Sawa tumezuia mifuko ya plastic, je vipi kuhusu hili suala?

Mnyenz

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
1,424
4,317
Wote kwa pamoja kama Watanzania ninaamini tumesikia na kukubaliana juu ya katazo la Serikali yetu ya TANZANIA kuhusu matumizi ya mifuko ya nylon (plastic).

Kwa mujibu wa wataalamu wetu(hata kwa akili ya kawaida tu) mifuko hii imekua na madhara mengi kwa jamii yetu kwa ujumla.

Na marufuku/katazo hili si hapa nchini kwetu tu bali mataifa mbali mbali yameshatangulia kufanya hivyo na pia naamini na mengine yatafuata baadae.

Madhara machache kati ya mengi yanayosababishwa na mifuko hii ni pamoja na:

UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU.
Ifahamike wazi ya kwamba mifuko hii ya plastic huwa haiozi kwa haraka, hivyo inapotupwa honyo mara nyingine hujikusanya kwa kubebwa na maji ya mvua na kisha kwenda kuziba mitaro inayopitishia maji.

HATARI KWA VIUMBE HAI.
Mara nyingine mifuko hii hutupwa hovyo maeneo yote hivyo kuna baadhi ya wanyama (ng'ombe, Mbuzi) huila na kuimeza pale wawapo malishoni na mara nyingi husababisha vifo kwa wanyama hao.
Nyakati nyingine huenda hata kuhatarisha maisha ya viumbe wengine kama samaki n.k

NI KWA NAMNA GANI SERIKALI IMEJIANDAA NA MADHARA BAADA YA KATAZO HILO?
Hapa sizungumzii mbadala wa mifuko ile, ila ninachotaka kusema ni;

Kwa kuwa tarehe moja ni marufuku kwa mtu yeyote kutumia mifuko hiyo, (kwa tafsiri nyepesi tuitupe/kuiteketeza) ina maana siku chache mbeleni kila kona kutakua kumezagaa mifuko iliyotupwa na hivyo ile sababu ya kukataza itakua imekubwa na changamoto ile ile wanayohubiri kuwa ni madhara, na hata kama tukisema kila mtu aichome bado kutakua na uchafuzi wa hali ya hewa.

Waliposema ni kuanzia tarehe moja ina maana kuna uwezekano hata viwanda viliendelea kutengeneza au kuuza stock iliyokua imebaki maana katazo linasema ni kuanzia tarehe moja(hapa kuna kisa nilisikia kuna jamaa alikua akiitengeneza mifuko hii, walipomfuata kumuhoji aliwajibu simple tu ya kwamba tarehe bado) hivyo kuna uwezekano kukawa na idadi kubwa sana ya mifuko hiyo mitaani kuliko hata ilivyokua kawaida hivyo kusema tu kwamba ni marufuku kuitumia kuanzia tarehe fulani ina maana unaandaa bomu la uchafuzi wa mazingira ambalo lengo lako lilikua kulikwepa.

Pendekezo langu ni kuwa ni bora ingetangazwa kila mwananchi /familia kulingana na anapoishi apeleke mifuko hiyo kwa kiongozi wa mtaa halafu Wahusika wapite kuikusanya kwa viongozi hao wa mitaa na kwenda kuiteketeza kitaalamu pasipokuwa na uchafuzi wa mazingira.

Tofauti na hapo ni kuwa tutakataza kutumia mifuko hivyo kwa nia ya kuzuia uchafuzi wa mazingira ila ndio tutayachafua mazingira kwa speed ya 5G japo kwa muda mfupi.
 
Hilo wazo lako litatuletea tu usumbufu mwingine ukiondoa huu wa usajili wa line za simu unaoendelea. Hivyo kwa niaba ya watanzania wote wasiopenda usumbufu, nalipinga kwa 100%.
 
Wazo lako ni kama langu, hata mimi nilifikiri kwa nin wasizuie chanzo? kama inatokea viwandani hapa nchini viwanda vinapigwa marufu kama ni importer inapigwa marufu kama uzalishaji haupo automatically itaisha yenyewe mtahani bila ya watu kuangaika
 
Back
Top Bottom