Sekeseke la Bandari ya Bagamoyo

Sekeseke la Bandari ya Bagamoyo

SOPINTO

Senior Member
Joined
Oct 19, 2020
Posts
153
Reaction score
388
HILI NDIO SEKESEKE LA BANDARI YA BAGAMOYO.

MIAKA sita iliyopita, Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo nchini Tanzania ulikuwa ukitajwa kama mmoja wa miradi ya kimkakati yenye fursa kubwa ya kuzimua uchumi wa taifa hilo. Midomoni kwa watumishi wa umma na viongozi wa serikali, neno bandari ya Bagamoyo halikutoka.

Hata hivyo, miaka miwili iliyopita, upepo ukaanza kubadilika. Aliyekuwa Rais waTanzania wakati huo, hayati John Magufuli, alizungumza hadharani kuhusu mradi huo na kusema ulikuwa na "masharti ya hovyo" ambayo serikali yake isingeweza kuyakubali. Watanzania ni watu ambao kwa tabia wanapenda kuwaamini viongozi wao. Kauli hiyo kutoka kwa Kiongozi Mkuu wan chi ilizua mkanganyiko miongoni mwa wananchi; wengine wakiamini wale waliosema bandari hiyo ijengwe na wengine wakiamini mradi huo ni wa hovyo.

Hiyo ndiyo Tanzania ambayo Rais Samia Suluhu Hassan ameirithi linapokuja suala la ujenzi wa bandari hiyo. Kwenye kujibu swali kubwa la makala haya, ni muhimu kurudi nyuma kidogo kufahamu kuhusu mradi wenyewe.

Kuhusu mradi wa Bandari Bagamoyo
Kwa sadfa ya kijiografia, Tanzania imejikuta ikiwa nchi yenye bandari katika eneo ambalo wengi wa jirani zake hawana bandari. Miongoni mwa jirani zake nane; Malawi, Msumbiji, Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia, ni Kenya na Msumbiji pekee ndiyo wenye bahari. Bandari ya Dar es Salaam ndiyo imekuwa kama lango kuu la kupitishia bidhaa zinazokwenda katika nchi jirani zisizo na bahari. Hata hivyo, ingawa huduma za bandari hiyo zinahitajika sana, bandari ya Dar es Salaam- kwa sababu tofauti ikiwamo udogo wa eneo lake na ongezeko la mahitaji ya huduma na teknolojia za kisasa za meli, imeanza kuzidiwa.

Iliyokuwa Mamlaka ya Bandari wakati huo, iliona changamoto hiyo na ndiyo ikapendekeza kujengwa kwa bandari nyingine kubwa zaidi katika eneo la Bagamoyo - umbali wa takribani kilomita 75 tu kutoka Dar es Salaam ili kuendelea kuwa kitovu cha usafiri wa maji katika eneo la Afrika. Katika kutimiza azma hiyo, Mamlaka ya Bandari ikaja na Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania - ambao, pamoja na mambo mengine, ulipendekeza Bandari ya Bagamoyo ijengwe katika miaka ya 2021/2022.

Sadfa nyingine ya kijiografia ni kwamba eneo la Bagamoyo ni mojawapo ya maeneo ambayo China imeyatambua kama ya kimkakati katika Mpango wake Kabambe wa Belt and Road - ambao kimsingi unaunganisha dunia kupitia njia ya maji. Tanzania iko katika eneo la kimkakati kwa sababu inazungukwa na nchi nyingi zisizo na bahari, tayari ina reli mbili zinazounganisha na nchi jirani; TAZARA kwa maana ya Zambia na ile ya Kati inayokwenda mpaka Kigoma ambako ni jirani na Congo, Rwanda na Burundi pia.

Kama ujenzi wa Reli ya Mwendokasi (SGR) ukikamilika, Tanzania itakuwa na reli ya kisasa ya kusafirisha watu na mizigo kutoka Tanzania kwenda katika nchi jirani kwa haraka. Kwa hiyo, wakati Tanzania ikipanga kuwa na Bandari ya Bagamoyo kubwa na imara, wawekezaji kutoka China na Oman waliona fursa ya Eneo la Uwekezaji wa Biashara (EPZ) katika mji huo kwa sababu ya urahisi wa kusafirisha bidhaa kutoka eneo la Maziwa Makuu kwenda kwingineko duniani.

