Sauti za milipuko Boko usiku huu

Sauti za milipuko Boko usiku huu

labda tatizo ni kuchukua sheria mkononi kwenye ndogondogo ,tuchukue sheria mkononi kwenye kubwa kama escrow,sasa hata ukitaka kufuata mkondo wa sheria ni kazi bure majaji wenyewe wengi wao ni wala rushwa, refer to escrow scandal

Ndio hivyo kuchomaa gari haisaidii .Sijaona. watu wanaandamana kuhusu escrow.Kisheria bodaboda wamefanya kosa.
 
Badaboda ni watu wa ajabu sana..Wadhibitiwe maana wana tabia za ajabu sana.Pakitokea ajali hata kama wao ndio wenye makosa huchoma gari.Hawajui vyombo vya moto sio salama mfano gari kupasuka tairi ni nje ya control ya dereva.Kwa nn wachome.??I dont like it.Ukitizama thamani ya gari hata uwape 10 yrs hawawezi kulipa.Wat if huna bima??
 
Badaboda ni watu wa ajabu sana..Wadhibitiwe maana wana tabia za ajabu sana.Pakitokea ajali hata kama wao ndio wenye makosa huchoma gari.Hawajui vyombo vya moto sio salama mfano gari kupasuka tairi ni nje ya control ya dereva.Kwa nn wachome.??I dont like it.Ukitizama thamani ya gari hata uwape 10 yrs hawawezi kulipa.Wat if huna bima??

huuu niushenzi kabisa unakuta wao ndio wenyemakosa mwisho wasiku ndio wakwanza kuchukua sheria mkononi.
harafu unachoma gari ya mtu ili iweje?
lakini mm siwalaum wakuwalaum ni serikali yetu na vyombo vya usalama ndio sababu ya kufikia hapa.
yashakuwa mazoea ya kutowawajibisha wavunjifu wa sheria au wenye makosa na hasa haki hupewa mwenye nacho na wanyonge wao kutwa niwatu wakuonewa tuu ndio maana mwisho wa siku njia sahihi ya kupata haki yao ni kuchukua sheria mikononi
 
Hii nchi kila mtu ni mbabe tu, watu washachoka kuwa waungwana sasa maana wanajihisi kama uungwana wao unawafanya waburuzwe. Bodaboda wanechoma moto gari kibabe na sasa mwenye gari anawasaka kibabe. Utemi kama huu huwa ni dalili mbaya sana.
Ova

Sasa hapo mtu akisema watu wa namna hii "wapigwe tu!" anaonekana amechafua hali ya hewa.

Tairi limepasuka kwa bahati mbaya,mambo yanakuwa hivyo.

JE,HUU NI UUNGWANA?
 
Ndio ugumu uliopo kwa kupata taarifa muhimu za matukio ya kushtusha Bongo, ona hawa wote ni wakazi Bunju na kila mmoja ana taarifa yake. Sasa hapa sijui tushike lipi?!
Ova

Huyu #zamiluni si mkazi wa bunju. kama haishi #kivule ,basi tuko naye huku kusini! sio dar.
 
Haya yote ni matokeo ya "wapigwe tu" kila mtu anajichukulia sheria mkononi!!!
 
Suala la watanzania kuchukua sheria mkononi sio zuri
Watazichukua wapi hizo sheria? Wahenga waliziweka kwenye vitabu ilu kila raia azipate, pia wakaziundia chombo ili kizilinde. Sasa hicho chombo kimezifungia kabatini na wananchi wakizitaka kila mmoja atanyofoka kivyake na kakifungu chake mkononi.
 
Kwa anayejua atujuze kuna sauti za milipuko mikubwa maeneo ya boko na Bunju. Pia vingora tunavisikia Kwa mbali. Kwa anayejua atujuze nn kinaendelea

si kuna watu wamenasa wakiwa kwenye uzinzi?
 
hawa jamaa wa bodabado ni zao la viongozi wazembe kuruhusu huu using tangu mwanzo ......sasa wanachomewa magari yao Ndio wanashituka.....
 
Kodi kwenye Pikipiki upandishwe ili zipungue

Nchi nyingi zimefanya hivyo, kwa sababu kila mahali pikipiki zimekuwa chanzo cha ajali za barabarani. Hivyo ni wazo zuri kuwafanya liwe na wamiliki wachache wa hizi pikipiki nchini. Ila kwa viongozi wa Bongo watakuambia tukizizuia tutakosa kura za waendesha bodaboda.
Ova
 
Sasa hapo mtu akisema watu wa namna hii "wapigwe tu!" anaonekana amechafua hali ya hewa.

Tairi limepasuka kwa bahati mbaya,mambo yanakuwa hivyo.

JE,HUU NI UUNGWANA?

Nchi ikishatawaliwa na ubinafsi kwa kuanzia ngazi za juu, ujue vurugu kama hizi hazikosekani. Kila mmoja anajikuta akifikiria kujipendelea yeye na watu wake wa karibu tu.
Na kwa kuwa ana ubinafsi, ukimchubua sikio hata kwa bahati mbaya anaweza kukutoa macho ili usimuone tena. Kwa kunielewa zaidi fikiria yaliyompata Kibanda na Dr. Ulimboka. Hapo ndiko nchi yetu iliko.
Ova
 
Back
Top Bottom