Saud Arabia Yahusishwa na 9/1

badison

JF-Expert Member
May 29, 2015
1,450
2,758
Saudi Arabia yahusishwa na 9/11, Obama aitetea

Saudi Arabia imehusishwa na hujuma za kigaidi za Septemba 2001 nchini Marekani lakini pamoja na hayo Rais Barack Obama wa nchi hiyo amelaani mswada wa sharia unaotaka watawala wa Saudia wawajibishwe.

Katika mahojiano na Televisheni ya CBS, Obama amepinga hatua ya Bunge la Kongresi kupitisha muswada ambao utawapa idhini waathirika wa mashambulio hayo ya kigaidi kuwashtaki viongozi wa Saudia. Obama amesema atatumia kura yake ya turufu na hatatia saini muswada wowote wa sharia dhidi ya Saudia.

Rasimu ya sheria hiyo Kongresi ambayo inaungwa mkono na vyama vya Democrat na Republican inalenga kuwapandisha kizimbani waungaji mkono wa ugaidi. Ikipitishwa, sheria hiyo itaruhusu familia za waliopoteza maisha au kujeruhiwa katika hujuma za kigaidi za 9/11 kuzishtaki ndani ya Marekani serikali zinazodaiwa kuhusika na hujuma hiyo au zingine za kigaidi.

Obama yuko chini ya mashinikizo makali kutangaza hadharani kurasa 28 za ripoti ya mwaka 2002 ya Kongresi ambayo imeihusisha Saudi Arabia moja kwa moja na mashambulio ya Septemba 11 mwaka 2001 ambapo zaidi ya watu 3000 waliuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa. Familia za walipoteza maisha katika mashambulio hayo zilimwandikia barua Obama Jumatatu iliyopita na kusema hakuna kisingizio chochote cha kukataa kufichua ukweli.

Seneta wa zamani wa Marekani, Robert Graham, aliyekuwa mwenyekiti mwenza wa tume ya pamoja ya Congress iliyoandika ripoti yenye kurasa 838 kuhusu matukio ya 9/11, hivi karibuni aliiambia televisheni ya CBS kuwa kuna nyaraka za siri ambazo zinaweza kufichua uungaji mkono wa Saudi Arabia kwa watekaji nyara walioangusha ndege katika majengo mawili pacha ya World Trade Centre mjini New York na Pentagon mjini Washington.

Kwa kuhofia kufichuka siri hiyo, Saudi Arabia imesema kuwa itauza mali zake zote zenye thamani ya dola bilioni 750 nchini Marekani iwapo Bunge la Kongresi litapitisha sheria ya kuruhusu kushtakiwa watawala wa ukoo wa Aal Saud. Obama anatazamiwa kuwasili katika mji mkuu wa Saudia, Riyadh Jumatano ya leo ambapo kadhia hiyo itajadiliwa na watawala wa nchi hizo mbili.
 
Back
Top Bottom