Faida nyingine ya Bandari ya Bagamoyo ilikuwa kwamba kwa sababu ya ukubwa wake, itakuwa na uwezo wa kupokea mizigo zaidi ya mara 20 ya Bandari ya Dar es Salaam na pia kupokea meli kubwa za kisasa ambao kwa sababu ya ukubwa wake, haziwezi kuja Dar es Salaam. Bandari ya Dar es Salaam ndiyo imekuwa kama lango kuu la kupitishia bidhaa zinazokwenda katika nchi jirani zisizo na bahari.

Kupitia mradi wa EPZ, ilielezwa vitafunguliwa zaidi ya viwanda ya 700 na kuajiri takribani watu 250,000 - ukiwamo mradi wa masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano kutoka kwa wawekezaji kutoka Korea Kusini. Huu ulikuwa uwe mradi mkubwa zaidi katika historia ya Tanzania ambako wawekezaji hao kutoka China, Oman na Korea Kusini wangeingiza nchini mtaji wa zaidi ya dola bilioni 10 (zaidi ya shilingi trilioni 23).Wawekezaji hao na nchi wanazotoka kwenye mabano ni China Merchants Ports Limited (China), Mfuko wa Uwekezaji wa Oman (OIA), na Science and Technology Policy Institute (STEPI)Korea Kusini.

Hofu Juu ya Mradi wa Bagamoyo
Maneno ya Magufuli yalikuja katika wakati ambao kulikuwa na taarifa nyingi kuhusu namna China inavyotwaa mali zisizohamishika za nchi zilizokopa fedha kutoka kwake na zikashindwa kurejesha kwa wakati. Mifano iliyokuwa ikitolewa sana ilihusu nchi kama Zambia na Sri Lanka. Katika mkutano wake na wafanyabiashara wa Tanzania, Magufuli alizungumza waziwazi kwamba kwa namna makubaliano yale ya Tanzania na wawekezaji yalivyokuwa, mkataba ule ulikuwa hauna maslahi na Tanzania naye asingekubali kuona mradi huo ukiendelea kwa namna hiyo.

"Yaani kwenye eneo lote kuanzia Tanga hadi Mtwara kusijengwe bandari yoyote. Bandari ya Kilwa tusiiendeleze, Bandari ya Mtwara ambayo itawezesha mikoa ya Kusini kupokea mafuta badala ya Dar es Salaam kisha yarudihuko, hatutakiwi kuiendeleza, barabara kutoka Mtwara hadi Bamba Bay ambayo itatuwezesha kusafirisha mizigo hadi Msumbiji tusiijenge," alisema Rais Magufuli.

Rais huyo aliyefariki dunia Machi 17 mwaka huu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Makamu Rais wake, alisema masharti mengine ya kufanyika kwa mradi huo ni kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutotakiwa kwenda kukusanya ushuru wala kodi katika eneo hilo, umiliki wa eneo hilo kwa miaka 33 na kufidiwa kwa gharama za uwekezaji wa ujenzi huo.

Spika wa Bunge, Job Ndugai, alizungumza katika nyakati hizo na kulalama kwamba serikali inafanya makosa kutoendelea na mradi huo kwa vile una faida kubwa na hizo ambazo zinaonekana kasoro zinaweza kuzungumzika.

Je, Kuna ukweli kwenye madai ya "mkataba wa hovyo"?....​

Tatizo nchii hii tunakosa mkakati wa muda mrefu na mfupi ki ujumla hatujui tunataka nini.

Bandari si jambo baya ki maendeleo tujiulize je hizi zilizopo tunaweza kuzitumia vema kujiletea maendeleo.

