Sehemu nzuri ya kumpata mchumba

doppla2

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2014
Posts
1,393
Reaction score
1,462
Watu husema maisha popote ila linapokuja suala la kumpata mwenza wa maisha unapaswa kujiongeza.

Tulipokua vyuoni wengi tulipata wapenzi na kwa kipindi kile japo tulikua tumeshapevuka kiakili ujana maua ulituzuzua sana . Leo uko na Jane kesho una Manka and vice vesa. Tulijiamini sana tukimaliza masomo tukienda makazini ndio tutawapata akina mr and mrs right...

Turipofika makazini all to find wote wako married, au ni wachumba wa watu , wakiajiriwa wapya tayari wameshadakwa huko walikotokea. Na kutokana na nature za kazi tunaingia asubuhi kutoka jion...kuja kufika home tayari night.

Watu wapya tunakutana nao kwenye vyombo vya usafiri au sehemu za migahawa au bar....tatizo wengi unakua hujui background zao ukijilipua baada ya outing mbili tatu unabaini is not my type

Na mzunguko unajirudia.........ukiwaeleza washikaji watakushauri uwe unaenda church au kwenye conference huenda utapata huko, but wengi wanaoenda maeneo kama ya church wanakua wameshaaribu kifupi ukisikia tu Cv yake unakata tamaa na wazee wa conference wengi wako desperate....kama wewe.

Kwa changamoto hizi utakuta wengi sasa wanapenda kuanzisha mahusiano na mtu aliyekutana naye kwenye social media...kiukweli wengi wa kundi hili ni wazee wa drama na fake life, siku mkikutana ni mtu tofauti kabisa na uliyechat naye kwenye platform mlizokutana.


Wadau ebu leteni uzoefu where is the best place to meet with mrs and/or mr right?
 
Ukitulia utapata tu usiumize akili kusaka wa kuoa

Uki behave like gentleman wala hukai muda mrefu utatafutwa sana.

Sisi wanaume tunatafuta nani wa kumuoa wanawake nao wanatafuta nani wa kumuoa, isitoshe wanawake ndo wenye mzigo mkubwa na ndo maana anaweza kudate na wanaume wengi ili tu atafute ni yupi anayestahili ktk kudanga huko hujikuta muda umepita na anadandia yeyote ajaye ambabatize Sharti goli liingie tu.

Mwanaume unapaswa ujiheshimu tu, tafuta pesa, uijali jamii unayoishi , hakika watakuja wenyewe wakikuambia furani anafaa kuwa mkeo

Mimi nililengeshwa sana, mpaka niliosoma nao chuoni walikuwa wakiniguatilia ile mbaya lkn mwisho wa siku wewe unachagua tu ni yupi sasa ktk hao
 
Hakuna sehem maalumu muhim mshirikishe Mungu katika maombi yako omba kwa nia thabiti sema na Mungu wako mpe sifa za mke au mume umtakaye huku ukiendelea kujipenda na kuendelea kuishi maisha yako

Mungu hujibu kila goti lipigwalo muhimu tu omba kwa nia thabit na usisahau kua mwema huwez kuomba upewe mke au mume bora ikiwa wewe hauko hivo pia
 
Mkuu sisi kwetu ukitaka kuoa na kama umeshindwa kupata mchumba kama wewe,unawatonya wana familia wa karibu kwa mfano mama, ama dada ama shangazi, halafu unawapa criteria aka TBS yako unataka wa hivi mwenye hiki na hiki asie na hiki baaaaas mchezo umekwisha, hakuna mtu anaemjua mwanamke kama mwanamke mwenzake niamini kaka, lakini mind you lengo iwe ni ndoa. hapo sasa unatikwa uwe na subira na usiwe na pupa utaletewa mambo wewe mwenyewe utagwaya.
 
Daaah mpaka tumechanganyikiwa....tired to b single.
 
Shuleni. Nawe ukiwa mwanafunzi au mwalim ni rahisi kumstudy mtu kuliko sehemu ingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…