Sasa ni wakati wa kuanza upya atcl | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa ni wakati wa kuanza upya atcl

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, May 28, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,061
  Likes Received: 5,552
  Trophy Points: 280
  SASA NI WAKATI WA KUANZA UPYA ATCL

  Na mhariri Cosmus Ruhembiza
  Nipashe

  Juzi katika ukurasa wa kwanza wa gazeti la nipashe kulikuwa na habari inayosema “”ATCL NI BOMBA LA KUFUJA FEDHA HAZINA”” ikielezea taarifa zilizotolewa katika kamati ya bunge ya fedha na uchumi na afisa wa hazina msajili jinsi shirika hilo la ndege lilivyokuwa mzigo mzito kwa hazina, Afisa huyu tunaethubutu kusema ni jasiri,alisema wazi kwamba ATCL imekuwa ikijiendesha kwa hasara kubwa mwaka wa pili sasa huku ikitegemea kupewa fedha kutokahazina kwa ajili ya mishahara,na garama zingine za uendeshaji kama vile ada na malipo ya sheria na pesa za vifaa vya ndege

  Kauli hiyo tunaiona kama ni ujasiri sababu ofisa huyo anajua vilivyo jikoni kwamba serikali imekuwa na mtazamo tofauti na huo juu ya ATCL,Serikali kama waziri kawambwa anavyosema wanataka kufufua ATCL na kwasasa wanaitafutia mbia wa kichina huku akijua fika mchina alishakuja mara tatu nakuondoka na kusema mbele ya rais na mbele ya Tv za watanzania kwamba wizara husika inashiriki kumhujumu kuichukua ATCL….huu ni uongo wa kila siku wa Waziri Kawambwa ambao ulimsababisha hata kutoleana maneno machafu na Mh nyanganyi akiwa anaulizwa na kamati ya miundo mbinu…amekuwa si mkweli matokeo yake anaaibika kwenye kamati ya bunge..amekuwa akifwata kila siku kutoa pesa za mtaji wa atcl matokeo yake akisema tunajiandaa kuto pesa nyingi tu , ,kama mtaji, Kuna mbia wa kichina,kihindi,mwarabu mpaka leo hii ambapo bodi ya ATCL imekwisha muda wake!!!ingawa anajua fika kiwango cha madeni ya ATCL inakuwa kazi ngumu kumpata mbia ikizingatiwa mashirika mengi ya ndege kwa sasa yako kwenye msukosuko.mkubwa kiuchumi

  Tunajua ni fahari kwa taifa kuwa na shirika lake la ndege,,lakini fahari hiyo lazima iwe na maana kwani kuwa na shirika mzigo kama ATCL ambalo alijiendeshi lenyewe zaidi ya miaka miwili hata kuweza kumudu gharama zake muhimu achilia mbali kutoa gawiwo la serikali,haina maana ,ni hasara ,ni MATUMIZI MABAYA YA RASILIMALI ZA UMA kwa maana ya KODI za wananchi ambazo zingeweza kuelekezwa kwenye mambo mengine muhimu zaidi

  Hakuna asiejua historia ya ATC kabla ya kuwa ATCL tangu mwanzoni mwa miaka ya tisini tumekuwa na juhudi kubwa za kuvunja nguvu ndogo ya ATC iliokuwepo,,kwanza ilikuwa ni kuunganisha na AJAS ambayo iliposhindikana ikauzwa kwa Shirika la ndege la afrika kusini hadi miaka michache iliopita ambayo haikuwa na manufaa kwa ATCL hadi ilipovunjwa

  Kwa maelezo mengine ATC na sasa ATCL imepita katika mabonde na vikwazo vingi kwa muda mrefu bila mafanikio,,imetengenezwa mikakati ambayo kwa hakika haijutii ni wapi walikosea.ndio maana kila hatua inayochukuliwa kwa nia ya kuikoa badala ya kuwa neema zaidi inakuwa ni balaa..zaidi ya awali

  Kwa wastani kwa muongo mmoja na nusu sasa tunaweza kusema bila hofu ATCL imeshindwa kubadilika na kuwa shirika la umma matokeo yake ni kuwapa shida wafanyakazi na viongozi wake katika kuliendesha..na kuwa fahari kama ilivyo mashirika mengine ya ndege