Binafsi nakubali ujenzi uendelee ila mambo ya msingi kwa faida ya nchii yazingatiwe.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kwa kweli mkuu umetupotezea muda wetu hakuna ulichoandika....nihadithi tu

1. Sema ama dadavua issuesmatatizo against mapendekezo na ni njia gani sahihi
2. Najua kuna timu iliundwa kufanya negotiations kuhusu maeneo yote yenye utata na yalitatuliwa
3. Wakubwa wa bandari ya dsm wakapenueza taarifambazo sio sahihi kumislead
4. Mkataba huwa ni maridhiano kati ya pande mbili na mnakubaliana kuongeza ama kutoa sehemu ambazo mmoja wenu haafiki "EIN WIN SITUATION"
 
kwa kweli mkuu umetupotezea muda wetu hakuna ulichoandika....nihadithi tuuu
1.sema ama dadavua issuesmatatizo against mapendekezo na ni njia gani sahihi
2.Najua kuna timu iliundwa kufanya negotiations kuhusu maeneo yote yenye utata na yalitatuliwa
3.wakubwa wa bandari ya dsm wakapenueza taarifambazo sio sahihi kumislead
4.Mkataba huwa ni maridhiano kati ya pande mbili na mnakubaliana kuongeza ama kutoa sehemu ambazo mmoja wenu haafiki "EIN WIN SITUATION"
Binafsi nashindwa kutoa maoni kwa kuwa mkataba wenye sijauona. Mkataba huu bado ni siri ambayo ni serikali pekee inayojua. Hata hivyo jambo lililo dhahiri ni kwamba tunahitaji bandari ya Bagamoyo. Bandari ya Dar in limitations zake. Serikali iendelee kufanya mazungumzo ikizingatia maslahi mapana ya nchi.
 
Kila mara hili jambo likitaka kusahaulika huku jamii forum..basi hutokea mtu na kujifanya kuchambua na kujiuliza maswali yale yale..

kwani mmetumwa au?
mods unganisheni huu uzi na wenzake
 
Bandar Kama ikijegwa lazima iwe na faida ila kutokana na China kukopesha na kuchukua vitu kweny nchi za watu it's better usiendelee manake bandar ya dsm inaweza ikafa
 
Hayo maneno ya kutetea ujenzi Wa bandari ya bagamoyo bila kutuwekea mkataba wenyewe bayana tujisomee wenyewe ni ushahidi tosha kuwa huo mkataba ni wa hovyo!! Kwanza nadhani so kweli muda ni miaka 33! Lease ya mradi mkubwa kama ule itakuwa ni miaka 99! Watuwekee mkataba kwenye tovuti ya bunge. Kama kuna maslahi mapana ya taifa wanaogopa nini kuuanika huo mkataba?
 
kwa kweli mkuu umetupotezea muda wetu hakuna ulichoandika....nihadithi tuuu
1.sema ama dadavua issuesmatatizo against mapendekezo na ni njia gani sahihi
2.Najua kuna timu iliundwa kufanya negotiations kuhusu maeneo yote yenye utata na yalitatuliwa
3.wakubwa wa bandari ya dsm wakapenueza taarifambazo sio sahihi kumislead
4.Mkataba huwa ni maridhiano kati ya pande mbili na mnakubaliana kuongeza ama kutoa sehemu ambazo mmoja wenu haafiki "EIN WIN SITUATION"
Mkuu tujadiri mpira tu; maelezo mengi hayana maana yeyote. Tuendelee na kujua hatma ya Simba huko club bingwa Africa na Dar Young African baasi; hu uzi umejaa utoporo mwingi
 
Binafsi nashindwa kutoa maoni kwa kuwa mkataba wenye sijauona. Mkataba huu bado ni siri ambayo ni serikali pekee inayojua. Hata hivyo jambo lililo dhahiri ni kwamba tunahitaji bandari ya Bagamoyo. Bandari ya Dar in limitations zake. Serikali iendelee kufanya mazungumzo ikizingatia maslahi mapana ya nchi.
Bila hata kuona mkataba. Nchi itakabidhije lango kuu lake kwa nchi nyingine? Wewe unaona kuna usalama hapo? Yaani ufunguo wa nyumba yako umpe jirani yako awe ndiye anaamua ni nani aingie kwenye nyumba yako na ni nani atoke. Ujinga wa hali ya juu huu. Na zaidi: Angalia njia kuu za meli bahari uniambie hiyo bandari itakuwa na nini la zaidi kushinda bandari ya Dar, Tanga na Mtwara. Nchi itakazohudumia ni zile zile. Unataka kuniambia tukiendeleza banzari zetu hizi tatu hazitakidhi mahitaji? Tuache kupenda vya bure, vitatutokea puani.
 
