Sasa ni rasmi Mechi ya Simba na Plateau haitoonyeshwa Runingani kwa Figisu za Wenyeji hivyo nawaomba Simba niwe Mkuu wa Kamati ya Kulipiza Kisasi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,569
108,911
CEO wa Simba SC Barbara (Babra) Gonzalez katika Kurasa zake za Mitandao amesema kuwa wamejitahidi vya kutosha tena kwa Kuhangaika huku na kule ile Mechi ya Simba SC na Plateau United unaochezwa leo Jumapili tarehe 29 Desemba 2020 uonyeshwe Mubashara na Azam TV lakini imeshindikana kwa Umafia na Figisu zinazofanywa na Wenyeji hao. Pia amewaomba Radhi wana Simba pamoja na Wanamichezo wote.

Sasa Mimi kama GENTAMYCINE wala sina Shaka na hili kwani kwa Mipira yetu ya Afrika nililitegemea lakini nina Ombi tu Kwenu Viongozi wa Simba SC na hata wana Simba wote popote pale mlipo kwakuwa Mechi yetu na marudiano nao ni Wiki (Weekend) ijayo naomba niteuliwe Mkuu wa Kamati ya UMAFIA,UKATILI NA ROHO MBAYA Maalum kwa Kuwanyoosha na Kuwalipizia Kisasi hawa Wanaijeria (Plateau United ) na nina uhakika wa 100% kwa nilichopanga Kuwafanyia wakienda Kwao watatukumbuka Milele.

Kama Mimi na Team yangu tuliweza Kumfanyia Umafia ( Unyangindo ) Mpuuzi Mmoja aliyekuwa ameshajiaminisha kuwa Dar es Salaam na Tanzania yote hii ni yake hadi kujiita Makamu wa Rais Kivuli na Kukosa Kura huko Baharini Dar es Salaam pamoja na kwamba alihonga sana, alitishia Watu na ana Network Kubwa hadi System ndiyo nitawashindwa hawa Matapeli FC Plateau United?

Na ole wake nione Mtu wa kutoka Serikali ( Wizarani ) au ndani ya Simba SC anasema tusiwalipizie Kisasi nitakufa na Wewe. Nimekereka nao sana.
 
Jiandaeni uwanjani mkacheze kwa juhudi , Ayo Mambo ya nje ya Uwanja hayata wasaidia,.Enzi za Enyimba mlikua mkifanya figusu na hawajawahi kuwafunga chini ya goli tatu apo apoTaifa.
 
Jiandaeni uwanjani mkacheze kwa juhudi , Ayo Mambo ya nje ya Uwanja hayata wasaidia,.Enzi za Enyimba mlikua mkifanya figusu na hawajawahi kuwafunga chini ya goli tatu apo apoTaifa.
Wewe hujui usemalo, unakohoa kama chura wa Kihansi. Enyimba anakufa Taifa goli la Joseph Kaniki na Boniphace Pawasa kwa kichwa enzi hizo ulikuwa bado uko Kasulu huko ndani ndani au hujui hata TV ulikuwa hujaanza kuangalia le Utopoloz.
Endeleeni kupanda daladala wenzenu wanapanda Boeing kwa akili za Kindezi namna hii.
 
Kwanini tunamalizia na neno la kwamba wamekataa kuonesha mechi sababu ya figisu badala ya kutueleza sababu zao za kukataa kuoneshwa mpira live ni zipi? Mazungumzo yalifanyika baina ya pande zote tatu (uongozi wa Simba, Plateau na Azam media) sasa kwanini sababu walizotoa plateau haziwekwi wazi ni zipi badala yake tunaaminishana ni figisu?
 
Kaka tumekupa kitengo hicho tusubiri maelekezo yako tu, pia napendekeza timu yao ishukie hapa bariadi, afu ndio mtawapeleka huko dar.
Mkuu kwa nilichokipanga kama Simba SC watanipa hili Jukumu huenda hawa Wanaijeria kabla na hata baada ya Mechi yetu Dar wakaomba Radhi.
 
Jiandaeni uwanjani mkacheze kwa juhudi , Ayo Mambo ya nje ya Uwanja hayata wasaidia,.Enzi za Enyimba mlikua mkifanya figusu na hawajawahi kuwafunga chini ya goli tatu apo apoTaifa.
Ulishasema Enzi kwani na leo pia ni Enzi?
 
Kwanini tunamalizia na neno la kwamba wamekataa kuonesha mechi sababu ya figisu badala ya kutueleza sababu zao za kukataa kuoneshwa mpira live ni zipi? Mazungumzo yalifanyika baina ya pande zote tatu (uongozi wa Simba, Plateau na Azam media) sasa kwanini sababu walizotoa plateau haziwekwi wazi ni zipi badala yake tunaaminishana ni figisu?
Itakuwa ni ishu ya maslahi lazima, huenda azam wametoa ofa kiduchu.

Mbona hata hapa hapa bongo yanga iliwahi kataa mechi zake za kimataifa zisionyeshwe
 
Wewe hujui usemalo, unakohoa kama chura wa Kihansi. Enyimba anakufa Taifa goli la Joseph Kaniki na Boniphace Pawasa kwa kichwa enzi hizo ulikuwa bado uko Kasulu huko ndani ndani au hujui hata TV ulikuwa hujaanza kuangalia le Utopoloz.
Endeleeni kupanda daladala wenzenu wanapanda Boeing kwa akili za Kindezi namna hii.
Screenshot_20201129-120826.jpg
Mimi wakati nacheza Soka uyo pawasa alikua bado pale kwa kipingu anasoma.
 
Mkuu kumbe ulishiriki zoezi la kumzamisha kijana wetu..

Basi hili la platyuu tumekukabidhi rasmi..

Tuwapeleke camp huko sanga sanga ngerengere..

Wakianza kuja taifa wapitie rufiji dam,kibiti, wapumzike mkuranga,tuwapishe hadi bunju kisha waje urafiki pale wafanye zoezi..
 
Tutaweza kuwazungusha hivyo endapo watakuwa wajinga na wapumbavu. ila kama sio hivyo basi hatutafanikiwa kuwazungusha sababu ukiingia kwenye Google map inaonesha routes za karibu kutoka pale ulipokuwepo.
 
Basi acha kuleta Uongo uongo. Waulize Enyimba wenyewe watakwambia, Simba aliwapiga 2 wakafuta mechi dkk ya 75 kisa maji uwanjani. Waulize akina Emmanuel Gabriel na Pawasa watakueleza ule mtafaruku
Inaonekana hujui unacho andika au umesimuliwa, Mechi iliyo lala kwasababu ya mvua ilikua Simba na Ismailia fixture ya pili, Fixture ya kwanza Simba walifungwa 2-0 kule Egypt. Mechi ya Taifa shamba la bibi ilivunjika baada ya mvua kunyesha mbaka mpira kuna baadhi ya maeneo uwanjani ilikua Uki elea juu ya Maji au kunasa. Mpango wa Ismail adeni Lage kuleta magodoro yatandikwe uwanjani kunyonya Maji ili mechi iendelee uli kwama, Mbaka mpira unasimamishwa Simba walikua wakiongoza 2-0. Mechi ikavunjwa ikaja kurudiwa siku ya pili na Simba ilishinda 1-0 na kufungasha virago.
 
Back
Top Bottom