Sekta za Elimu na Afya zinakwamisha na Ofisi ya Rais

Mr Emmy

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,219
550
Katika harakati za kuingia Ikulu ya Magogoni kuwatumikia Watanzania kwa Moyo wa kweli Rais Magufuli aliahidi kuboresha huduma za afya na elimu kwa kuhakikisha rasilimali watu na fedha zinapatikana kwa wakati.

Mpango wa Rais Magufuli wa kuhakikisha sekta ya Afya na Elimu inakuwa na Rasilimali watu wa kutosha unahujumiwa na watumishi wa Ofisi ya Rais Utumishi wanaoshughulikia utoaji wa vibali vya nafasi mpya katika bajeti za mishahara.

Katika hali ya kushangaza Utumishi imewaita Maafisa Utumishi kutoka Mikoani na Halmashauri kuja Dar eti kuondoa nafasi zote walizokuwa wametenga kwa ajira mpya katika sekta ya afya na elimu kwa kusingizia eti kwamba serikali haina fedha za kulipa mishahara kwa ajira mpya.

Kwa mfano halmashauri X iliomba nafasi mpya 154 kwa watumishi wa kada za Afya kulingana na mahitaji halisi ya Hallmashauri Husika lakini Ofisi ya Rais Utumishi kupitia Bw Mlay wameitaka halmashauri hiyo kupunguza nafasi hizo hadi kufikia 9 tu je hapa kuna logic kweli ya kuboresha huduma za Afya????????

Kutokana na Elimu Bure kuandikisha wanafunzi wengi sana Halmashauri Z iliomba nafasi mpya 222 za kuajiri walimu lakini Ofisi ya Rais Utumishi imepunguza nafasi hizo kutoka 222 hadi 13 je hapa OR- Utumishi chini ya waziri Kairuki na Bw Mlay hawahujumu kasi ya Dr Magufuli kuboresha sekta ya Afya na Elimu??????

Leo hii kuna malalamiko makubwa ya upungufu wa Madaktari, wauguzi, wahudumu wa afya, watalaam wa maabara, tabibu, wafamasia katika hospitali za mikoa, wilaya,vituo vya afya na Zahanati, upungufu huo unawafanya baadhi ya watumishi waliopo kulemewa na kazi na kuwakwaza wahitaji huduma ambao ni wananchi.

Kitendo cha Utumishi kusingizia ukomo wa bajeti kupunguza ama kuondoa kabisa nafasi zilizotengwa na Mikoa na Halimashauri kwa ajili ya kuajiri watalaam katika sekta ya AFYA na ELIMU ni HUJUMA nzito kwa Dr Magufuli; na tunapendekeza wahusika kama Bw Mlay na wenzake wachukuliwe hatua kwa hujuma wanazowafanyia wananchi.

Note kuna halmashauri nyingi tu ambazo zimepewa nafasi 0 kabisa za kuajiri watumishi wa afya na elimu na OR- Utumishi

Mwisho watalaam wa Kada za Afya na Elimu kwa sasa wapo katika soko la ajira hivyo
 
tulipokuwa tunakusanya bil900 pesa ilikuwepo sasa tri 1.7 hakuna pesa, huyu Mlay atakuwa anatokea mkoa gani? hawa watu sijui wanamtafuta nini JP.
 
Katika baraza la mawaziri jipya kuna kadhaa wameonyesha aina ya uongozi wenye tija kutokana na walivyoanza sisemi ndio bora hila wako realistic zaidi only time itaonyesha mafanikio yao.

Nape Nnauye baada ya kukabidhiwa ofisi alisema anataka mabadiliko, lakini ata yeye anatambua ana limitations kutokana na resources hivyo awezi kuwataka watu wafanye mambo ambayo yako juu ya uwezo wao kifedha hila watafanya tathmini ya pamoja na kuja na agenda zao.

Mwigulu huyu nasikia kutoka kwa baadhi ya watu kafungua uwanja wa mapendekezo anatumia wataalamu wake, wafanyakazi wengine serikarini ambao ni watekelezaji wa sera za serikari kuona nini kinatakiwa kufanyika na wadau wa diaspora kupokea mapendekezo ya wizara sehemu yoyote ambayo inaweza saidia kuleta mabadiliko ya ufanisi (not confirmed hila ndio wanavyodai)

Mwijage huyu ameonyesha ni mmbunifu hila hapa kwenye sukari kama analazimisha ngamia kupita kwenye tundu la sindano.

Hali halisi ni kwamba uwezo wa serikari kuajiri wafanyakazi wapya ni hafifu sana ukiangalia tu makusanyo ya kodi karibu ya nusu inaenda kulipa mishahara ya wafanyakazi sasa sijui kiasi gani inaenda kwenye utekelezaji wa sera zake. Kuongeza anymore wafanyakazi kwa hali ya sasa ni kujitafutia matatizo. Halikadhalika kuna watu wengi wameajiriwa maofisini awazalishi na hawana umuhimu kama walimu, wafanyakazi wa sector ya afya na wengineo ambao wako field directly wanatumikia jamii ana kwa ana kila siku kwenye shughuli za serikari.

Hawa jamaa inabidi warudi kwenye drawing board tumeona ziara ya raisi wafanyakazi tano sijui wangapi awako kazini siku ya kazi, uchelewaji wa wafanyakazi, etcetera with waste of resource ambazo serikari aina budi bali sasa kuanza kuangalia namna ya kufuta ajira kadhaa za administration bila ya kuathiri kazi zao kwa watu ambao kwanza wana mishahara mikubwa na nafasi zao azina impact kubwa.

