o_2
JF-Expert Member
- Jul 20, 2017
- 431
- 389
'You won't find faith and hope down a telescope,
You won't find heart and soul in the stars'
'Science and faith' ni albamu ya pili kutoka katika kundi la wanamuziki wa rock kutoka Ireland iliyotoka mwaka 2010. 'sayansi na imani' ni jina la wimbo lililobeba album hiyo.
Walijaribu kuelezea namna gani maisha yanavyoweza kuwa complicated hasa kwenye nyanja mbili kwa maana ya sayansi na imani.
Kuna vitu huwezi kuviona, huwezi kuvishika bali kwa imani. Mambo kama upendo, chuki na hisia huwezi kuvishika lakini vina impact kubwa sana kwa mwanadamu bali ukiwa na imani. Imani inaweza kufanya chochote kuwa. Imani haina kipimo. Huwezi kuipima lakini ina matokeo makubwa sana. Fikiria dini na madhehebu mbali mbalimbali yaliyopo duniani.
Leo watu wanaweza kuuana kwa sababu tu ya kuikashifu imani ya mtu mwingine. Unaweza kudhania ni ujinga usio na faida lakini ukitazama matukio yake kwenye jamii unagundua imani ndio msingi wa kila kitu katika dunia hii.
Imani na maisha.
Sayansi imekuja kutupa matokeo kwa yale tusiyoyajua. Sayansi inakipimo. Kama jibu ni hasi ni hasi, kama jibu ni chanya ni chanya. Maisha bila sayansi yangekuwaje? Sayansi imetupa njia ambayo imani imeshindwa kutatua. Leo ukienda hospitali unapimwa kwa vifaa maalum vilivyopo ili kupata majibu ya maswali yako. Vifaa na tiba watu walikaa wakafanya utafiti na kufikia hitimisho. Leo kuna madawa wa kila aina ambayo yamepatikana kutokana na uwepo wa sayansi.
Leo ukipata homa unaenda hospitalini kupima ujue shida. Wakigundua una malaria unapewa dawa. Kwa imani unakunywa na unapona.
Sayansi na imani zimetupa matokeo.
Maisha ni sayansi, imani ni maisha.
Tuendelee kuishi.
[emoji1685]