  Sisi hatuna kinyongo na ATCL ila tunaumia na kuumwa kuona uchungu wakati taifa hili likitumia mabilion ya hela kwenye pesa nyingi za uchaguzi zisizo na maana na watu wakichota kwenye mabenk ma billion na kuishia kuambiwa wakirudisha wanasamehewa…na kushindwa kuwa na shirika la ndege linaloweza kutimiza wajibu wa kusafirisha raia wake hata ndani ya mipaka yetu??achilia mbali safari za kimataifa..watanzania tumeamua kuamka na kuuliza tena na tena kwa nini tunakumbatia kitu ambacho kimeshindikana na kuishia kuwatesa waliomo huku viongozi husika wakiendelea kutafuna mabilion…iko wapi ripoti ya kawambwa ambayo wametumia zaidi ya mamilion ya pesa na kuishia kuhiifadhi, kabatini kwake!!ipo wapi ripoti ya hasara za hija zilizosababishwa na mtu mmoja tu ambae leo hii anadiriki kusema anaondoka na kumwachia ATCL yake atafute anaeweza kufikisha ATCL anapotaka,,haya yote uliyaataka mwenye Mh Waziri Kawambwa,,leo hii mtu huyu(MH Kawambwa) mnahisi anaitakia mema ATCL zaidi ya kuiua?? ..ni kwa nini basi tusianze upya kwa kuzingatia mazingira mapya kama NIC??na kujielekeza katika watendaji unaoweka malengo ili tuwe na shirika linalojiendesha kwa ufanisi na tija??

  Kwa maoni yetu msimamo wa serikali nasema ama kuhisi ni wa Waziri Kawambwa binafsi wa kutaka bado kuibadili ATCL hii kwa kutafuta wabia ni kuwaumiza wafanyakazi wa ATCL na kuwachosha viongozi wao…hakika tutapata matatizo tu.hatusemi haya kuichuria ATCL,ila tunasema kuwa njia pekee ingekuwa ni kukubali yote yaliotokea na kuivunja nakuanza upya kama ilivyofanyika NIC.na wafanyakazi wake kupata haki zao zote na pawepo na kampuni maalum itakayopewa jukumu la kutoa gharama za kila mtu ,na vyema wakafahamishwa mapema ili kila mtu ajue ameonewa ama la..

  Tuanze kuliunda upya kwa kuzingatia mambo mengi,

  1) KWANZA
  CHANGAMOTO ZA SASA NA MBINU ZA KUENDESHA MASHIRIKA YA NDEGE YA KIMATAIFA

  2)PILI
  KUWA NA DAMU MPYA YA WATENDAJI AMBAO WANATAMBUA MAANA YA UMUHIMU WA KUJIWEKEA MALENGO..WAJUE KWAMBA BILA KUZALISHA FAIDA YA KUJIENDESHA SHIRIKA HILO HALIWEZI KUWA NA NAFASI KATIKA SEKTA HIYO

  3)TATU
  UONGOZI UTAKAOPEWA MAMLAKA UNATAKIWA UPEWE MALENGO NA MUDA MAALUM WA KUWEZA KUTIMIZA YALE SERIKALI WANAYOITAJI BILA KUANGALIA WANATOKA NJE AMA LA..ILI MTU AJUE BAADA YA MUDA FULANI KAMA SIJATIMIZA HILI NA LILE KIBARUA KIKO MASHAKANI,UNDUGU,URAFIKI,MAHUSIANO YOYOTE YASIPEWE NAFASI KATIKA KUANZISHA UPYA NEW ATCL….

  4)NNE
  WAFANYAKAZI WATAKOKUWEPO WAPEWE MALENGO MAALUM NA MUDA MAALUM KUWEZA KUTIMIZA KILE AMBACHO KILA MTANZANIA ANATARAJIA KUKIONA …NA KILA MFANYAKAZI APEWE TIME LIMIT YA MALENGO YA KAMPUNI..
  5)TANO
  KUWEPO NA AUDITING YA MATUMIZI YA PESA ZINAZOTOLEWA AMA ZILIZOTOLEWA KILA BAADA YA MIEZI TATU HILI LITASAIDIA KUWEPO NA HESHIMA YA MATUMIZ I YA PESA KILA IDARA..HUKU KILA WAKUU WA IDARA WAKIELEZA PESA WALIZOPEWA WAMEZIFANYIA NINI NA WANAITAJI KIASI GANI ZAIDI KUWEZA KULIFIKISHA WATANZANIA WANAPOLITARAJIA???HILI LITASAIDIA KUONA HESHIMA YA ATCL IKIRUDI KWA KASI KULIKO MAELEZO

  Utaratibu wa kuendelea kuchota kodi za wananchi HAZINA na kutoa kwenye mashirika yasiojiendesha yenyewe ni utaratibu uliopitwa na wakati na hatuna budi kuulaani kama mtanzania unaetoa kodi,,..kama Vishirika vidogo vidogo vya ndege vikijiendesha kwa ufanisi mkubwa tena ndani ya Tanzania ni Balaa gani inaifanya ATCL nayo isifanye hivyo pia??.Tukatae kuendelea kuidekeza ama kuiua ATCL ,imeshindwa na sasa tuanze upya,Inawezekana
   
Loading...