Baba jayaron
JF-Expert Member
- Jun 29, 2015
- 4,646
- 6,398
inshallah!!Barikiwa Mtumishi.
yaani hapa nataka nitoke mapema ofisini ni wahi kutazama huu mkutano si wa kukosa kwa kweliPaul Semba nilimsikia jana yupo vizuri anatoa ujumbe makini
Nabii Issa sio Yesu ukilinganisha maandiko ya quroani na sifa za Yesu kwenye biblia kwa biblia ni Masihi, mpakwa mafuta, mwana wa Mungu aliye hai, mkombozi wa ulimwengu, mtakatifu, Mungu mwana, mwana kondoo wa Mungu aichukue dhambi ya ulimwengu, Yehova,Ivi Nabii Issa ama yesu mnatumbuaga kama nani nyie wasabato
Habari wana JF,
ni matumaini Mungu ametukirimu uzima, sote tumshukuru,
napenda kuwajulisha ndugu, rafiki na watanzania wenzangu kwa ujumla juu ya mkutano mkubwa unaorushwa kwa njia ya satellite kutoka kanisa la wasabato Kinyerezi Dar es salaam, ambao unarushwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari vya Hope channel Tz, morning star redio na vyombo vingine vya habari.
mkutano huu unamafundisho mengi ambayo yamesaidia watu wengi kufahamu kweli za biblia na lile kusudio la Mungu kwetu sisi wanadamu,
wengi wamefunguliwa wakubwa kwa wadogo na hata makanisa mengi yameongoka kwa mafundisho yake ya KWELI ya biblia.
ni fursa yako wewe mwenye kuhitaji kumjua Mungu na kufunuliwa mapenzi yake, fursa kwako mwenye maswali mengi juu ya Mungu kwani hakuna swali litaachwa na majibu yoote yatatoka kwenye Biblia na supplementaries ya vitabu vya kidini.
hakika hutabaki hivyo ulivyo karibu saaana.View attachment 1013341
Umenichanganya hapo,Inamaana kuna tofauti kati ya Yesu na Issa mwana wa mariamNabii Issa sio Yesu ukilinganisha maandiko ya quroani na sifa za Yesu kwenye biblia kwa biblia ni Masihi, mpakwa mafuta, mwana wa Mungu aliye hai, mkombozi wa ulimwengu, mtakatifu, Mungu mwana, mwana kondoo wa Mungu aichukue dhambi ya ulimwengu, Yehova,
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye biblia Yesu alikufa na kufufuka, na wakristo wooote, na pia alikufa kuibeba dhambi ya ulimwengu! Je kwenye Quroani wanamtambua hivyo??? Kama hatambuliki kwa staili ya wakristo maana yake ni watu wawili tofauti, maana kama nnayemjua Mimi naamini alikufa na kufufuka na wa kwako ni tofauti na hivyo maana yake tunazungumzia watu wawili tofauti, au tunamjua MTU mmoja mwenye sifa zisizoshabihiana kimtazamo!Umenichanganya hapo,Inamaana kuna tofauti kati ya Yesu na Issa mwana wa mariam
Ndio nataka wewe unitofautishie hapo,mbeleni kuna maswali magumu utakumbana nayo,nimesoma biblia na Quran na vyote vitabu nimevielewa,je utaweza nijibia maswali yangu huko mbeleni amaKwenye biblia Yesu alikufa na kufufuka, na wakristo wooote, na pia alikufa kuibeba dhambi ya ulimwengu! Je kwenye Quroani wanamtambua hivyo??? Kama hatambuliki kwa staili ya wakristo maana yake ni watu wawili tofauti, maana kama nnayemjua Mimi naamini alikufa na kufufuka na wa kwako ni tofauti na hivyo maana yake tunazungumzia watu wawili tofauti, au tunamjua MTU mmoja mwenye sifa zisizoshabihiana kimtazamo!
Sent using Jamii Forums mobile app
Kama umesoma biblia na qurani naamini pia umeona tofauti za huyo Yesu na Nabii Issa, nianze tu na walipozaliwa, Yesu alizaliwa horini mwa ng'ombe na nabii Issa kazaliwa Jangwani, yawezekana MTU mmoja kuzaliwa sehemu mbili tofauti? Ntakayoweza kujibu ntakujibu lakini pia ujue kuna wajuzi wengi humu ndani sio lazima nikujibu mimi, utaweza kupata majibu!Ndio nataka wewe unitofautishie hapo,mbeleni kuna maswali magumu utakumbana nayo,nimesoma biblia na Quran na vyote vitabu nimevielewa,je utaweza nijibia maswali yangu huko mbeleni ama
Kuna mahubiri furani hivi nilikua nayafatilia uko YouTube ya mchungaji Paul semba yanaitwa UNABII WA KITABU HIKI ni mazuri sana ila haya kuisha naona vipi nitayapataje mtumishi maana pale ameishia sehemu ya sita tu.Barikiwa sana kwa kutekeleza hili agizo-
Mathayo 28:19-20 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.