Sasa ni Dhahiri Watanzania tuna Undergo evolutionary Regression! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa ni Dhahiri Watanzania tuna Undergo evolutionary Regression!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chibenambebe, Jul 19, 2012.

 1. C

  Chibenambebe Senior Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wakuu mkichunguza kwa makini mtabaini kwamba Zamani babu zetu walikuwa na utaratibu mzuri sana wa jinsi ya kuwapata viongozi wao.
  Zamani mtuu uongozi alikuwa anapewa kutokana na sifa za mtu kama ushujaa wa mtuu, uvumbuzi au ugunduzi wa mambo, au kuwa kiungo muhimu cha kibiashara baina ya jamii moja na nyingine na kwa kuamini kuwa mambo hayo (Vipaji) huwa yanarithishwa kutoka kizazi kimoja mpaka kingine wakawa na imani na kuweza kurithisha madaraka kizazi kimoja hadi kingine. Na wale waliorithishwa walikuwa wakiwekwa chini ya baraza maalum chini ya uangalizi ilikuweza kuwajenga kimaadili na hatimae kukomaa, kuwa timamu kuweza kuongoza vizuri jamii husika.
  Leo mtu unaweza lala halafu ukiota au ukidanganya umeoteshwa kuwa rais na unapesa za kutosha kweli unaweza kuwa raisi. Siku hizi tulo tofauti na vigezo walivyokuwa wakitumia wazee wetu eti tunaangalia sura, pesa tena ya kuhongwa isiyokidhi hata mahitaji ya siku moja Halafu mtu unampigania hadi kufikia stage ya kumfia Sasa wanajamvi niambieni leo hii Kikwete alilifanyia nini taifa hili mpaka mkaamua kumpigia kura na kumchagua kuwa raisi?
  Zamani babu zetu walikuwa wanabadilisha madini kwa vitu kama shanga, vioo na vinginevyo wakaendelea wakaona wananyonywa wakasitisha hiyo biashara wakasema hata kuchimba basi hawaruhusu mgeni yeyote kuyachimba haya madini wakaamua kutokuwa wabinafsi na kuviachai vizazi vijavyo.
  Majuzi akaja Mbuzi ambaye kwa kweli ubongo wake ume undergo regression ya hatari akawahadaa wenye ubongo kama wake na kuwambia kuwa eti wachague kati ya Kupata 0/100 au 3/100 Kwa mwenye chake na mtu ambaye siyo chake apate 97/100. Hii hata mtoto mdogo ukienda kwao ukakuta kuna pipi ziko kabatini ambako hawezi kuzifikia ukamwambia uzitoe halafu yeye umpe 3 na wewe uchue 97 lazima dogo agomee na akatae. Sasa huyu mbuzi na wenzake kweli walitumia akili.
  Zamani ukweli ndio kigezo cha kumheshimu mtuu na hutawahi kusikia eti baba anadanganya au anadanganya na uongo wake unafichuka ilikuwa ni vigumu sana. Kutokana na hayo waliweza kuheshimiana kuanzia rika la chini mpaka la juu.
  Leo hii mtu mzima anadanganya tena umma na still watu mzidi si kumheshimu tuu bali hadi kumwabudu Oh Mheshimiwa! mheshimiwa! Mimi nakataa!!!! Kizazi hiki tutakuwa na matatizo.Kwa haya yote mimi nasema sasa ni dhahiri Ubongo wetu hasa watanzania una undergo regression na bado nafanya utafiti nikikamilisha nitawaambia sababu!
   
 2. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Msugu mlonjele mahala go muyagwe!
   
Loading...