Sasa tusiibiane waumini

Sasa tusiibiane waumini

musami

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2011
Posts
1,434
Reaction score
460
Umoja ulioanzishwa na maaskofu wa Kikristo ni jambo la kupongezwa.Lakini itakuwa vyema iwapo umoja huu hautaishia kwenye masuala ya katiba na mambo mengine ya kisiasa,bali pia mambo ya kiimani.Ingependeza iwapo ktk vikao vyao watajadili namna ya kukomesha mchezo wa kuibiana washirika.
 
Imani ni hiyari, sijui wewe unazungumzia wizi gani??????????
Mbona kuna watu wanasali hata makanisa 3 kwa wiki moja,
Kama shida zake anaamini akienda sehemu fulani zitaisha ashindwe kwenda kwani muumini ni kuku kwamba amefugwa?????
Kuabudu ni hiyari sio utumwa.
 
Mtu na akili zako uibiwe.. Kwani unafugwa au umekiwa mzigo....
 
Imani ni hiyari, sijui wewe unazungumzia wizi gani??????????
Mbona kuna watu wanasali hata makanisa 3 kwa wiki moja,
Kama shida zake anaamini akienda sehemu fulani zitaisha ashindwe kwenda kwani muumini ni kuku kwamba amefugwa?????
Kuabudu ni hiyari sio utumwa.

Hao wanaosali makanisa matatu kwa wiki moja,ndio wanaotupa shida siku wakifa,kila mchungaji anataka aongoze ibada ya mazishi
 
Mtang'ang'aniaje maiti ili hali roho ishaondoka??????
Mimi nasali makanisa mamiwi na yote yanatambua uwepo wangu.
Moja ni kanisa langu lililonikuza na naliamini hadi kesho, hivo ibada ya jpili utanikuta hapo.
La pili ni kanisa ambalo natumia kuabudu ibada za katikati ya wiki na wao wanajua hilo, tatizo lipo wapi?????
Wacheni watu tutumie uhuru wa kuabudu mwenye maamuzi ya mchungaji gani anizike ni mzazi wangu au mume wangu over.
 
Acha kutangatanga,kukua kiroho kunategemea uhusiano wako na Mungu wala sio idadi ya makanisa unayosali
 
Mbona unaninyima uhuru wa wakuabudu???? nikosa kisheria nitakustaki kwa kova.

Sikunyimi uhuru wa kuabudu ni haki yako ukitaka hata kujiunga na free mason ruksa.Lakini ni vyema uchague kanisa moja ambalo utapata nafasi na wewe kutumika,usiishie tu kwenda kukaa kwenye viti na kusikiliza mahubiri,ifikie hatua na wewe uanze kuwahubiria wengine au uwemo kwenye huduma zingine kama maombi,kwaya n.k
 
Aisee!!! tatizo muda sina.
 
Sawa na kusema vyama vya siasa visichuliane wanachama, sasa vitakuaje?
 
Kondoo siyo mali ya Mchungaji mwanadamu, bali ni mali ya Mchungaji Mkuu wa kondoo, Yesu Kristo, ambaye alimwambia Petro, "Chunga kondoo ZANGU", "Lisha kondoo ZANGU" (WAEBRANIA 13:20; YOHANA 21:15-17). Kama Mchungaji mwanadamu hawajibiki impasavyo katika kuchunga na kulisha kondoo wake Kristo, Mchungaji Mkuu Yesu Kristo, anaweza kumyang'anya kondoo hao, na akawaweka chini ya Mchungaji mwingine! (YEREMIA 23:1-4).
 
Hakuna kitu kama hicho,labda hujasikia hao maaskofu wanavyopondana kwenye mahubiri yao na kuwaona wengine hawana upako kama njia ya kuwavuta waumini wa makanisa mengine,wala si Bwana anayehusika hapo.Bwana Yesu anafurahi anapoona kanisa linajaa kutokana na watu wapya wanaookolewa na wala si wanaotangatanga kwa kubadilisha makanisa
 
Waumini huwafuata Wamiliki wa hizo Cults ie ufufuo, terbanacle,full baibo, upako, sloam, mlima wa moto, sunlight etc. Wakifa hizo Cults nazo zinakufa. Ziko kwenye miji mikubwa tena eneo moja tu. Kawe, mwenge, tegeta, kibangu,mikocheni
 
waumini hufuata wamiliki wa hizo cults ie terbanacle, full bibo, upako, mlima wa moto, sloam ,ufufuo. Wakifa basi cults zao hufa. halafu ziko tu mjini eneo moja ie kawe kibangu, mikocheni mwenge
 
Umoja ulioanzishwa na maaskofu wa Kikristo ni jambo la kupongezwa.Lakini itakuwa vyema iwapo umoja huu hautaishia kwenye masuala ya katiba na mambo mengine ya kisiasa,bali pia mambo ya kiimani.Ingependeza iwapo ktk vikao vyao watajadili namna ya kukomesha mchezo wa kuibiana washirika.

Sawa wamekusikia, naona wamekuudhi kwa kuikataa mahakama yako ya kadhi!
 
Hiyo mahakama iwepo ama isiwepo haitaweza kubadili imani yangu kwa Bwana Yesu Kristo.Ninacho waasa hawa Maaskofu watumie umoja wao kukemea tabia iliyozoeleka ndani ya jumuia ya wakristo nchini,ya kukashifiana kuonesha kwamba madhehebu mengine yana mapungufu,lengo likiwa ni kuwavuta waumini.Sasa kwa Kuwa sasa kuna huu umoja hii tabia ife.Kama unataka waumini nenda kawaubirie wapagani.Umoja usiwe kwenye kudai mambo ya kidunia peke yake
 
Hofu ya kuchukuliana waumini, mtu ana uhuru wa kuabudu popote panapo mpa amani ya moyo kuabudu eneo hilo
 
Ni kweli kabisa kuna huo uhuru wa kuabudu,ninachosisitiza kwenye vikao vyao waonyane kuhusu mahubiri ya kukashifiana kwa lengo la kuvuta waumini wa makanisa mengine,huo umoja wao usiishie kudai katiba
 
Back
Top Bottom