Sasa waweza kufanya mitihani ya PMP Tanzania

Sasa waweza kufanya mitihani ya PMP Tanzania

Joined
Apr 23, 2019
Posts
16
Reaction score
10
Hii ni habari nzuri kwa wasimamizi wa miradi, maafisa miradi na wadau wote wa mambo ya miradi. Furia Consulting Ltd tunachukua fursa hii kuwataarifu wadau wote wa sekta ya usimamizi wa miradi kwamba Taasisi ya Usimamizi wa Miradi (PMI) imechukua hatua madhubuti ili kuweza kuwapunguzuia usumbufu na gharama wadau wote wenye nia na dhamira ya kufanya mitihani yote inayosimamiwa na taasisi hiyo (PMI) kwa kuingia kwenye makubaliano na kampuni yausimamizi wa mitihani "Pearson Vue" ambayo ina vituo zaidi ya 5000 duniani ikiwemo Tanzania.

Kwa Tanzania huduma ya usimamizi wa mitihani inatolewa na CATS Tanzania Ltd ambao ni Test Center no. 75468 wanapatikana katika jengo la RITA TOWER gorofa ya 16, Mtaa wa Makunganya Dar Es Salaam.
[RITA TOWER, 16TH FLOOR, MAKUNGANYA STREET, DAR ES SALAAM]

Makubaliano kati ya PMI na Pearson Vue yameanza utekelezwaji wake rasmi 1 April 2019. Hapo awali watahiniwa wa mitihani ya PMP® au CAPM® walilzimika kwenda Nairobi Kenya, South Africa, Mauritius ama ndi za Afrika ya Kaskazini kwa ajili ya kufanya mitihani. Kitu ambacho ilikuwa ni ghali sana na wakati mwingine huwezi kupata ruhusa ya muda mrefu ofisini kwa ajii ya mitihani. Ila kwa sasa huduma imesogezwa kwa ukaribu zaidi.

Furia Consulting Ltd tukiwa wadau wa kufundisha na kuandaa wale wote wenye kuhitaji maandalizi kwa ajili ya mitihani ya PMP®, yaani "PMP® Exam Prep tunafarijika na juhudi hizi za PMI kuwaletea fursa hii hapa Tanzania kwa wote wenye uhitaji wa ,PMP®, PgMP®, PfMP®, PMI-PBA®, PMI-SP® na PMI-RMP® exams kuanzia 1 April 2019 kwa ajili ya kuchagua siku za mitihani (yaani booking/ scheduling exams na Mitihani itaanza rasmi tarehe 1 July 2019.

Tunawakaribisha wote wenye kuhitaji huduma ya maandalizi kwa ajili ya mitihani ya PMP®, CAPM®. Tunarajia kuanza kutoa mafunzo rasmi tarehe 13 May 2019 mpaka 17 May 2019 Dar Es Salaam. Waweza kututembelea kwenye wavuti yetu ya furiaconsulting.com, kwenye twitter, instagram, ukurasa wetu wa facebook, ukurasa wetu wa linkedIn kwa maelezo zaidi na mawasiliano. Asanteni sana.
 
MKO WAPI?
Asante kwa kuuliza.
Training venue ni 9th Floor Tanzanite Park - Victoria. Office zetu ziko Mbweni-Ubungo.
Maelezo ya ziada: tumebakiza PMP EXAM PREP Training session moja tu ambayo inatarajiwa kuanza tarehe 13 August 2019 mpaka 30 August 2019. Muda ni kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 3 usiku kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa. Training inachukua siku 12. Ni ya mwisho kabla ya mabadiliko ya mitaala (syllabus ya PMP). Syllabus mpya (New Exam settings) inatarajiwa kuanza 16 Desemba 2019. Hivyo tunatoa fursa ili wanaojiandaa wapate muda wa kutosha kujiandaa mpaka kwa PMP exam kwa format iliyoko.

Tutarejea tena Januari 2020 kutoa mafunzo kulingana na syllabus na mpangilio mpya wa mitihani. Asante sana!
 
Back
Top Bottom