Sauti Sol: Suzanna

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,448
16,314
Hawa wana wanajua haswaa! Acha tuwape sifa zao! Asiyekubali ni mchawi,tena mwanga, tena yule mwanga anayewanga mchana.

Hili goma ukilisikiliza linatoa mikosi yote, linaponya mapunye, harara, na mba, linaponya kaswende, kisonono hata ngiri, linaua mbu, nzi hata kunguni.

Haya mahadhi ya namna hii ndio muziki asili wa ki-Afrika, muziki ulosheheni mashairi heavy, melody nzuri, ala za mziki zinasikika vizuri kabisa, yani kila kitu kipo on point.

Halafu nyie Sauti Sol, hizi ndio aina zenu za miziki inayowafaa, zile ngoma zenu zingine za kizungu mlikuwa mnakimbizana na upepo tuu, mnatakiwa mkomae na mahadhi haya haya. Tangu mlipotoa ile hit song yenu ya Sura Yako hamkutoa ngoma iloifunika ile, nadhani hii ndio inaenda kuvunja rekodi yake sasa.

BTW mnatakiwa mtulipe kodi wa-Tanzania maana haya mahadhi ni halali yetu. Hizi pigo ni zetu kabisaaa, bahati mbaya hatuna wa kuyaendeleza, naona mmeamua kutake advantage.(joke)

Big up sana kwa hili dude, tunaenjoy sana mimi na mama kija wangu muda huu.

 
Wamekuja kivingine hawapoi
Midnight train
My everything
Insecure
Rhumba japani
Nenda lote
Set me free
....
 
Sauti Sol ni kiboko kabisa , kwenye albam yao ya mpya ya Midnight train kuna ngoma linaitwa Rhumba Japani nalo ni noma kabisa Rhumba limepigwa kwenye beat ya Trap
 
Back
Top Bottom