Wakati ule alipochukua uamuzi mgumu wa kujiuzulu, alisema, " ETI KISA NI UWAZIRI MKUU" ni kama vile alikuwa mtu aliyekuwa ameshinikizwa na mtu fulani kujiuzulu ili kupisha kelele za watanzania baada ya kubaini nae alihusika katika kashfa ya Richmond.......lakini wakati ule nilidhani Lowasa alikuwa hajui analofanya kwa kukubali kwake kuwajibika hadharani akasema, ...."najiuzulu"..Wengi tulidhani baada ya kujiuzulu Mhe. Lowasa mambo ya Nishati ya Umeme katika nchi hii yata kaa vizuri kwani ni kipindi kile kile ambapo tulitangaziwa mikakati kibao Bungeni na Kwenye hotuba ya Mhe. Rais ile ambayo sasa hatuisikii ya kila mwezi kuwa tatizo la umeme litakuwa historia...
Kumbe sasa kwa fikra za wazi mnaweza kubaini tatizo halikuwa na wala sio Lowasa..., Lowasa alijitahidi kadiri ya uwezo wake kutimiza maagizo ya mkuu..haya tunayaona sasa ni yale yale yaliyomtokea Lowasa, yamemgusa Mhe. Waziri Mkuu mwingine Pinda, sasa kwa staili nyingine ya posho za kuwahonga wapitisha bajeti kwa maana ya kyufunika kombe, Awali Mhe. Waziri Mkuu alionyesha kughazabika eti haya mambo ya "posho za kulainisha maamuzi" hayapo Serikalini. .., safari hii kupitia Mtendaji Mkuu wa Wizara ile ile ya Nishati Bw. David Jairo..huyu ambae alikuwa ni Mtumishi muadilifu, mtaalamu wa Sheria, ambaye alipata kufanya kazi kwa karibu sana na Mkuu wa nchi kule IKULU akiwa pia na Mhe Katibu Mkuu Kiongozi wa sasa ambaye ametangaza kuanza hatua za kuwajiwabisha Jairo ilihali nafasi yake ya Ukatibu Mkuu Nishati inatangazwa kupangiwa mtumishi mwingine (Eliakim Maswi)...Hapo napo tena ni funika kombe mwaharamu apite kama ilivyokuwa kwa wale watendaji waliotajwa kuhusika na kashfa ya Richmond...(Jairo atapangiwa kazi nyingine) Home
.Eti Jairo sasa anaonekana kikwazo cha upatikanaji wa UMEME, kama ilivyiokuwa kwa Mhe. Lowasa, Je, ni wapi Jairo alipata ujasiri wa kuandika yale aliyioandika kama haikuwa mazoea au hakupata maagizo yoyote toka kwa mtu fulani wa juu yake? ..Mhe, Msabaha wakati ule nae aliponzwa kwa kunadika ...lakini alipokuwa akichomoka akitoa kauli ambayo iliashiria kuwa nae aliagizwa na mkubwa wake wa kazi kufanya yale aliyofanya na wakati ule tukasema ni "Lowasa tu' Lakini kauli za kujiuzulu kwa Lowasa nazo zilionyesha kana kwamba nae aliagizwa kufanya vile na mtu mwingine wa juu yake ...ni nani? hatukujua!!...... Sasa tumefumba macho kabisa, hatuna mjadala tena juu ya kulipa sdeni la Mrithi wa RICHMOND yaani DOWAS hasa baada ya Wakuu wa Dunia hii (Marekani) kuingilia kati kwa staili ya Symbion Power, ...........tunamjadili Jairo..... Hatujui kumbe hapa tulipo, tunachohitaji ni umeme, umeme kwa gharama zotote zile (hayo ndio maamuzi magumu ambayo Lowasa aliyasimamia na yakamfanya aonekane hafai). Tulidhani Lowasa ndio kikwazo cha maendeleo ya nchi hii, eti kumbe hata baada ya kujiuzulu kwake bado matatatizo ni yale yale tena sasa ni mazito zaidi..tumeona bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini imeashindwa kupita kwa kile kinachodaiwa kukosa mikakati ya kuondoa tatizo la Umeme na wakati huo Katibu wake Mkuu kung'olewa kwa kashfa ya kutaka kuiwezesha bajeti hiyo ipite kimya kimya...eti sasa si Waziri Msabaha, Karamagi wala Lowasa wameshiriki katika hili sakata....
