Sasa tumefika kwenye fundo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa tumefika kwenye fundo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwankuga, Feb 9, 2011.

 1. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Sasatumefika kwenye fundo.Mambo hamkani si shwari katika nchi yetu.Wakati mgawo wa umeme ukiendelea kote nchini na harakati za DOWANS,hali ya maisha mtaani imekuwa mgumu,bidhaa nyingi zimepanda bei,huku shughuli ndogo zilizokuwa zinawapatia kipato watu wa hali ya chini zikisimama hadi hapo mgawo wa umeme utakapoisha.

  Serikalini na nako mambo si shwari,mgawanyiko wa wazi na kificho wa baraza la mawaziri una jambo moja kuu kwetu,kuwa mfumo tulionayo umeshindwa kufanya kazi,huku maisha ya wananchi yakiendelea kuwa yaleyale.Maovu mengi yanafanyika serikalini bila ya wananchi kuchukua hatua zozote,pengine kwa kujua au kutojua au ni kwa sababu hatujui cha kufanya.Scandals km vile IPTL,SONGAS,AGGREKO,RICHMOND/DOWANS,MEREMETA,TANGOLD,RADA NK,zilitosha wananchi kuamuka na kuchukua hatua zaidi,lakini tuko kimya.

  Wakulima wanaendelea kunyauka na kunyonywa na hakuna anayewatetea,walaanayewaamusha.Leo tunasema KILIMO KWANZA,lakini wengi tumeshuhudia hizo vocha za pembejeo zikiangukia kwa watu wenye uwezo huku wakulima wa kawaida wakiachwa bila mtetezi wao.

  Wafanyakazi wa kati katika taasisi za umma,mishahara yao ni kiduchu na haikidhi mahitaji ya kibinadamu.Makato kama vile kodi ya kipato na mengine ya kinyonyaji kama vile mifuko ya Penseni,kuchangia vyama vya wafanyakazi na bima ya afya haiwezi kuvumilika kamwe.

  Wachuzi wadogowadogo au wamachinga hali zao ni mbaya zaidi,kutwa wanafukuzana na wagambo kama vile ni waharamia.Matokeo ya shule zetu za kata yametuonyesha dhahiri kuwa elimu yetu ipo mashakani,na hivyo kuwa tishio kwa mustakabali wa nchi yetu.

  Pengo kati ya masikini na matajiri linazidi kupanuka kwa haraka sana,huku viongozi wa kisiasa na kiutendaji wakizidi kuneemeka na rasimali za wananchi.Maadili ya viongozi yamepolomoka kwa kasi ya ajabu.Uharamia umepewa nafasi zaidi katika kuendesha nchi,ambapo inawezekana kabisa watu ambao hawako serikalini lakini ni wakwasi wakatumia nafasi zao kujinufaisha kupitia taasisi za umma.Rais cheo ambacho ni kikubwa katika nchi,hakina heshima tena,na wala cheo si dhamana tena.

  Bila shaka tumefika kwenye fundo,wananchi wamekuwa na mafukuto mioyoni mwao lakini hawachui nini cha kufanya.Wanachi walio wengi hawaridhiki na namna serikali inavyoendesha mambo japo tunatofautina kiitikadi,lakini bahati mbaya sana ugumu wa maisha hauchagui chama.

  Tumefika hapa kwa matakwa ya kikundi cha watu wachache.Wanachotaka wananchi na mabadiliko au maendeleo katika maisha yao,issue sio chama gani kiongoze.Tunashindwa kuchukua hatua kwa sababu za kichama zaidi,huku kila upande ukivutia kwake.

  Ifike hatua tuseme lugha moja tusahau habari za vyama,tuzungumze kuhusu ukali wa maisha na namna ya ku-solve.Mifumo ndiyo iliyotumikisha hapa.Tuungane kwa pamoja kupinga udhalimu.Watu toka serikalini hawanatua sana,wanajua hatuwezi kufanya kama yaliyofanyika Tunisia.

  Tumeongea sana,tumeandika mengi na kupishana sana lakini bado viongozi hawawezi kutusikiliza,wametupuuza na kutudharau.Sasa ni muda wa kutafuna fundo,wananchi tuamue kuwalamizisha viongozi kutusikiliza.Mass demostrations(popular democracy) ndio suluhisho.Tupunguze kulalamika na kulia,tufanye kazi tuingie barabarani.Huu ni mtazamo wangu na niko tayari kuusimamia.Naomba kuwasilisha.
   
 2. K

  Kidagaa Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inauma sana kuona yale yaliyo ya msingi yanaachwa kwa kupitishwa taratibu mbovu. Wengi tunadhani wakati wa mabadiliko ulikuwa sasa lakini bado tunao watu ambao wanafikiri nyuma ya wakati. La msingi sasa hatutakiwi kupoteza ufikirivu wetu, tuendelee kusema yaliyo ya ukweli na kutenda yaliyo sawia tukijua kwamba wale wote wanaotaka yaendelee yaleyale watakwisha kwa nguvu za umma tu.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Leo nimepitia sheli ghafla nikapigwa bumbuazi kukuta petroli imepanda kutoka 1820 hadi 1840!...
  Nilitaka kuwajia juu wahudumu, lakini nimerudisha moyo baada ya kuchanganya na zangu!
  Sasa tukilipa hiyo Dowans wiki ijayo nadhani Petroli itakuwa 2000/=
   
Loading...