In short agenda ya raisi/ilani yao ya chama or whatever the source of central policies inabidi kipindi hiki ifanyiwe kazi upya kuanzia budget wise, implementation yake na watu sahihi kushika nafasi kwa sasa ni mzunguko na watu kubahatisha wakati system mbovu, mipango ya matumizi aiko sawa na kila kitu ambacho sio sahihi kufanya good governance kimekuwa wazi. Kwa mfano wewe ujapanga budget ya kununua ndege halafu mara bin vup umeibuka umetenga hela ya ndege kutoka kwenye budget hiyo hiyo unadhani hakuna sehemu itaathirika kweli, ina maana na washauri wenyewe pia majipu vile vile walau wangesema kwenye budget ijayo tutatenga.
 
Hapo kwenye kada ya elimu hakuna upungufu wa walimu labda kwa upande wa walimu wa sayansi. Walimu wa masomo ya sanaa wamejazana hadi kufundisha kwa kugawana subtopics. Mtu anakaa miezi miwili hajaingia darasani akisubiria mwenzake amalize topic nda na yeye afundishe topic yake.
 
mbona sielewe.....juzi tu nilimsikia waziri mkuu anasema wataajiri walimu elf40 mwaka huu...kwa hyo wameahirisha au wamepunguza idadi
 
Bajeti huwa chini ya wizara gani?

Inakuwaje kama wizara husika imeiambia Utumishi kuwa bajeti hakuna????

Unataka utumishi wafanyaje???
 
Hapo kwenye kada ya elimu hakuna upungufu wa walimu labda kwa upande wa walimu wa sayansi. Walimu wa masomo ya sanaa wamejazana hadi kufundisha kwa kugawana subtopics. Mtu anakaa miezi miwili hajaingia darasani akisubiria mwenzake amalize topic nda na yeye afundishe topic yake.
research yako uliifanyia naeneo gani....ulihusisha shule zp primary au sec...unaweza kuanisha ni masomo gani ya art na topic gani zimegawanywa....yani wabongo kwa wivu hawajambo
 
tulipokuwa tunakusanya bil900 pesa ilikuwepo sasa tri 1.7 hakuna pesa, huyu Mlay atakuwa anatokea mkoa gani? hawa watu sijui wanamtafuta nini JP.
HIYO FEDHA IMEKUSANYWA LINI NA BAJETI TUNAYOTUMIA NI YA LINI WE NYUMBU????????????????
 
Hapo kwenye kada ya elimu hakuna upungufu wa walimu labda kwa upande wa walimu wa sayansi. Walimu wa masomo ya sanaa wamejazana hadi kufundisha kwa kugawana subtopics. Mtu anakaa miezi miwili hajaingia darasani akisubiria mwenzake amalize topic nda na yeye afundishe topic yake.
NA WAKISHAAJIRI WALIMU 40000 MWAKA HUU(KWA MUJIBU WA SIMBACHAWENE NA MAJALIWA) TATIZO LA WALIMU LITAKUWA LIMETATULIWA KWA 98%
 
research yako uliifanyia naeneo gani....ulihusisha shule zp primary au sec...unaweza kuanisha ni masomo gani ya art na topic gani zimegawanywa....yani wabongo kwa wivu hawajambo
Wewe ni mwalimu???????
 
research yako uliifanyia naeneo gani....ulihusisha shule zp primary au sec...unaweza kuanisha ni masomo gani ya art na topic gani zimegawanywa....yani wabongo kwa wivu hawajambo
Hakuna cha wivu hapo huo ndo ukweli jaribu kuwapigia hata ndugu na jamaa wako ambao ni walimu wakwambie hali ilivyo. Alafu kwa nini mwanaume mzma unapenda kusoma Kuswahili na historia? Ona sasa unavyoishi kwa wasiwasi ukitegemea huruma za serikali kama ikiona iwasaidie tu.
 
Ili kuboresha huduma hizo ni vema kurekebisha maslahi ya watumishi waliopo kwanza, haina tija kuajiri wengi wakati kuna malalamiko kibao ya mishahara duni, madeni, upandaji madaraja. PAYE kubwa kuliko nchi yoyote Afrika mashariki nk
 
Kwa kifupi mtoa mada..ajira hutolewa kutokana na bajeti iliyopo na si mahitaji tu ya wafanyakazi. Bajeti ya utumishi sio ajira mpya tu bali pia kuboresha maslahi ya wafanyakazi na kupandisha vyeo wafanyakazi..promotion..usidhani hata hao JPM na Majaliwa hawajui wanafahamu kuwa kuendesha serikali sio mchezo. Trilioni zinazokusanywa ni chache bado kwa mahitaji halisi ya uendeshaji wa serikali.

Kila kitu kiende kwa mipango kama ilivyo pangwa kabla. Ukitaka kila hitaji likamilike kwa matakwa ya kila mahala basi ujue fika serikali ya mpenndwa wetu JPM haitaweza kamwe. Ajira zinazotolewa ni kwa mujibu na uwezo wa serikali uliokuwepo wala sio huyo Mzee Mlay kama unavyomtaja. Anajibu kwa niaba ya serikali na si matakwa yake kwani yeye nani hasaa.??mtoa mada ushauri kidogo kwako..soma Government standing Order utafahamu mambo mengi juu ya ajira na upandishwaji vyeo wafanyakazi serikalini..
 
Back
Top Bottom