kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,784
- 20,155
Mfalme wa Saudi Arabia, Salman bin Abdulaziz Aal Saud amewaalika wakuu wa nchi 17 kwenda kuonana na Donald Trump, wakati rais huyo wa Marekani atakapokuwa ziarani nchini Saudia.
Trump anatarajiwa kutembelea Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia mwishoni mwa mwezi huu wa Mei. Juzi Jumatano (Mei 10, 2017), Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudia Arabia, kwa idhini ya Mfalme Salman, iliwaalika viongozi wa nchi 17 kutembelea Riyadh wakati wa ziara ya Trump nchini humo. Viongozi walioalikwa kutembelea Saudi Arabia wakati wa ziara hiyo ya Donald Trump ni pamoja na mtawala wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mfalme wa Bahrain, Amir wa Qatar, Amir wa Kuwait na Rais wa Uturuki. Mfalme wa Saudia amewaalika viongozi hao kutembelea Riyadh wakati wa ziara ya Rais Donald Trump kwa madai ya kushiriki katika kikao cha eti nchi za Kiarabu - Kiislamu na Marekani. Swali linalojitokeza hapa ni kwamba, hivi Mfalme wa Saudi Arabia ana lengo gani katika hatua yake hii ya kuwaalika wakuu wa nchi 17 kwenda kuonana na Rais wa Marekani mwenye chuki na Waislamu na wageni, huko mjini Riyadh?
Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, moja ya malengo ya hatua hiyo ya mfalme wa Saudia ni kutaka kuonesha kuwa nchi yake ina nguvu sana katika eneo la Mashariki ya Kati. Mfalme huyo ana nia ya kuwakusanya pamoja wakuu wa nchi 17 waonane na rais wa Marekani huko Riyadh ili amuoneshe Donald Trump kuwa Saudi Arabia ndiyo nchi bora zaidi ya kulinda maslahi ya Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati. Inaonekana wazi kuwa lengo la Salman ni kutaka kumuonesha nguvu za Saudi Arabia, rais mwanagenzi wa Marekani. Hata hivyo ni jambo lililo mbali kuweza wakuu wote hao wa nchi 17 kuitikia mwaliko huo wa mfalme Salman wa kwenda kuonana na Trump nchini Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa wachambuzi hao wa mambo, shabaha ya pili ya hatua hiyo ya mfalme wa Saudi Arabia ni kuanzisha wimbi jipya la chuki dhidi ya Iran ili kwa njia hiyo awaoneshe Wamarekani kuwa Saudia inafuata siasa zao dhidi ya Iran hivyo wasiiache mkono Riyadh. Ijapokuwa hata serikali iliyopita wa Marekani ilikuwa na uhusiano wa kiistratijia na Saudi Arabia dhidi ya Iran kiasi kwamba Washington iliiwekea Tehran vikwazo vikali sana na kuviita kuwa ni vikwazo vya kuifanya kilema Iran, lakini Riyadh haikuridhishwa hata kidogo na makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa baina ya Iran na kundi la 5+1. Saudi Arabia haifichi hata kidogo hamaki zake kuhusu makubaliano hayo. Hivyo hivi sasa mfalme wa Saudi Arabia ameamua kuanzisha upya wimbi la madai ya uongo kama ya kuisingizia Iran kuwa inaunga mkono ugaidi ili avutie uungaji mkono wa Donald Trump kwa Riyadh na kumshawishi azidi kuiwekea vikwazo Iran. Hata hivyo, Saudi Arabia haiwezi kufanikisha uadui wake huo kwa Iran bila ya uungaji mkono wa nchi nyinginezo. Hivyo hatua ya Salman ya kuwaalika wakuu wa nchi 17 za Kiarabu na Kiislamu kwenda kuonana na Donald Trump wakati atakapokuwa ziarani nchini Saudi Arabia ni kutaka kumuonesha rais huyo wa Marekani kuwa si Saudi Arabia pekee inayounga mkono siasa za kiuadui za Marekani dhidi ya Iran.
Shabaha ya tatu ya mwaliko wa mfalme wa Saudi Arabia wa kuwataka wakuu wa nchi 17 za Kiarabu na Kiislamu kushiriki katika kikao kitakachohudhuriwa pia na rais wa Marekani huko Riyadh kwa mujibu wa weledi wa mambo ni kuyatia nguvu magenge ya kigaidi yanayofanya jinai katika nchi kama za Iraq na Syria. Bila ya shaka ni kwa sababu hiyo ndio maana Zaynab al Sahlani, mbunge wa kundi la al Ahrar katika bunge la Iraq akasema kuwa, lengo la kikao hicho cha Riyadh ni kuyaunda upya magenge ya kigaidi kama vile Daesh (ISIS) baada ya kupata pigo la kufedhehesha katika nchi za Iraq na Syria. Saudi Arabia na Marekani zina msimamo mmoja kuhusu magenge hayo katika eneo la Mashariki ya Kati. Hivyo inaonekana mfalme wa Saudi Arabia ameitisha kikao hicho ili sambamba na kuunda muungano mpya, aweze kuzuia kusambaratika na kufuta kikamilifu makundi ya kigaidi katika nchi za Syria na Iraq.
Source;parstoday