Saudi Arabia: Polisi wanavyo wapiga wananchi wa ki-Ethiopian

Kwa jinsi tunavyokwenda itafika mahali tutakubaliana, labda niweke sawa kuhusu mkorogo, hapa sikumaanisha kuwa kwenye ukoo wetu hakuna hanayetumia maana ukoo ni kitu chenye marefu na mapana yake. Hapa nilimaanisha kuwa familia ya Bwana na Bibi Kyenju hakuna mtu anayetumia mkorogo.

Ahaaaa, kwa hiyo hao katika ukoo wako wanaotumia mkorogo ili wawe kama watu weupe, wanawabaguwa nyinyi kwa kuwa ni weusi? au wanawapenda sana watu weupe hata wao wawe kama wao?

Ndipo niliposema, akili za samaki.
 
Sina babu mjinga kama hili zee ambalo liliwachuuza waafrika wenzake. Lakini nikuulize swali, nani walikuwa wanamtuma na watumwa hao alikuwa anawauzi watu gani.

Baada ya Afrika ambako ni asili yao, tazama watu weusi wengi wako wapi duniani. Utapata jibu, au nalo inabidi ufundishwe?
 
Kwanini sasa wanawapiga hivyo jamani? Duh!

SWALI LA NJE YA MADA: Hivi Ethiopia kuna Vita pia?Mbona raia wake wanaikimbia nchi kupita kiasi au nchi inaongozwa kidikteta kama Eritrea?Mbona kiuchumi haipo vibaya sana hii nchi kunani huko?

Maswali magumu hayo ndugu yangu. Hao ni wakimbizi wa kiuchumi, sio kisiasa kama walivyo Wacongo na Wasomali hapa kwetu.
 
Mi nimekiri kuwa sijui kiarabu, sasa huyu mwenzio badala ya kunijibu kwa urahisi analeta kejeli nyingi zisizo na mpango ambazo zinanipa hisia kuwa na yeye hajui ila anataka kujifanya anajua. labda wewe unisaidie. Mimi sijui tafsiri ya maneno yafuatayo naomba unipe. kama hakuna tafsiri ya maneno haya kwa kiswahili au maneno haya hayapo katika lugha ya kiarabu vile vile usisite kuniambia.

1. Abd/Abid (عبد)
2. Amah( أمة)
3. ma malakat aymanukum (kama inavyotumika hapa: Qur’an 4:24).

4. vile vile hawa watu mtume anaowaongelea hapa (The Noble Qur'ân An-Nisa 4:221) wanaitwaje katika kiarabu? yaani msamiati unaotumika, nauliza hivi kwa sababu quran naisoma kiingereza, imetumia neno "slave". sasa FaizaFoxy ananiambia neno kama hilo halipo katika lugha ya kiarabu. Mimi siwezi kumbishia nilichotaka anipe neno la kiarabu ambalo mtume amelitumia katika aya hii na nyinginezo kuwadescribe hawa ndugu.
asante.

Tatizo lako ni ubishi wa kijinga. Nna uhakika una matatizo ya kumbukumbu. Nimekuelewesha vizuri sana, kuwa Kiarabu ni lugha tajiri na ni mara chache kukuta neno lenye "derogatory terms", labda utake tu kumkirihisha mtu kwa makusudi. Tofauti kubwa sana na lugha zingine ambazo ukipenda usipende utatumia neno la kudhadhalilisha kwani hayana neno mbadala.

Kumbuka kuwa, biashara ya kuuza na kununuwa watu, mpaka leo hii inafanyika lakini haiitwi biashara ya utumwa, imewekewa sheria na kanuni na imekuja kwa majina tofauti.

Jee unajuwa Tanzania ni nchi ya 29 kwenye rank ya nchi zenye "watumwa" duniani? na Saudi Arabia inayoongelewa humu ni nchi ya 82 kati ya nchi 162 (A number one ranking is the worst, 160 is the best.) Jijuwe uko wapi, pata darsa dogo hapa: Walk Free Foundation – Global Slavery Index 2013 | Findings - Walk Free Foundation - Global Slavery Index 2013
 
Ahaaaa, kwa hiyo hao katika ukoo wako wanaotumia mkorogo ili wawe kama watu weupe, wanawabaguwe nyinyi kwa kuwa ni weusi? au wanawapenda sana watu weupe hata wao wawe kama wao?

Ndipo niliposema, akili za samaki.

Kiswahili nacho ni kigumu, kwa hiyo sishangai kwa kutonielewa nilicho andika.
 
we dada mbona kila kitu unageuza ugomvi? mi naomba hilo neno la kiarabu (unalosema halimaanishi mtumwa) uniambie linaitwaje?

Wewe nimekueleza mara kadhaa u mfinyu wa kumbukumbu na sasa naona kuwa licha ya hiyo, bali pia u mzito wa kuelewa, naomba kukuuliza, Jee, uliwahi kuuguwa sana utotoni mpaka wazazi wako wakakukatia tamaa? jibu utalonipa litasaidia kukupatia njia mbadala ya kukufundisha.

