SAU: Mbatia ni kibaraka wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SAU: Mbatia ni kibaraka wa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Jun 8, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Chama cha Sauti ya Uma-SAU kimesema kimeshtushwa na uteuzi wa Mkiti wa NCCR James Mbatia kuwa mbunge,uteuzi uliofanywa na Mkiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete.

  Mwenyekiti wa SAU Paul Kyara alisema hata mtoto mdogo atatambua kwamba Mbatia anakwenda kutetea CCM bungeni na kupambana na upinzani.

  Kiongozi huyo wa SAU pia ameunga mkono kauli ya Mbunge wa Nyamagana Ezekiah Wenje aliyotoa kwamba Mbatia ni kibaraka wa CCM. Amesema ili kurejesha heshima yake ni bora Mbatia ajiuzulu uenyekiti wa NCCR ili apate muda mzuri wa kutetea hoja za serikali bungeni.

  Source:Tanzania Daima Alhamisi.
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Good.Hatimaye SAU nao wamefunguka
   
 3. K

  KISAKA MORIS JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo kila mtu analijua halina mjadala' NCCR ni ccm 'C' baada ya CUF kukubali kuwa CCM 'B', pale hamna chama tena. Mbatia ni jirani yangu kule kijijini kwetu Kirua Vunjo lakini kwa ndoa hii tutamwadhibu ipasavyo.
   
 4. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mosses Machali sijui atahaidi nini, kama kauli ya Wenje alisema Wenje asipoifuta kauli na CDM kuomba msamaha atajiuzulu nyazifa zake zote ikiwemo nafasi yake ya ubunge wa Jimbo la kasulu mjini, kwa inavyoonekana yeye ndiye atakayelazimika kufuta kauli zake.
   
 5. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2012
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  siasa za Bongo, du! Yaani Kyala anategeshea naye asemwe kama Wenje...
  Aidha anasahau kwamba watanzania wanakumbuka jinsi mwaka 2005 yeye akiwa mmoja wa wagombea urais, badala ya kutangaza sera zake akawa anampigia kampeni JK. Kwa kitendo hicho yeye alidhihirisha wazi u ccm-sau wake.
   
 6. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  mtamwadhibuje funguka zaidi??
   
 7. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  kama ni jirani yako vip zile ishu alizosema Mdee wakati wa kampeni kumhusu ni za kweli au zilikuwa kampeni tu???
   
 8. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Wote ni vibaraka wa magamba kasoro makamanda wa ukweli CHADEMA
   
 9. M

  Molemo JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo yeye na Mbatia wote ni vibaraka?
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Moses Machali si ni yule aliyebebwa na Kafulila hadi akashinda ubunge?
   
 11. M

  Molemo JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda hii
   
 12. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2012
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kama nilivyosema, hata kuitana vibaraka ni siasa za bongo; mfitini huyu, mchafue yule, wakejeli hawa, gombana na wale, sera za kuendeleza nchi hamna.
  Unaikumbuka hii ya Kyara dhidi ya Mbowe? nadhani itakukumbusha kumwelewa Kyara ni nani, na kwa kiasi gani siasa zake (kama walivyo wengine) ni za kibongobongo tu;
  Kutoka website ya chadema; 27 Agosti 2005
  SAU kwenda kortini kusimamisha kampeni za Mbowe
  Chama Cha Sauti ya Umma (SAU), kimesema kitafungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania Jumatatu, ili kuiomba isimamishe mara moja kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe.

  Kimesema kinataka kampeni za Mbowe zisimame, hadi kesi watakayofungua pia Jumatatu, itakapotolewa hukumu.

  Kesi hiyo ni ya kutaka Mahakama Kuu imwengue kugombea Bw. Jumbe Rajabu Jumbe, ambaye ni Mgombea Mwenza wa Bw Mbowe.

  Kimedai kuwa Jumbe hana sifa ya kugombea na pia vijikaratasi alivyotoa kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), havitoshelezi kuthibitisha Uzanzibari wake.

  SAU kimedai kuwa NEC imemrejesha Jumbe kugombea Umakamu wa Rais, kwa mlango wa nyuma.

  Kimedai kuwa huko Mahakama Kuu, kitatetewa na jopo la mawakili wanne, na kwamba hivi sasa mawakili hao wanasuka madai ya kesi hiyo.

  Hayo yalielezwa na Mgombea Urais wa SAU na Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Paul Kyara.