Leteni mkatàba tuone kilichopo tusijadili uvumi usio na misingi weka hapo.chanzo sahihi
 
Kila mara hili jambo likitaka kusahaulika huku jamii forum..basi hutokea mtu na kujifanya kuchambua na kujiuliza maswali yale yale..

kwani mmetumwa au?
mods unganisheni huu uzi na wenzake
Mkuu hawa k.ima wametumwa na vigogo2014 na baba zao wastaafu. Wameahidiwa pesa nyingi wakifanikisha hili na spika yupo upande wao.
 
HILI NDIO SEKESEKE LA BANDARI YA BAGAMOYO.

MIAKA sita iliyopita, Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo nchini Tanzania ulikuwa ukitajwa kama mmoja wa miradi ya kimkakati yenye fursa kubwa ya kuzimua uchumi wa taifa hilo. Midomoni kwa watumishi wa umma na viongozi wa serikali, neno bandari ya Bagamoyo halikutoka.

Hata hivyo, miaka miwili iliyopita, upepo ukaanza kubadilika. Aliyekuwa Rais waTanzania wakati huo, hayati John Magufuli, alizungumza hadharani kuhusu mradi huo na kusema ulikuwa na "masharti ya hovyo" ambayo serikali yake isingeweza kuyakubali. Watanzania ni watu ambao kwa tabia wanapenda kuwaamini viongozi wao. Kauli hiyo kutoka kwa Kiongozi Mkuu wan chi ilizua mkanganyiko miongoni mwa wananchi; wengine wakiamini wale waliosema bandari hiyo ijengwe na wengine wakiamini mradi huo ni wa hovyo.

Hiyo ndiyo Tanzania ambayo Rais Samia Suluhu Hassan ameirithi linapokuja suala la ujenzi wa bandari hiyo. Kwenye kujibu swali kubwa la makala haya, ni muhimu kurudi nyuma kidogo kufahamu kuhusu mradi wenyewe.

Kuhusu mradi wa Bandari Bagamoyo
Kwa sadfa ya kijiografia, Tanzania imejikuta ikiwa nchi yenye bandari katika eneo ambalo wengi wa jirani zake hawana bandari. Miongoni mwa jirani zake nane; Malawi, Msumbiji, Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia, ni Kenya na Msumbiji pekee ndiyo wenye bahari. Bandari ya Dar es Salaam ndiyo imekuwa kama lango kuu la kupitishia bidhaa zinazokwenda katika nchi jirani zisizo na bahari. Hata hivyo, ingawa huduma za bandari hiyo zinahitajika sana, bandari ya Dar es Salaam- kwa sababu tofauti ikiwamo udogo wa eneo lake na ongezeko la mahitaji ya huduma na teknolojia za kisasa za meli, imeanza kuzidiwa.

Iliyokuwa Mamlaka ya Bandari wakati huo, iliona changamoto hiyo na ndiyo ikapendekeza kujengwa kwa bandari nyingine kubwa zaidi katika eneo la Bagamoyo - umbali wa takribani kilomita 75 tu kutoka Dar es Salaam ili kuendelea kuwa kitovu cha usafiri wa maji katika eneo la Afrika. Katika kutimiza azma hiyo, Mamlaka ya Bandari ikaja na Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania - ambao, pamoja na mambo mengine, ulipendekeza Bandari ya Bagamoyo ijengwe katika miaka ya 2021/2022.

Sadfa nyingine ya kijiografia ni kwamba eneo la Bagamoyo ni mojawapo ya maeneo ambayo China imeyatambua kama ya kimkakati katika Mpango wake Kabambe wa Belt and Road - ambao kimsingi unaunganisha dunia kupitia njia ya maji. Tanzania iko katika eneo la kimkakati kwa sababu inazungukwa na nchi nyingi zisizo na bahari, tayari ina reli mbili zinazounganisha na nchi jirani; TAZARA kwa maana ya Zambia na ile ya Kati inayokwenda mpaka Kigoma ambako ni jirani na Congo, Rwanda na Burundi pia.

Kama ujenzi wa Reli ya Mwendokasi (SGR) ukikamilika, Tanzania itakuwa na reli ya kisasa ya kusafirisha watu na mizigo kutoka Tanzania kwenda katika nchi jirani kwa haraka. Kwa hiyo, wakati Tanzania ikipanga kuwa na Bandari ya Bagamoyo kubwa na imara, wawekezaji kutoka China na Oman waliona fursa ya Eneo la Uwekezaji wa Biashara (EPZ) katika mji huo kwa sababu ya urahisi wa kusafirisha bidhaa kutoka eneo la Maziwa Makuu kwenda kwingineko duniani.