MAJI ziwa Victoria mpaka KAHAMA pamoja na kuwepo mkataba wa kikoloni kuzuia watz wasitumie maji yaleNia si klumtetea Lowasa wala Mtu yeyeote ambae anatuhumiwa kwa kuchangia kurejesha nyuma maendeleo ya nchi hii. Ila kwa hali ilivyo sasa hata kama huwezi kushawishika unaweza kuona jinsi ilivyotofauti kuwa na Kiongozi wa mfano wa Lowasa katika mfumo wa utawala wetu...ni mangapi tumekuwa tukielezwa kwa nadharia na hakuna vitendo? Lowasa pamoja na ufisadi wake lakini aliweza kuthibutu katika mambo mengi magumu: (i) alidiriki kulitafutia ufumbuzi tatizo la umeme hafi likamchafua kisiasa: (ii) alibuni mipango mbadala ya kuzuia foleni jiji la Dar ikiwemo njia tatu na kutambua barabara za pembeni ya mjini ambazo sasa zimeshindwa kuendeklezwa; (iii) alisimamia mpango wa ujenzi wa shule za kata na zahanati japo hazikuwa na mtizamo wa muda mrefu ikiwemo kuandaa wauguzi na waalimu;(iii) Ndie aliesaidia kwa kiasi kikubwa kuleta ufumbuzi wa tatizo la maji kwa baadhi ya miji japo hali bado inasuasua;(iv) aliwezesha mpango wa ruzuku za pembejeo kwa wakulima japo uzalishaji katika sekta ya kilimo haukjakaa vizuri; (v) aliweza kuchukua maamuzi magumu ya papo hapo ikliwemo kuwafukuza watendaji wabovu pasipo kujali ni nani mwenye dhamana ya kuwachukulia hatua za nidhamu (juzi mmesikia wenyewe Mwenzake akitamba i hadharani "kama yeye angekuwa Rais angemfukuza kazi Jairo) lakini baadae tunatangaziwa amesimamishwa ili kuchunguzwa kwanza....na wanaomchunguza ni wale wale wanaoendelea kutuhumiwa kuhusika katika kashfa nyingine ikiwemo kushindwa kushauri ipasavyo kwenye suala la Richmond...
Mkuu jaribu kutumia kichwa kufikiri na siyo "marufi"Ngoshwe, kama hakufanikiwa katika yote hayo uliyoainisha juu tena iweje mtu huyo awe ni msafi? Ina maana mipango yake ni ya kukurupuka na alikuwa hasikilizi ushauri, mambo ambayo yalimgharimu na yanendelea kumgharimu.
Kufukuza watu bila ya kufuata utaratibu inadhihirisha wazi kwamba alikuwa hafahamu vipi serikali ilitakiwa ishughulikie issue kama ile. Itakuwaje yeye Waziri Mkuu amfukuze engineer wakati kuna viongozi wa kati wengi tu ambao wangeweza kufanya hiyo shughuli? Sasa WAziri Mkuu akianza kupita njiani na kufukuza watu ovyo ovyo unadhani hiyo ndiyo ingekuwa bora?
Si umeona matokeo ya kufanya vitu bila ya kufuata sheria? Matokeo yake ni Serikali ndiyo inalipa tena fidia kubwa zaidi ..... mfano yale majumba ya masaki yaliyovunjwa imefikia wapi?
Jamani tuenzi maneno ya mwalimu juu ya Lowasa tusije pata laana ya baba wa taifa uko aliko.
Nasikia alimwambia kijana utajiri wote huu umeutoa wapi?
tatizo halikuwa lowasa, lowasa ni safi ndo maana atakuwa rais wa nchi/inji hii mwaka 2015. period.
ona alivyokuwa anachapa kazi, tungeendelea na kasi ile, tungekuwa mbali pamoja na kwamba wengi wangekuwa wameumia, napenda rais wa aina ya lowasa kuliko rais wa aina ya kikwete......it hasn't been proven kwamba lowasa alikula rushwa hadi leo, rushwa hiyo haionekani, wala fungu hilo la kumbi halionekani.....which means jamaa walimwonea tu, ndo maana hata anavyoondoka alisema naachia ngazi, tena kwa majonzi akijua hakufanya kitu kwa nia mbaya....kama yalitokea matatizo yalitokea kwasababu tu kiutendaji na haikuwa necessary kwenda mbaliiii kiasi kile kwa kina mwakyembe na wengine....