Nilikupa darsa hili, mara hii umesha sahau?:

Nilisha kujibu hilo, naona bado unaendelea kuudhihirishia umma ufinyu wako. Lakini nami sitosita kukuendelezea darsa.

Kwanza kabisa kumbuka hata hao watumwa walipokuwa wakichukuliwa huku kwetu kupelekwa Ulaya, Amerika (wengi zaidi ya kote), Asia na Afrika kwenyewe kwa Kiswahili walikuwa hawaitwi "watumwa". Walikuwa wakiitwa "mahadimu" neno ambalo niilikupa darsa hapo mwanzoni (rejea chini hapa, naona somo halikukuingia kwa kuwa tu u mfinyu wa kumbukumbu).

Neno mtumwa ni neno la Kiswahili linalotokana na maneno mawili, "mtu wa...". Kumbuka hilo pia. Ambalo ni neno geni katika msamiati wa Kiswahili kuliko neno "hadimu".

Nilikufunda hivi:



Kwa hiyo kwenye hiyo blank yako uliyoweka, utajaza neno "hadimu" ambalo linakaribiana lakini si tafsiri ya moja kwa moja (not a direct translation) ya neno "slave" au "mtumwa, kama nilivyokufundisha awali.

Pia kumbuka ni "almost impossible" kujaribu kutafsiri Kiarabu neno kwa neno kwa lugha nyingine yeyote ile hautapata maana kamili, kwani Kiarabu ni lugha tajiri sana (rich language) na adhyim sana haukuti "derogatory words" kama ilivyo kwenye lugha nyingine nyingi.

Kwa kuwa wewe hujui Kiarabu unapoona "translation" ya neno kwa neno ujuwe kuna maneno mengine imeazima kwa yanayokaribia lakini si kwa maana halisi.

Kumbuka, kwa kiarabu hakuna neno kwa neno lenye maana ya "utumwa" na au 'slave", hizo ni "derogatory words".

Jee. unajuwa kuwa neno Mtumwa limetokana na maneno "mtu wa"?
 
Kiswahili nacho ni kigumu, kwa hiyo sishangai kwa kutonielewa nilicho andika.

Labda kigumu kwako ambae si lugha mama kwako, kwangu Kiswahili ni sahali sana tena sana, kwani ni lugha yangu mama.

Hivi haya maswali niliyokuuliza ni magumu sana kwako hata kushindwa kuyajibu? au unaona haya?

Ahaaaa, kwa hiyo hao katika ukoo wako wanaotumia mkorogo ili wawe kama watu weupe, wanawabaguwa nyinyi kwa kuwa ni weusi? au wanawapenda sana watu weupe hata wao wawe kama wao?

Ndipo niliposema, akili za samaki.
 
Maswali magumu hayo ndugu yangu. Hao ni wakimbizi wa kiuchumi, sio kisiasa kama walivyo Wacongo na Wasomali hapa kwetu.

Mbona Waethiopia wenyewe wameshajibu hayo na jibu tulilibandika huko juu, ni hili hapa:
Saudi Arabia is currently rounding up Ethiopian immigrants who do not have permits to stay in the country or whose permits have expired. Those who try to escape from the police are brutally attacked. No body is asking any more why Ethiopians leave their beautiful, fertile country and go to a barren, miserable, ugly country named Saudi Arabia. The answer is that Ethiopia is currently ruled by an evil gang of thugs, more evil than those Saudi police who savagely beat up and gun down poor Ethiopian immigrants such as the young man shown in the photo below.
 
Labda kigumu kwako ambae si lugha mama kwako, kwangu Kiswahili ni sahali sana tena sana, kwani ni lugha yangu mama.

Hivi haya maswali niliyokuuliza ni magumu sana kwako hata kushindwa kuyajibu? au unaona haya?

Ooooh kumbe! lakini unaweza kuelewa alafu ukajifanya kutoelewa.
 
Waethiopia waliokufa kwenye gari walifungiwa na dola? Au dereva aliyekua anawasafirisha! Inawezekana polisi aliuawa na wahamiaji haramu lakini haimanishi polisi watumie excessive force ili kuweza kuwakamata wahalifu, tukubali/ tukatae Saudi Arabia ni wakiukaji wakubwa wa haki za binadamu japokuwa wachangiaji wengine mnaonyesha defensive mechanism ya kidini! Mtu mweusi kwa waarabu ni takataka.
 
Kwenye hiyo operation kuna aliekatwa katwa kama hao Waethiopia ?????????? au unasema ili uonekane umesema ??????, sorry ngoja niheshimu mawazo yako EMT

Hatutakuwa wanafiki mpaka utakapoweka picha za watu waliopasuka vichwani kwa vipigo vya askari,maiti zilizotokana na operesheni kimbunga au vielelezo vya unyanyasaji!!!!!

