasi mbaya mbele ya vyombo vya dola.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Alipoulizwa na Mwandishi wa Jambo TV kuhusu matumizi ya nguvu ya Umma kwenye kuuzuia uchaguzi,Selasini ameeleza kuwa hakuna chama chenye uhakika wa matumizi ya nguvu ya umma, akikumbusha namna ambavyo kumetokea mfululizo wa maandamano kufeli yaliyokuwa yakiitishwa na vyama vya upinzani nchini.
Source: Jambo TV