Sekunde Bilioni 2.2 Zinavyowazuzua Wanadamu!!

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Ukiachilia mbali vifo vya mapema! Umri wa kawaida wa mwanadamu hapa duniani kwa mujibu wa maandiko matakatifu ni miaka 70.

Pamoja na kwamba huu si umri mkubwa kivile, hata hivyo walimwengu tumekuwa tukijidanganya kuwa; bado tuna muda mrefu wa kuwapo katika sayari hii tata!
Kimsingi hii ndiyo sababu kuu inayopelekea wengi wetu kujirimbikizia mali ilihali wenzatu wakifa kwa sababu ya ufukara wa kupindukia!

Katika kulitafakari hili kuhusu sababu hasa inayopelekea sisi kujidanganya kiasi hiki cha kutisha! Kuona eti bado tuna maisha marefu hata kama tuwe tumebakiza siku moja tu!
Mimi niligundua kwamba tatizo linalotusumbua hapa ni lile jina mwaka au miaka! Hiki ni kitu ambacho tunadhani kuwa ni kirefu sana!

Sasa basi mimi nilijitahidi sana kutafuta dawa yake, kwa kuundoa umri wetu katika miaka na kuuweka katika jumla ya sekunde!
Na nikafanya hesabu hii:

Saa moja ina sekunde........ 3600

Siku moja ina sekunde .......86,400

Mwaka mmoja sekunde...... 31,536,000

Miaka sabini sekunde......... 2,207,520,000.

Hivyo basi badala ya kusema tunaishi miaka sabini duniani ni vizuri ukaelewa kuwa hiyo miaka ni sawa na sekunde 2,207,520,000 tu!

Baada ya kulifahamu hilo hebu sasa jiulize kuwa tangu uzaliwe mpaka siku ya leo tayari umeshakata sekunde ngapi kutoka kwenye hiyo idadi hapo juu?

Na tangu uanze kusoma ujumbe huu zitakatika ngapi mpaka utakapomaliza.

Nadhani sasa umefahamu kwamba mimi na wewe hatuna maisha marefu hapa!
Kimsingi ni wewe uliyekuwa hujui kwamba hatukuja hapa duniani kuishi; vinginevyo maisha yenyewe yalivyo mafupi hayana maana yoyote!

Ni kweli kwamba duniani humu kuna wasomi na wasiosoma, matajiri na masikini, waliofanikiwa na wasiofanikiwa! Lakini kinachoshangaza ni kwamba mara baada ya sekunde hizi bilioni 2.2 kupita; matabaka haya hugeuka na kuwa sawa kwa kila kitu!

Wote huwa makaburini, wote huwa hawajui rugha yoyote, wote huwa hawafundishiki, wote huwa mifupa mikavu!

Mwisho ukumbuke kuwa tumekuja duniani kufanya uchaguzi tu na si vinginevyo!
Kuchagua mema au mabaya.
Kumchagua Mungu au Shetani.
Kumchagua Kristo au Mtume.
Kuchagua Upendo au Chuki.
Kuchagua Amani au Vita.
Kuchagua Kuponya Watu au Kuwaua!
Kuchagua Kiburi au Unyenyekevu

Chaguo ni lako!

Uwe na sekunde njema za leo!
 
Uuuwoiiiiiiiie, yeuwiiiiiiiiiiiiie, auwiiiiiiiiiiiiiiiieee, staki kufa mie
 
Sasa nzi na mbu wakifanya hesabu nao itakuwaje....maisha ndio haya haya... enjoy kadri uwezavyo. Je unajua ulikuwa nani au kitu gani kabla haujazaliwa??? Why should u care where u are going??
 
1470680045062.jpg
 
Wakati ukuta,kila sekunde uitumie kuwafariji wanaokuzunguka.bila kujali hali yako.kuna wanaotamani hata hicho ambacho wewe unakiona kidogo.
 
Ukiachilia mbali vifo vya mapema! Umri wa kawaida wa mwanadamu hapa duniani kwa mujibu wa maandiko matakatifu ni miaka 70.

