Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,991
Inaonekana mastratejisti wa CCM hawajaelewa uzito wa Waraka wa Makatibu wakuu wastaafu wa CCM, wazee Kinana na Makamba. Ukiusoma huo waraka katika hali ya kawaida tu, utaona kwamba waliouandika ni watu wenye weledi na wametafakari sana na kuchagua maneno na sentensi za kutumia. kuna strateji nyingi sana zinazofikirisha. nitataja baadhi tu. kwamba waraka umeelekezwa kwa baraza la ushauri pia ni strateji. Kwamba barua imewekwa wazi hadharani, nayo ni strateji.
Kilichotarajiwa ni kwamba wahusika ndani ya CCM nao wangetafakari sana. moja ya hatua za haraka ingekuwa ni kuwapongeza hao walioandika waraka, kwamba wametumia haki yao ndani ya chama, na kwamba chama cha CCM kama Baba wa Demokrasia, kitafanyia kazi malalamiko yao kwa mujibu wa taratibu za chama. umuhimu wa kauli ya namna hii ni kuliondoa SAKATA hili kwenye uwanja wa nje na kulileta ndani ya chama. Hii ingesaidia kukipa chama nafasi ya kurekebisha makosa yaliyofanywa kwa kuwaruhusu akina Musiba wakitumbukize chama kwenye UVUNDO.
Kinyume chake, tumeshuhudia ubabaishaji na ukosefu wa weledi na umakini, wa kiwango cha juu kuwahi kuonekana. Katika mwendelezo wa utendaji wa KIBASHITE, zimeonekana clip zikiwa na udukuzi wa mawasiliano kati ya akina Nape, Kinana, Mzee Makamba, Ngeleja, Membe, nk. Nadhani lengo hapa ni KUWAZODOA na KUWAANIKA akina Kinana na Makamba na hivyo kutia mchanga kwenye waraka wao. Hili ni kosa kubwa sana kistrateji.
Kwanza kuna matatizo mengi ya kisheria kwenye udukuzi huo, ambao unaleta complications nyingi sana. Pili inathibitisha kwamba kweli CCM inatumia MBWA KOKO kufanya kazi zake, na kuwahalalisha hao MBWA KOKO wote kwamba wanatumwa. hata kauli ya Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ali, inaonekana kuthibitisha kwamba chama kinatumia magenge machafu. Hatujaona akina Musiba wakikemewa, lakini kwa kuwakemea walalamikaji, inathibitisha madai ya Waraka kwamba hawa akina Musiba wanalindwa na hawawezi kuguswa na mtu yeyote au taasisi yoyote ya hapa nchini. Pia Bashiru anaonekana kutumia maneno ya kwenye hizo clip kutoa matamko na makemeo yake. kwa hiyo hizo clip ni kama zimetolewa IN ADVANCE ili kusafisha njia.
Tatu, hizo Clip zinatoa ujumbe mwingi sana tofauti na malengo ya waliozirusha. Kama kweli watendaji wakuu wastaafu wa CCM wanaweza kudukuliwa, ni fedheha kubwa kwa CCM. CCM ina sifa ya kulinda wastaafu wake. Leo kulikoni? na mbaya zaidi, kwa kusikika hadharani wakiongea hayo wanayoongea, ni ishara kwamba CCM ipo kwenye hali mbaya sana. EEeee, unawezaje sasa ukainuka na kudai kwamba CCM ni imara, kama watangulizi wako na wasaidizi wao, tena wanaokuzidi kwa ukongwe na weledi katika kukitumikia chama, wamefikia hatua ya kukata tamaa kiasi hicho, na kutaharuki kiasi hicho? Yaani CCM inaruhusu watu wa ngazi za juu hivyo kusikika hadharani wakitoa ya moyoni? huo ni upungufu mkubwa sana hata kijasusi. Kwa kweli kitendo cha kutoa clip hizi kumewathibitisha hao watendaji wakuu na kuimarisha madai yao, na kwa upande mwingine, kimefichua uchafu wa ndani kabisa wa CCM kwa namna ambayo haijawahi kutokea.
Lakini kuna kitu kibaya zaidi ya yote hayo kilichofichuliwa kwenye hizo clip, kiasi kwamba naanza kuhisi kwamba pengine aliyefanya hivyo ana akili zaidi kwa maana kwamba ana lengo la kumhujumu bosi wake kwa kumwanika hadharani!!! Kitu hicho ni kumhusisha Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, kwamba naye ameonesha kukerwa na hali ya mambo ilivyo. Sasa tunajua kwamba Rais Mkapa aliwahi kumkosoa Magufuli hadharani siku ambayo watendaji wakuu wastaafu waliiitwa ikulu na Rais Magufuli. Mkapa alisema kwamba hii ni Serikali ya CCM, na siyo ya fulani. sasa tunajua kwamba Mkapa ndiye BABA MLEZI wa Magufuli. kama naye ana kichefuchefu, basi hali ni mbaya sana
Hapa naona jambo moja tu linaloniingia akilini. Mastratejisti wa CCM wamewekwa pembeni na ni Magu Mwenyewe anayeshika usukani na kuelekeza nini kifanyike. hiyo ndiyo consistency ninayoiona katika madhila mbalimbali yanayoikuta nchi yetu hivi sasa. Najiuliza CCM inajua inakokwenda? lakini mbaya zaidi, Taifa la Tanzania linakwenda wapi?
Sasa tunashuhudia msururu wa wachumia tumbo lukuki wakimsifu Magufuli. lakini ukweli tumeujua. Ni wakati muafaka watanzania tuwe na msimamo kama CAG Prof. Assad. Tutetee maslahi ya Taifa letu, ambayo siyo maslahi ya Magufuli