Sasa turudi kilingeni


VUTA-NKUVUTE

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
5,984
Likes
7,851
Points
280
VUTA-NKUVUTE

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
5,984 7,851 280
Ya vyamani yameshatokea.Sisi CCM tulimfukuza uanachama Mwakilishi wa kule Zanzibar.Yakapita.CHADEMA wamewavua uongozi (na wala si uanachama) viongozi wake.Mambo yao yanaendelea kichama. Mambo ya majukwaani yanaendelea. Vyama vyote vikubwa vya kisiasa nchini vinajipanga na uchaguzi wa mwaka 2014 (Serikali za Mitaa) na 2015 (Uchaguzi Mkuu). Kila chama sasa kinajipanga kwa mbinu ima halali au batili kukabili wapinzani wake. Hapa CCM;pale CHADEMA. Hapatoshi!

Ya ndani ya vyama yasitusiamishie fikra zetu.Tuna mengi ya kujadili kama Taifa. Lakini,tunategemea viongozi wetu wa kisiasa kutuongoza. Yapo mambo ya gesi asilia Mtwara,mgawo wa umeme na kadhalika. Bado tuna nafasi,sababu na nia ya kujadili mambo yetu. Hakuna muda wa kupoteza.Turudi kilingeni!

Sekretarieti ya CCM inapuyanga nchi nzima kutangaza Ilani na Sera za CCM. Kinana yuko mbele akiongoza viongozi wengineo wa chama. Mikutano inafanyika;watu wanafika na sera zinasikika. Wananchi wanaelewa. Wanatunza kumbukumbu.Wanaangalia maisha yao wakifananisha na maneno ya viongozi wao. Sasa hawasemi.Watasema 2014 na 2015.

CHADEMA nao wametuma vikosi-kazi mikoa mbalimbali nchini. Kipropaganda,wanachorwa kama wapeleka ujumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA kuhusu suala la akina Zitto. Timu husika zinawaambia wananchi uimara,upekee na utofauti wa CHADEMA na CCM katika kufanikisha maisha mazuri kwa watanzania. Wanasikilizwa. Wanaeleweka.Watapewa jibu lao kupitia boksi la kura hapo 2014 na 2015.

Hakuna haja ya kuzushiana na kutengenezeana Propaganda. Kama chama kina viongozi safi,sera imara na mikakati kabambe,hofu inatoka wapi? Ilani inayotekelezeka;viongozi wanaoheshimika na mambo mazuri ya kusikika,woga wa nini? Tafadhali wanasiasa wetu,siasa ni hoja.Si vihoja visivyo na haja.Turudi kilingeni!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Mpaka Kieleweke

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Messages
4,134
Likes
74
Points
145
Mpaka Kieleweke

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2007
4,134 74 145
Ujumbe huu aupate Mwigulu Nchemba , ambaye alipanga kumuua Benson Kigaila leo Kigoma , kumbe amejikuta ka rushwa asiye husika bomu na kuja hapa na Breaking news kuwa Kigaila amenusurika kufa huko Kigoma .......wakati Kigaila yupo kanda ya Nyanda za Juu Kusini akichapa kazi....

CHADEMA itayafikia Majimbo 103 kwa ajili ya kujipanga , ....wao waendelee na Propaganda zao...
 

Forum statistics

Threads 1,263,320
Members 485,844
Posts 30,148,010