Pamoja na kwamba huu si umri mkubwa kivile, hata hivyo walimwengu tumekuwa tukijidanganya kuwa; bado tuna muda mrefu wa kuwapo katika sayari hii tata!
Kimsingi hii ndiyo sababu kuu inayopelekea wengi wetu kujirimbikizia mali ilihali wenzatu wakifa kwa sababu ya ufukara wa kupindukia!

Katika kulitafakari hili kuhusu sababu hasa inayopelekea sisi kujidanganya kiasi hiki cha kutisha! Kuona eti bado tuna maisha marefu hata kama tuwe tumebakiza siku moja tu!
Mimi niligundua kwamba tatizo linalotusumbua hapa ni lile jina mwaka au miaka! Hiki ni kitu ambacho tunadhani kuwa ni kirefu sana!

Sasa basi mimi nilijitahidi sana kutafuta dawa yake, kwa kuundoa umri wetu katika miaka na kuuweka katika jumla ya sekunde!
Na nikafanya hesabu hii:

Saa moja ina sekunde........ 3600

Siku moja ina sekunde .......86,400

Mwaka mmoja sekunde...... 31,536,000

Miaka sabini sekunde......... 2,207,520,000.

Hivyo basi badala ya kusema tunaishi miaka sabini duniani ni vizuri ukaelewa kuwa hiyo miaka ni sawa na sekunde 2,207,520,000 tu!

Baada ya kulifahamu hilo hebu sasa jiulize kuwa tangu uzaliwe mpaka siku ya leo tayari umeshakata sekunde ngapi kutoka kwenye hiyo idadi hapo juu?

Na tangu uanze kusoma ujumbe huu zitakatika ngapi mpaka utakapomaliza.

Nadhani sasa umefahamu kwamba mimi na wewe hatuna maisha marefu hapa!
Kimsingi ni wewe uliyekuwa hujui kwamba hatukuja hapa duniani kuishi; vinginevyo maisha yenyewe yalivyo mafupi hayana maana yoyote!

Ni kweli kwamba duniani humu kuna wasomi na wasiosoma, matajiri na masikini, waliofanikiwa na wasiofanikiwa! Lakini kinachoshangaza ni kwamba mara baada ya sekunde hizi bilioni 2.2 kupita; matabaka haya hugeuka na kuwa sawa kwa kila kitu!

Wote huwa makaburini, wote huwa hawajui rugha yoyote, wote huwa hawafundishiki, wote huwa mifupa mikavu!

Mwisho ukumbuke kuwa tumekuja duniani kufanya uchaguzi tu na si vinginevyo!
Kuchagua mema au mabaya.
Kumchagua Mungu au Shetani.
Kumchagua Kristo au Mtume.
Kuchagua Upendo au Chuki.
Kuchagua Amani au Vita.
Kuchagua Kuponya Watu au Kuwaua!
Kuchagua Kiburi au Unyenyekevu

Chaguo ni lako!

Uwe na sekunde njema za leo!
Umeeleweka ndugu, wenye akili wamekuelewa sana.
 
Ujumbe murua sana huu.

We are all travellers on earth... with undefined destination!

-Kaveli-
 
mkuu unatuongezea stress tu.kila mtu akifikiria kufa hakitaenda kitu.
kuwaza unakufa lini ni kuyakumbusha mauti kufanya kazi yake!#
 
Dah!!! Umepiga penyewe kabisaaa means always after hizo 2.2 biln seconds hakuna cha mguu wa bia, mahips, timba, ndevu umbo "O", six packs, dimpoz,...... Daaah ni vyema kuwa karibu na Mungu.
 
Ndo maana waafrika atuendelei
mzungu kila siku anaiba huko uarabuni kwani yeye haogopi kufa. Acha mawazo mgando tafuta mali tu kama mzungu sio kila siku Magu kabana kila kitu tumia akili
 
Back
Top Bottom