'Sekretari' wa balozi mbaroni Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Sekretari' wa balozi mbaroni Dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Dec 10, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 10, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,403
  Likes Received: 5,678
  Trophy Points: 280
  POLISI Kanda Maalum ya Dar es Salaam wamemkamata Katibu Muhtasi wa Ubalozi wa Canada, Jean Touchatte(48) kwa tuhuma za kuwatemea mate askari wa Usalama barabarani na Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)

  Touchatte anatuhumiwa kumshambulia askari wa usalama barabarani aliyekuwa akiongoza magari katika eneo la Banana wilaya ya Ilala.

  Kaimu kamanda wa kanda hiyo, Charles Kenyela, amesema, mtumishi huyo wa ubalozi anadaiwa kufanya makosa hayo Desemba 9 saa 8.45 mchana wakati askari huyo namba E 1653, Koplo Samson akiwa kazini maeneo hayo.

  Kwa mujibu wa Kenyela, wakati akiendelea kuyaruhusu magari yanayotokea Ukonga kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Touchatte alifika eneo hilo akiwa anaendesha gari lenye namba za usajili T 17 CD 178 Toyota Land Cruiser Prado mali ya Ubalozi wa Canada.

  Amesema, mtuhumiwa huyo alikuwa anatoka Ukonga kwenda uwanja wa ndege, ghafla alipunguza mwendo, akafungua kioo cha gari lake na kumtemea mate askari huyo.

  Kenyela amedai kuwa,kitendo hicho kiliwashangaza wengi walioshuhudia,na kwamba sababu ya kufanya hivyo haikufahamika, hivyo polisi wa doria walipewa taarifa ili kulifuatilia gari hilo.

  “Askari wetu walianza kufuatilia kwa nyuma gari hilo na walipofika barabara ya Nyerere karibu na Kamata gari hilo lilikamatwa na kupelekwa moja kwa moja hadi makao makuu ya polisi Trafic Kanda Maalum ya Dar es Salaam na kuwekwa chini ya ulinzi” amesema.

  Kwa mujibu wa Kenyela, wakati mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa,waandishi wa habari akiwemo Jerry Muro(29) wa TBC walifika kituoni hapo, wakitaka kufahamu nini kilichotokea ndipo mtuhumiwa huyo akamtemea mate sehemu ya chini ya kidevu chake na kusambaa katika flana aliyokuwa amevaa.

  Muro alifungua jalada la shambulio CD/IR/4818/2009, na kwa mujibu wa Kenyela, mtuhumiw alipohojiwa hakuwa tayari kujibu wala kutoa maelezo yake kwa madai kwamba mpaka balozi wake awepo.

  Vielelezo vya tukio hilo vimehifadhiwa polisi Kati na kwamba maelezo mengine zaidi juuu ya tukio hilo yatatolewa na Inspekta Jenerali wa Polisi.
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  hawa lowlives wengine wanapataje kazi katika diplomatic corps ya Canada?

  Si angeenda kutafuta gig katika bendi za Punk Rock (sub genre ya kutemeana mate) za Canada, angekutana nao kibao machizi wenzake.

  Askari zetu wana matatizo kibao kuanzia maslahi na mengine mengi, haina maana kuwazidishai matatizo. ungekutana na mchizi mjeshi ana ma complex na wadhungu angekuchabanga risasi hapo hapo halafu mambo mengine baadaye.
   
Loading...