Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,869
- 828,385
Jumuiya ya wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDA imetoa tamko zito kupinga vitendo vyautekaji. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Anangisye yeye amenukuliwa na Nipashe Digital akisema kuwa msimamo wa UDASA si msimamo wa [Uongozi wa] Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Katika kupanua mjadala huo ili kujenga uelewa mpana, tunapenda kutoa uangavu ufuatao:
1. UDASA haijawahi kuwa msemaji wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na haitakuja kuwa msemaji wake. UDASA ni msemaji wa jumuiya ya wanataluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao ni wahadhiri wa ngazi zote (wakufunzi, wahadhiri wasaidizi, wahadhiri, wahadhiri waandamizi, maprofesa washiriki na maprofesa).
2. UDASA ina historia ya kutetea haki, kupinga uonevu na ukandamizaji na hufanya shughuli zake na kuzigharimia kutumia michango ya wanachama wake. Miaka ya 1990s wakati Prof. Chachage Seth Chachage, UDASA ilikwenda Songea kumtetea mwandishi wa habari Adamu Mwaibabile aliyekuwa anashikiliwa kinyume cha sheria na utawala.
3. Wakati hayo ya Mwaibabile yakitendeka, Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam haukuwahi kutoka hadharani kukana au kuunga mkono msimamo wa UDASA kwa kuwa hayo ya UDASA hayamo katika majukumu ya uongozi wa Chuo Kikuu.
4. Kitendo cha Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu kutoka hadharani kujitenga na tamko la UDASA ni ishara kuwa watawala wametoa shinikizo ili kutaka kulipooza tamko hilo kwani Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yupo katika mnyororo wa amri na mamlaka za utawala wa serikali (chain of command).
5. Kitendo cha watawala kujitokeza kupingana na tamko la UDASA kwa kumtumia Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni dalili za kuporomoka kwa ushawishi wa hao watawala miongoni mwa jamii ya wanataaluma
6. Waandishi wa habari wanatakiwa kumuuliza na kumhoji maswali magumu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam badala ya kupokea 'vitini' kama wanasemina na kuchapa bila kuchakata
7. Prof. Anangisye, ambaye ameukana waraka (kwa nafasi yake kama mwanataaluma pale Chuo Kikuu) ni memba au mwanachama wa UDASA. Alichokifanya ni "insubordination" kwa Mwenyekiti wake na ni kukwepa uwajibikaji wa pamoja (collective responsibility) ya jumuiya au wana UDASA! Hii ni ajabu sana.
Soma Pia
Nitumie nafasi hii kuwapongeza UDASA kwa kuungana na Watanzania kupinga vitendo vya utekaji ambavyo vinafumbiwa macho na kuonewa aibu na watawala na mawakala wao. Wanataaluma ni sehemu ya jamii ya Tanzania na wao ni waathirika wa vitendo vya utekaji kwani wanaotekwa ni ndugu zao (watoto, wake, waume, wazazi, wapwa, wajomba, shemeji, bibi, babu, binamu, wachumba, jirani, rafiki zao!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 24 Oktoba 2025; Saa 8:30 alasiri.
HUYU HAPA

- GE2025 - Jumuiya ya wanataaluma wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDASA) watoa tamko kali hali ya kiusalama nchini wagusia Utekaji
- GE2025 - UDSM yailaani UDASA kwa kukosa “Maadili ya Umma” baada ya kulaani uvunjifu wa haki nchini