Seif amgeukia Tendwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Seif amgeukia Tendwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jan 9, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Amwambia aache kuingilia maamuzi ya CUF
  [​IMG] Asisitiza: ``Hamad sio mwanachama wetu``  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad


  Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, sasa amemgeukia Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, na kumtaka aache mara moja kuingilia maamuzi yaliyofanywa na chama hicho.
  Badala yake amemtaka afuate sheria na kanuni ya uendeshaji wa Taasisi yake na kwamba hadi anazungumza hajapokea amri yoyote ya mahakama.
  Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Manzese Bakhresa jijini Dar es Salaam jana, Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, alisema anashangazwa kuona Tendwa mwenye jukumu la kulinda Katiba za vyama vyote anakuwa mtetezi mkuu wa Mbunge wa Jimbo la Wawi, Hamad Rashid Mohamed, ambaye amefukuzwa uanachama kwa kufuata sheria na taratibu zote.
  Mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wanachama wa chama hicho, ulikuwa maalum kutoa ufafanuzi wa hatua iliyochukuliwa na Baraza Kuu la Uongozi wa chama hicho wa kuwafukuza uanachama watu wanne akiwemo Hamad.
  Alisema kwa ujumla anamheshimu sana Tendwa kutokana na majukumu yake ya kitaifa lakini kwa hatua yake anayoichukua ya kumtetea Hamad ni jambo linalomshangaza.

  "Baada ya kuchukuliwa maamuzi yale, Msajili wa vyama vya siasa leo amejitokeza hadharani kumtetea Hamad, jambo hili linanishangaza sana, nilitegemea yeye angetuunga mkono kutokana na kutumia Katiba yetu vizuri," alisema.

  Alhamisi iliyopita Tendwa, alisema tabia ya kufukuzana uanachama kwenye vyama vya siasa sio mzuri na unalisababishia hasara taifa na wananchi wanakosa haki yao ya msingi ya kuwakilishwa bungeni.

  Maalim Seif alisema nia ya Msajili kutetea jambo hilo ni kuona chama hicho kinaendeshwa kihuni bila kufuata taratibu kitu ambacho kamwe hakitafanyika.

  "Kweli Msajili anatetea kwa maana gani hasa, anataka kuona CUF ikiendeshwa kihuni? Kamwe haitawezekana kwani chama hiki hapendwi mtu," alisema huku akionekana kuchukizwa na jambo hilo.

  Aidha amemtaka Msajili huyo pamoja na watu wengine waliojitokeza kusimama mstari wa mbele kupinga maamuzi hayo waache mara moja kwa sababu chama hicho sio mali ya mtu bali ni taasisi inayomilikiwa na Watanzania.

  Akizungumzia mazingira ya kufukuzwa Hamad na wenzake watatu, Seif alisema kabla ya kuchukua maamuzi hayo kwanza walijaribu kuitisha vikao viwili vya kumuonya kuhusu mwenendo wake mbaya, lakini hakuonyesha kubadilisha mwenendo wake.
  Alisema kikao kimoja kilifanyika Zanzibar na kikao cha pili kilifanyika jijini Dar es Salaam na kuwashirikisha watu mashuhuri.

  Alieleza kwa ujumla baada ya hali hiyo kushindikana waliamua kufuata taratibu za chama hicho ikiwemo kuwaita watu wote wanaotuhumiwa kukihujumu chama kwa ajili ya kujitetea na walifanya hivyo.
  Alisema Baraza Kuu la uongozi wa chama hicho lilichukua maamuzi hayo kwa kuangalia haki ya mwanachama na sio ubunge wa mtu,

  kwani ndani ya chama hicho mtu yeyote hata akiwa kiongozi akionekana kwenda kinyume na taratibu anachukuliwa hatua.
  Pamoja na hayo alisema CUF imefuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kumtaarifu Spika wa Bunge juu ya uamuzi huo na kama haikutekelezwa hayo chama chake hakitahusika.

  "Hakuna atakayeweza kurudisha nyuma jambo hili, tumemwambia Spika kuwa huyu Hamad sio mwanachama wetu, akitaka kumlea hilo lake," aliongeza kusema.

  Akizungumzia tishio la mahakama, Maalim Seif alisema kamwe hatishiki na jambo hilo kupelekwa mahakamani kwa sababu anatambua kila kitu kiliendeshwa kisheria na hakuna kitu kilichokiukwa.

  Alisema watu kuwafukuza ndani ya chama hicho sio mara ya kwanza na wote walikimbilia mahakamni lakini baadae ukweli ulibaki palepale. Hata Mahakama ikimrudishia Hamad ubunge wake, watamtambua na ataendelea kuwa Mbunge wa mahakama.

  Alisema amegundua kuna ajenda za siri zinazofanywa na baadhi ya watu waliochukizwa na muafaka wa Zanzibar ambapo sasa wanafanya kila juhudi kuwarudisha nyuma Wazanzibari walioanza kupata faida ya amani.
  Alisema CUF itazidi kusimama imara kupinga njama zozote zitakazosababisha visiwa vya Zanzibar kukosa amani na kurudi katika hali ya siasa za huko nyuma.

  Awali Naibu Katibu Mkuu wa chama hichoTanzania Bara, Julius Mtatiro, alisema zoezi la kuwasafisha viongozi wanaoaminika ni waasi litaendelea katika ngazi zote kuanzia Wilaya, Kata hadi Matawi ya chama hicho.
  Alisema kuanzia sasa wanachama wote wawe makini kuwatambua watu wa aina hiyo na baadae wafanye utaratibu wa kuwafukuza kulingana na katiba na kanuni ya chama hicho.

  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

   
 2. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Domocrazy.......Loading.....
   
 3. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wananchi waliomchagua je?.....
  Hao wanahusika vipi na ugomvi wa vyama?
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Pamoja na Wananchi waliomchagua ili awaongoze, lakini kama anafanya makosa kiongozi aliyechaguliwa na wanachi ,itabidi viongozi wenzake pamoja na wanachama wamuonye ikiwa hataki kujirekebisha itabidi uongozi umng'oe kwenye Uongozi pamoja na Uanachama wake au kwa heshima zake ingebidi ajiuzulu kwa hiari yake. alivyofanya maalim Seif nakubaliana nae.
   
 5. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwani kosa lake ni nini?
  Au hairuhusiwi kuhoji ufanisi wa katibu mkuu?
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hamad rashid apumzike sasa..kama cuf wameshakufikuza unang'ang'ania nini sasa?si uondoke ?
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  si akahoji huko aendako au
   
 8. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Au nini?.....
   
 9. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,140
  Likes Received: 7,391
  Trophy Points: 280
  Rangi za hizo Mic + Pazia lake hapo nyuma linanifanya niamini kweli hawa jamaa ni CCM-B,
  Mtatiro upo???
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  CUF na CCm ni tofauti mkuu lakini
   
 11. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,140
  Likes Received: 7,391
  Trophy Points: 280
  Tofauti majina tu, hizo rangi hazikuwekwa hapo kwa bahati mbaya kaka!!!
  Ni jibu tosha kwa wale wasioamini ndoa baina ya hivi vyama.
  Tangu lini CUF wakawa na rangi ya kijani??
   
 12. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,144
  Likes Received: 2,178
  Trophy Points: 280
  Dada. huyo anaolewa..... Dada huyo Anaolewa Mahari...

  Ishatolewa Dada huyo Anaolewa....

  Kazi hizi ni kama Nyimbo Zetu za Bongo Tutasahau karibuni tu
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #13
  Jan 9, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Tofauti zao ni zile za mke na mume!
   
Loading...