Sekretarieti ya maadili: Uwasilishwaji wa hati za mali madeni unasuasua, rais Samia awasilisha

Kiturilo

JF-Expert Member
Sep 27, 2021
709
2,858
Kamishina wa tume ya maadili nchini Jaji Sivangilwa Mwangesi amesema kati ya watumishi 15,000 wanaotakiwa kuwasilisha hati zao kwenye tume ni watumishi 120 tu mpaka sasa waliowasilisha hati zao ikiwemo rais Samia Suluhu!

Jaji Sivangilwa amempongeza Rais kwa kuwasilisha hati ndani ya muda huku akishangazwa na watumishi wengine walioshindwa hadi na rais ambaye ana majukumu mengi. Mwisho wa kuwasilisha hati ni tarehe 31/12/2021.

===

Rais Samia awasilisha hati ya mali na madeni kwa Sekretarieti ya Maadili​

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassam amewasilisha hati ya tamko la viongozi wa umma kuhusiana na mali na madeni waliyo nayo kwa mwaka 2021 kwenye Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Taarifa hiyo imetolewa leo Desemba 3, 2021 na Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa umma, Jaji Sivangilwa Mwangesi wakati akizungumza na waandishi wa habari, ikiwa ni njia ya kuwakumbusha viongozi wa umma ambao hawajawasilisha hati hizo kufanya utaratibu huo mara moja.

Amesema takwa hilo ni kwa mujibu wa sheria No.13 ya mwaka 1995 sura ya 398 ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwataka kuwasilisha hati hizo kwa Kamishna wa maadili.

Amesema kwa mwaka 2021, uwasilishaji data ulianza Oktoba mosi, 2021 mpaka 31, Desemba ambapo viongozi wanatakiwa kuwasilisha tamko hilo.

“Kati ya wale waliowasilisha mpaka sasa hivi ni Rais wa Tanzania ambalo tamko lake limewasilishwa Novemba 29 Kanda ya Dar es Salaam, ambapo hapa makao makuu limewasilishwa jana,” amesema Jaji Mwangesi.

Akizungumzia hali ya utekelezaji wa takwa hilo amesema viongozi hao wameonekana kusuasua, kwani hadi mwishoni mwa Oktoba waliokuwa wamewasililisha tamko lao ni Kanda ya kati 28, Dodoma 6, Kanda ya Kusini 7, Kanda ya Kaskazini 11, Nyanda za juu Kusini 20, Kanda maalumu 53, Magharibi 18, Mashariki 8 na Kanda ya Ziwa 16.

Amesema idadi hiyo inasuasua kwa kuonekana bado kuna pengo kubwa la uwasilishaji huo kwani viongozi wanaotakiwa kupeleka ni zaidi ya viongozi 15,300.

“Kama Kiongozi wa nchi anajua majukumu yake mapema basi ni vema viongozi waliobaki nao wafate nyayo zake, kwani muda uliobaki ni mchache,” amesema.

Jaji Sivangilwa amesema kutokurejesha wasilisho hilo ni kosa chini ya kifungu cha 15 cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma ambapo sheria inaruhusu kuwapeleka viongozi wasiowasilisha tamko lao katika Baraza la maadili kuweza kuwatolea maamuzi.

Mwananchi
 
Kamishina wa tume ya maadili nchini Jaji Sivangilwa Mwangesi amesema kati ya watumishi 15,000 wanaotakiwa kuwasilisha hati zao kwenye tume ni watumishi 120 tu mpaka sasa waliowasilisha hati zao ikiwemo rais Samia Suluhu!
Jaji Sivangilwa amempongeza rais kwa kuwasilisha hati ndani ya muda huku akishangazwa na watumishi wengine walioshindwa hadi na rais ambaye ana majukumu mengi. Mwisho wa kuwasilisha hati ni tarehe 31/12/2021.

Rais Samia awasilisha hati ya mali na madeni kwa Sekretarieti ya Maadili | Mwananchi - Rais Samia awasilisha hati ya mali na madeni kwa Sekretarieti ya Maadili
Rais wa mfano kwetu....
Rais bora mwenye uadilifu na anayekwenda na wakati.....

Tanzania imepata bahati kubwa mno kuwa na CHIFU HANGAYA🙏

Kongole kwake Amiri Jeshi wa Majeshi ya Ulinzi na usalama mh.Rais msikivu Samia Suluhu Hassan 💪

#SiempreJMT👊
#NchiKwanzaKablaYaNafsiZetu🙏
 
Kweli sisi watanzania ni watu wa "Deadline" yaani kati ya watumishi 15,000 ni watumishi 120 (sawa na 0.8%) tu ndio wamewasilisha ?

Na mwisho ni siku 28 zijazo.

Kazi kwelikweli.
 
Sekretarieti yenyewe ni li toothless dog majitu yamejipa ulaji tu hakuna kazi ya maana wanayofanya zaidi ya kupokea fomu na kufanya uapisho na kuwahoji wanaochelewesha fomu
Hawanauwezo wa kumchukulia mtu/ kiongozi aliyekiuka maadili zaidi ya kutoa ushauri.
Ni vyema hii sekretarieti ikapewa meno ya kuchukua hatua ikiwemo kupeleka viongozi wanaovunja maadili mahakamani wakashtakiwe la sivyo mi naona ni kama taasisi hewa ni bora hata isiwepo
 
Back
Top Bottom