Faida nyingine ya Bandari ya Bagamoyo ilikuwa kwamba kwa sababu ya ukubwa wake, itakuwa na uwezo wa kupokea mizigo zaidi ya mara 20 ya Bandari ya Dar es Salaam na pia kupokea meli kubwa za kisasa ambao kwa sababu ya ukubwa wake, haziwezi kuja Dar es Salaam. Bandari ya Dar es Salaam ndiyo imekuwa kama lango kuu la kupitishia bidhaa zinazokwenda katika nchi jirani zisizo na bahari.

Kupitia mradi wa EPZ, ilielezwa vitafunguliwa zaidi ya viwanda ya 700 na kuajiri takribani watu 250,000 - ukiwamo mradi wa masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano kutoka kwa wawekezaji kutoka Korea Kusini. Huu ulikuwa uwe mradi mkubwa zaidi katika historia ya Tanzania ambako wawekezaji hao kutoka China, Oman na Korea Kusini wangeingiza nchini mtaji wa zaidi ya dola bilioni 10 (zaidi ya shilingi trilioni 23).Wawekezaji hao na nchi wanazotoka kwenye mabano ni China Merchants Ports Limited (China), Mfuko wa Uwekezaji wa Oman (OIA), na Science and Technology Policy Institute (STEPI)Korea Kusini.

Hofu Juu ya Mradi wa Bagamoyo
Maneno ya Magufuli yalikuja katika wakati ambao kulikuwa na taarifa nyingi kuhusu namna China inavyotwaa mali zisizohamishika za nchi zilizokopa fedha kutoka kwake na zikashindwa kurejesha kwa wakati. Mifano iliyokuwa ikitolewa sana ilihusu nchi kama Zambia na Sri Lanka. Katika mkutano wake na wafanyabiashara wa Tanzania, Magufuli alizungumza waziwazi kwamba kwa namna makubaliano yale ya Tanzania na wawekezaji yalivyokuwa, mkataba ule ulikuwa hauna maslahi na Tanzania naye asingekubali kuona mradi huo ukiendelea kwa namna hiyo.

"Yaani kwenye eneo lote kuanzia Tanga hadi Mtwara kusijengwe bandari yoyote. Bandari ya Kilwa tusiiendeleze, Bandari ya Mtwara ambayo itawezesha mikoa ya Kusini kupokea mafuta badala ya Dar es Salaam kisha yarudihuko, hatutakiwi kuiendeleza, barabara kutoka Mtwara hadi Bamba Bay ambayo itatuwezesha kusafirisha mizigo hadi Msumbiji tusiijenge," alisema Rais Magufuli.

Rais huyo aliyefariki dunia Machi 17 mwaka huu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Makamu Rais wake, alisema masharti mengine ya kufanyika kwa mradi huo ni kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutotakiwa kwenda kukusanya ushuru wala kodi katika eneo hilo, umiliki wa eneo hilo kwa miaka 33 na kufidiwa kwa gharama za uwekezaji wa ujenzi huo.

Spika wa Bunge, Job Ndugai, alizungumza katika nyakati hizo na kulalama kwamba serikali inafanya makosa kutoendelea na mradi huo kwa vile una faida kubwa na hizo ambazo zinaonekana kasoro zinaweza kuzungumzika.

Je, Kuna ukweli kwenye madai ya "mkataba wa hovyo"?....​

Alokwambia mkataba unajadiliwa mtandao nan!! Wauweke waziiii wote tuuone ndo tutajua cha kusema
 
Huu ni mradi wa kunufaisha watu binafsi zaidi. Hakuna sababu ya msingi ya kuwa na bandari mpya wakati tayari kuna bandari mbili ambazo ziko karibu bandari ya Tanga na Dar. Lakini bandari ya Tanga inatakiwa kupanuliwa na kuanza kusafirisha mafuta ya Uganda kwanini tusikuze hiyo bandari ambayo ipo na uwekezaji umeanza na kufungua bandari ya tatu kwenye eneo la umbali wa 341 kilometers (212 miles) tu. Tena tunaaza upya tujiulize hii ina maana gani
 
Back
Top Bottom