Imani ni hiyari, sijui wewe unazungumzia wizi gani??????????
Mbona kuna watu wanasali hata makanisa 3 kwa wiki moja,
Kama shida zake anaamini akienda sehemu fulani zitaisha ashindwe kwenda kwani muumini ni kuku kwamba amefugwa?????
Kuabudu ni hiyari sio utumwa.
Hao wanaosali makanisa matatu kwa wiki moja,ndio wanaotupa shida siku wakifa,kila mchungaji anataka aongoze ibada ya mazishi
Mtang'ang'aniaje maiti ili hali roho ishaondoka??????
Mimi nasali makanisa mamiwi na yote yanatambua uwepo wangu.
Moja ni kanisa langu lililonikuza na naliamini hadi kesho, hivo ibada ya jpili utanikuta hapo.
La pili ni kanisa ambalo natumia kuabudu ibada za katikati ya wiki na wao wanajua hilo, tatizo lipo wapi?????
Wacheni watu tutumie uhuru wa kuabudu mwenye maamuzi ya mchungaji gani anizike ni mzazi wangu au mume wangu over.
Acha kutangatanga,kukua kiroho kunategemea uhusiano wako na Mungu wala sio idadi ya makanisa unayosali
Mbona unaninyima uhuru wa wakuabudu???? nikosa kisheria nitakustaki kwa kova.
Sikunyimi uhuru wa kuabudu ni haki yako ukitaka hata kujiunga na free mason ruksa.Lakini ni vyema uchague kanisa moja ambalo utapata nafasi na wewe kutumika,usiishie tu kwenda kukaa kwenye viti na kusikiliza mahubiri,ifikie hatua na wewe uanze kuwahubiria wengine au uwemo kwenye huduma zingine kama maombi,kwaya n.k
Kondoo siyo mali ya Mchungaji mwanadamu, bali ni mali ya Mchungaji Mkuu wa kondoo, Yesu Kristo, ambaye alimwambia Petro, "Chunga kondoo ZANGU", "Lisha kondoo ZANGU" (WAEBRANIA 13:20; YOHANA 21:15-17). Kama Mchungaji mwanadamu hawajibiki impasavyo katika kuchunga na kulisha kondoo wake Kristo, Mchungaji Mkuu Yesu Kristo, anaweza kumyang'anya kondoo hao, na akawaweka chini ya Mchungaji mwingine! (YEREMIA 23:1-4).
Umoja ulioanzishwa na maaskofu wa Kikristo ni jambo la kupongezwa.Lakini itakuwa vyema iwapo umoja huu hautaishia kwenye masuala ya katiba na mambo mengine ya kisiasa,bali pia mambo ya kiimani.Ingependeza iwapo ktk vikao vyao watajadili namna ya kukomesha mchezo wa kuibiana washirika.
Sawa wamekusikia, naona wamekuudhi kwa kuikataa mahakama yako ya kadhi!
Hofu ya kuchukuliana waumini, mtu ana uhuru wa kuabudu popote panapo mpa amani ya moyo kuabudu eneo hilo