Na hata ukileta;kukaa kwako uchi hakufanyi uchi hakuondoi sababu ya mwanao kuficha uchi wake!!!!

Otherwise ni uzandiki tu na ujuaji!!!!

Watu kama wewe ndio huwa wanajisaidia kando ya tundu kisa kwake hana choo kizuri!!!!

Is that how you reason? Poor you.
 
Waethiopia waliokufa kwenye gari walifungiwa na dola? Au dereva aliyekua anawasafirisha! Inawezekana polisi aliuawa na wahamiaji haramu lakini haimanishi polisi watumie excessive force ili kuweza kuwakamata wahalifu, tukubali/ tukatae Saudi Arabia ni wakiukaji wakubwa wa haki za binadamu japokuwa wachangiaji wengine mnaonyesha defensive mechanism ya kidini! Mtu mweusi kwa waarabu ni takataka.

Ukitazama picha zote ambazo zina askari wa Polisi wa Sadi Arabia hauioni hata moja inayoashiria wametumia excessive force.

Imeandikwa kwenye vyombo vya habari na link tumeziweka huko juu, kuwa Waethiopia wameanzisha fujo kwa raia wa Saudia na wakauwa raia mmoja na raia nao wakaua murthiopia. Ni nini usichokielewa hapo?

Tanzania raia aliuwa 45 kwa ujinga wake, Msaudi kauwa mmoja kwa kuuliwa nduguye. Bado ni kosa la polisi tu?
 
Kwa hiyo darsa lote unalopewa na maswali unayoulizwa unajifanya huelewi?

Hapo sasa unamdanganya nani zaidi yako mwenyewe?

Maana yangu ni kuwa, wewe unajifanya kutokuelewa unachoelezwa badala yake unaruka ruka kama kinda la ndege.
 
Hizo picha ni baada ya vipigo na hao wahamiaji haramu Kama tunavyo habarishwa kuwa apprehended unaweza kuona watu mapaji ya uso yamepasuliwa hayo ndio matumizi ya nguvu kubwa ya jeshi la polisi, narudia tena kazi ya jeshi la polisi lolote duniani ni kusimamia sheria na sio kuchukua sheria mikononi regardless Kama Askari mwenzao ameuawa ni jukumu Lao kuwakamata wahalifu na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria, kuuawa kwa watu 45 tanzania, nimekuuliza waliuawa na dola? Au dereva aliyechukua pesa za kuwavusha hao wahamiaji haramu na kuwafungia kwenye truck lake wakakosa hewa na kufariki?
 
1. we kweli nimekukubali kumbe wasaudi wanajulikana kwa sura? mi nilidhani kuna wasaudi wahindi, waafrika n.k kumbe woote as long as ni wasaudi we ukiwaona tu unawafahamu!

2. Hoja yako kuwa haiwezekani mtaa mzima (btw, ukihesabu hapo hao ni watu 7 tu, hardly "mtaa mzima") ukavaa mashati na suruali naijibu kwa picha lakini i must say it is a very weak argument.
saudi-street-racing-spectators.jpg

(saudi street racing)
kwenye picha hapo ni saudi na nadhani unaona mwenyewe kuwa ni mtu mmoja tu (wa kwanza kushoto) ndiye aliyevaa tofauti na wenzie (mashati-suruali). Na pia hawa ni zaidi ya watu 7 (ambao we unaita "mtaa mzima"). source ya picha hii hapa.

3. maneno uliyoniambia quote: "The answer is that Ethiopia is currently ruled by an evil gang of thugs, more evil than those Saudi policeThe answer is that Ethiopia is currently ruled by an evil gang of thugs, more evil than those Saudi police who savagely beat up and gun down poor Ethiopian immigrants such as the young man shown in the photo below. " nimeyaona. Ndugu MziziMkavu hakuniomba nimtafsirie.
lakini tafsiri yake ni hii:
"jibu ni kuwa Ethiopia sasa inaendeshwa na genge la majambazi waovu kuliko hata hawa askari wa saudi wanaopiga na kuwaua kwa risasi wahamiaji wa ethiopia kama huyu kijana mdogo aliye pichani".
kwa hiyo nadhani unakubaliana kuwa walio pichani ni wasaudi!

Hata Wachagga nikiwaona nawajuwa kwa kuwaona tu. Vipi wewe? huwajui?

Naona vigezo vingine hukuvipenda au umekiona hicho cha kuwaona tu?
 
Maana yangu ni kuwa, wewe unajifanya kutokuelewa unachoelezwa badala yake unaruka ruka kama kinda la ndege.

Maana yako ni kuwa umekiri huelewi Kiarabu na nimekupa darsa la kutosha na sasa unaelewa Khadim na Khadama, oppss, hadimu na kijakazi ni nini.

Na sasa umeelewa pia kuwa hakuna neno Mtumwa katika kiarabu.
 
Back
Top Bottom