Sauti ya watu ni sauti ya Mungu

Sauti ya watu ni sauti ya Mungu

Calamity

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2013
Posts
856
Reaction score
47
Nimekuwa mwanachama wa TANU ( baadaye CCM )tangu mwaka 1972 hadi tarehe 16/06/2013,nimejifunza mengi katika siasa za nchi hii hususani baada ya mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.Katika mfumo wa vyama vingi nchini nimeshuhudia chaguzi(general election) kuu tatu:
1;mwaka 1995 tulibanwa kweli kweli lakini shukrani zimwendee hayati Baba wa taifa kwa kuokoa jahazi!
2;mwaka 2000 upinzani ulikuwa kiasi
3;mwaka 2005 tulishinda kwa kishindo
4;mwaka 2010 tulishinda kwa mbinde!
Matukio(mabomu n.k) mbali mbali yanayotokea hapa nchini yanasababishwa na kazi ya siasa.Siasa sasa imegeuka kuwa vita hasa hasa kwa vijana ambao hawana hata uzalendo na nchi yetu.
Nimekuwa kwenye siasa tangu ujana wangu hivyo ni ngumu sana kuacha siasa ingawa nimeshauriwa sana na familia yangu.Kwa kutambua kuwa bado mchango wangu unahitajika katika taifa langu,nimetafakari sana na kuamua kuanzia tarehe 16/06/2013 nimeachana na CCM na kwa moyo mkunjufu nimeamua kujiunga na JESHI LA UKOMBOZI LA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO(CHADEMA).
Wana JF tusahau yote yaliyopita,kama kuna comment zangu ziliwakwaza tusameane.
Tayari nimechukua kadi ya uanachama ya CHADEMA ambayo kwa ndani kuna majukumu tisa(9) ya mwanachama
Nawakilisha
 
Hongera kwa kuupokea uponyaji.Wakristu tungesema karibu kundini.
 
Bora umeona haujachelewa kabisa mkuu karibu sana kwenye ukombozi sasa ni kupambana tu hakuna kulala.
 
Ni nini kimekufanya hasa ujivue magamba?
mabomu ya arusha yamemuondoa ndungu yangu yaani imeniuma sana...sasa siasa imegeuka kuwa vita sio kama zamani!
jaribu kufikiria mtoto mdogo anakufa,bora sisi tuna wajukuu.
naomba kila mwenye mapenzi mema na nchi hii atafakari!
 
Ccm ni pango la wanyang'anyi mafisadi Wauaji na wapora mali za uma tu.
 
Praise to the Most High!! Kwa kweli kuendelea kusuport ccm ni kuendelea kusali kanisa ambalo tayari ushatambua lina ushetani!
Ila CCM4REAL ni kwamba ndugu yako asingekufa usingebadili msimamo wako!?
Hapo naona sio sahihi. Hivyo wakati wanauliwa wa wengine kwako ilikua sawa tu!?
Mkuki kwa nguruwe....
 
karibu sana mzazi wangu najua umri wako utakuwa ni mkubwa unanizaa mimi,
Nakukaribisha kwa mikono 2 kwamba karibu sana chadema
 
Nimekuwa mwanachama wa TANU ( baadaye CCM )tangu mwaka 1972 hadi tarehe 16/06/2013,nimejifunza mengi katika siasa za nchi hii hususani baada ya mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.Katika mfumo wa vyama vingi nchini nimeshuhudia chaguzi(general election) kuu tatu:
1;mwaka 1995 tulibanwa kweli kweli lakini shukrani zimwendee hayati Baba wa taifa kwa kuokoa jahazi!
2;mwaka 2000 upinzani ulikuwa kiasi
3;mwaka 2005 tulishinda kwa kishindo
4;mwaka 2010 tulishinda kwa mbinde!
Matukio(mabomu n.k) mbali mbali yanayotokea hapa nchini yanasababishwa na kazi ya siasa.Siasa sasa imegeuka kuwa vita hasa hasa kwa vijana ambao hawana hata uzalendo na nchi yetu.
Nimekuwa kwenye siasa tangu ujana wangu hivyo ni ngumu sana kuacha siasa ingawa nimeshauriwa sana na familia yangu.Kwa kutambua kuwa bado mchango wangu unahitajika katika taifa langu,nimetafakari sana na kuamua kuanzia tarehe 16/06/2013 nimeachana na CCM na kwa moyo mkunjufu nimeamua kujiunga na JESHI LA UKOMBOZI LA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO(CHADEMA).
Wana JF tusahau yote yaliyopita,kama kuna comment zangu ziliwakwaza tusameane.
Tayari nimechukua kadi ya uanachama ya CHADEMA ambayo kwa ndani kuna majukumu tisa(9) ya mwanachama
Nawakilisha
je unamkataa shetani na kazi zake zote?
 
Back
Top Bottom