  Alisema hayo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, uliofanyika Dar es Salaam jana, akiwa na Katibu Mkuu wake, Bw. Jacob Nkomola.

  Bw. Kyara alisema Tume ya Uchaguzi, ilifanya makosa juzi, ya kutupilia mbali pingamizi lao lililotaka Tume imwengue Bw. Jumbe.

  ''Kama mlivyoona kwenye kikao cha maamuzi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ni dhahiri kwamba Jumbe Rajabu Jumbe alishindwa kuudhihirishia umma wa Watanzania Uzanzibari wake.

  Kwa sababu vijikaratasi alivyotoa havitoshelezi kabisa kuonyesha Uzanzibari wake," alisema Bw. Kyara.

  Sijui kama kwa mfano labda angepatwa na tatizo akiwa nje ya mipaka ya nchi yetu, sema akiwa labda visiwa vya Comoro, halafu itokee hali ya kutakiwa kuthibitisha Uzanzibari wake, sijui kama angetoa hati ya TEXCO ya kumlipa nauli yake ya mizigo kwenda Zanzibar na ikatosheleza kuthibitisha Uzanzibari wake, alisema.

  Bw. Kyara alifafanua kuwa katika maamuzi yake, NEC ilijihusisha zaidi na Uzanzibari wa Bw. Jumbe, wakati yeye(Kyara) katika pingamizi lake amekuwa akijihusisha zaidi na suala la mtu huyo Jumbe, kuwa amekosa sifa za kuwa Mgombea Mwenza.

  ''Wacha awe Mzanzibari kwa sababu Tume kwa upande mmoja, imekuwa ikitoa vifungu vinavyopandana kutaka Jumbe awe Mzanzibari.

  Mimi bado naendelea kusema kwamba huyu hana sifa,'' alisisitiza Bw. Kyara.

  Wapinzani wa nchi hii siyo kichaka cha wahalifu, wahuni na watu wasioheshimika, alisema

  Sisi wapinzani tunajiheshimu, tunaheshimika na tunazingatia sheria ya nchi na tunaishi kwa misingi na taratibu hizo. Tupo hapa kuikemea na kuikosoa serikali iliyopo madarakani na hata ile inayokuja, alisema.

  ''Hivyo basi itakuwa ni upuuzi na ujinga uliotopea, kumwangalia macho mtu anayegombea Urais amejaa kasoro kibao, unamwacha aingie Ikulu eti ni mpinzani mwenzangu. Hatufanyi kazi hiyo sisi!,'' alisema.

  Chama chetu hakitumiwi na chama chochote. Chama chetu ni kichanga, lakini ni chama imara na ndiyo maana vyama vingine visivyojiamini, vinapata wasiwasi kwa mambo yetu haya makubwa, alieleza.

  ''Tume imemfungulia Jumbe mlango wa nyuma, ili aweze kugombea.

  Sawa! Msimamo wangu na chama chetu, sasa ni kwenda Mahakamani kutafuta haki," alisisitiza Bw. Kyara.

  Kwa upande wake, Bw. Nkomola alisisitiza ''Tutaizuia CHADEMA mahakamani isifanye kampeni, mpaka tupate tafsiri ya kisheria kuhusiana na suala la Jumbe.''

  Karibu vigogo wote walioanzisha SAU, ikiwemo Bw. Kyara na Bw. Nkomola, walitokea CHADEMA ambako walikuwa ni wanachama waanzishi.

  Naye Mgombea urais kupitia chama cha CHADEMA, Bwana Freeman Mbowe alipohojiwa alisema amegundua kuwa kuna njama zinafanywa na watu mbalimbali ili kuhakikisha kuwa hapati nafasi ya kugombea Urais mwaka huu.

  Akizungumza Jijini na waandishi wa habari, Bw.Mbowe amesema kuwa njama hizo zinafanywa na wapinzani wake wasiokitakia mema chama chake ambao wamekuwa kila kukicha, wakikiletea majungu.

  'Kuna njama za kunifanya nisigombee urais mwaka huu.' akasema mgombea huyo.


  Haya, ukitaka nitakukumbusha aliyoyasema huyo katibu mkuu wa SAU (Nkomola) juu ya vyama vya upinzani mwaka huo huo


   
 13. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Kweli mahakama ya kadhi ni muhimu sana kwa ccm ina wake wengi sana(cuf sau na nccr)
   
Loading...