Sayari 4 Mstari Mmoja - Na Mwezi Unazikaribia Angani

Sayari 4 Mstari Mmoja - Na Mwezi Unazikaribia Angani

njiwaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
289
Reaction score
209
Sayari 4 ziko katika mstari angani na Mwezi unazikaribia kati ya 14 hadi 23 Agosti 2018

Zuhura (Venus), Mshtarii (Jupiter), Zohali (Saturn) na Mirihi (Mars) zinaonekana angani zikiwa katika mstari mnyoofu kutoka magharibi kwenda mashariki na Mwezi unazikaribia kati ya tarehe 14 hadi 23 Agosti, 2018.

Muda wa kuziona sayari zote hizi ni kuanzia saa moja. Zuhura itatua magharibi na kupotea baada ya saa tatu.

Sayari huonekana kama nyota angani kwa hiyo namna ya kutofauitsha ni kwa mn'gao wake. Sayari ya Zuhura (Venus) inawaka kabisa kwa unjano upande wa magharibi wakati Mirihi (Mars) inamulika kwa rangi nyekundu upande wa mashariki.

Mshtarii (Jupiter) inan'gaa sana utosini.

Mn'gao wa Zohali (Saturn) ni mkali lakini ni sawa na nyota zingine. Kwa hiyo namna ya kutofautisha ni kwamba mwanga wa sayari zote haumeremeti kama nyota za kawaida.

Kwa hiyo uangalie nyota kwa makini na kama haimeremeti basi ni sayari.

Sayari 4 ziko katika mstari angani na Mwezi unazikaribia kati ya 14 hadi 23 Agosti 2018==.png

4 planets in line close to the Moon 14 to 23 August 2018==.png
 
Kwanini haya matukio yanaongozana sana nyakati hizi?
 
Four planets Venus, Jupiter, Saturn and Mars form a straight line in the sky from west to east and the Moon will be close to each one in turn from 14 to 23 August 2018

Venus is extremely bright in the west soon after sunset, while Mars is an very bright RED star on the opposite side towards the east. Jupiter shines brightly overhead, and Saturn shines sharply in mid-eastern sky.

Planets look like stars in the sky but their shine is steady and does not twinkle when you compare with nearby stars.

All four planets can be seen from 7 pm onwards soon after sunset. Venus sets in the west after 9 pm.

4 planets in line close to the Moon 14 to 23 August 2018==.png

Sayari 4 ziko katika mstari angani na Mwezi unazikaribia kati ya 14 hadi 23 Agosti 2018==.png
 
Mwenyewe nimeona mkuu ila mwezi saivi saa tatu haupo tena.
Ni kwa bahati tu. Huwa mara moja moja sayari zinakaribiana kuwa eneo moja la anga. Kwa hiyo ni bahati yetu nzruri.

Pia anga haina mawingu mengi wakati huu kwa hiyo nyota na sayari tunaziona vizuri na kwa urahisi.
 
kabla ya july 11 mercury nayo ilikua karibu na dunia ila kwa sasa imeshasogea mbali, baadae ikaja mars july 27 yenyew ndo ilipita karibu kabisa na dunia tangu ifanye hvyo miaka 15 iliopita, sayari hizo kwe mpangilio huo zitaanza kusogea taratibu na kwenda mbali zaidi na dunia ila venus itaendelea kuonekana maeneo hayo mpk kwenye mwezi october nayo itapotea kwenda mbali zaidi
 
Ni kweli uliyoandika.

Kwa vile sayari zinazunguka katika mizingo ya miduara iliyoingiliana, mara kwa mara Dunia inakuwa jirani zaidi kwa kila sayari kufuatana na kasi ya mzunguko wa sayari.
 
Nini kifanyike ili kuinufaisha jamii yetu na elimu hii hususani wanafunzi
 
Nini kifanyike ili kuinufaisha jamii yetu na elimu hii hususani wanafunzi
Waalimu wa primary na sekondari waanzishe vikundi vya wanafunzi kuzungumzia na kuangalia nyota angani. Wanaweza kuwasiliana na chama cha ASSAT ambacho ni chama cha Astronomia Tanzania kwa kutuma baruapepe Assat.Astronomy@gmail.com kwa maelezo na habari zaidi ya namna ya kuwaendeleza wanafunzi wao.

Wazazi nao watumie mvuto wa nyota za angani kuwaendeleza watoto wao kwa kupata habari kutoka ASSAT.
 
Back
Top Bottom