VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Mkutano wa Sekretarieti ya CCM ulioisha usiku wa manane wa kuamkia leo umeibuka na mpya ya 2015. Habari za kuaminika toka kikaoni zinadokeza kuwa Sekretarieti imeamua na kupendekeza kuwa makada wote waliotangaza kuwa hawatagombea Ubunge,wasipitishwe tena majimboni wakikosa Urais.
Sekretarieti imebainisha kuwa hilo litapunguza mvutano majimboni kwakuwa tayari wameshachomoza makada wa kuwapokea vijiti walioaga. Sekretarieti inapendekeza watakaokosa ugombea wa Urais wasubiri nafasi za kuteuliwa endapo CCM itashinda uchaguzi ujao.
Wazo kama hili lilikuwepo 2005 na 2010 lakini wengi waliokosa kugombea Urais waligombea Ubunge majimboni mwao. Mwaka huu itawezekana. Tusubiri tuone. Watangaza nia wakae chonjo!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)