Sasa tunaishi kwa ndoto!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa tunaishi kwa ndoto!!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Wakuletwa, Mar 28, 2011.

 1. Wakuletwa

  Wakuletwa Senior Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndoto, ndoto, babu anatibu kwa sababu kaoteshwa! Yes ameoteshwa kuponya magojnwa matano sugu! Hii ni kwa mujibu ya wenzetu walioenda huko kupata tiba. Siwalaumu hata kidogo wagonjwa kukimbilia huko hebu jiulize ingekuwa wewe unaumwa gonjwa lisilo dawa halafu unasikia kuna mtu anatibu ugonjwa huo ungefanyaje?
  Ila nawalaumu sana watu wanaowatoa wagonjwa hospitali kuwapeleka huko na matokeo yake kuwasababishia hayo.

  Kikombe cha babu ni uthibitisho tosha ni aina gani ya taifa ambalo tunalo. Hatuamini tena katika utafiti na uchunguzi bali katika ndoto na imani. Hii ni hatari na ndio maana kuna wajanja wachache kwa kugundua udhaifu huo wamegeuka mamilionea. Hujawaona wachungaji wakitembelea magari ya thamani kubwa kwa sadaka za waumini wao? Mashekh wakimiliki majumba makubwa makubwa kwa sadaka za waumini wao? Hao wametumia udhaifu wetu wa imani. Siku chache zilizopita gazeti la The citizen liliorodhesha nchi ambazo watu wake wanapenda sana ushirikina katika Afrika Tanzania tupo kwenye tano za juu na leo kikombe cha babu kimethibitisha.
  Vyovyote itakavyokuwa iwe ni tiba kweli au au vinginevyo, madhara yake yatakuwa ni makubwa kuliko faida.
  Hebu tujifunze kufanya tafiti kwanza halafu tuhangaike na matokeo ya hizo tafiti, itakuwa heri sana ikibainika dawa ile inatibu barabara. Lakini ikiwa kinyume chake sijui itakuwaje?
  Ndugu zangu hakuna asietaka tiba na nina hakika ni familia chache sana kama zipo ambazo hazina mgonjwa wa magojwa hayo 5 ambayo babu anatibu lakini tuvute subira, maana waswahili wanasema subira yavuta heri.
  Ni mtazamo tu.
   
Loading...