Sasa nec inataka kufuata mtindo wa kivuitu


I

Inkoskazi

Member
Joined
Apr 12, 2010
Messages
29
Likes
4
Points
15
I

Inkoskazi

Member
Joined Apr 12, 2010
29 4 15
Sitayatambua matokeo ya urais - Dk. Slaa Send to a friend Wednesday, 03 November 2010 05:18 digg


_dk%20wilbord%20slaa.jpg
Dk Willbrod Slaa

MGOMBEA urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema), Dk Willibrod Slaa amesema, atayakataa matokeo ya urais yatakayotangazwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa kuwa kumefanyika wizi mkubwa wa kura.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Dk Slaa alisema, kama NEC inaitakia mema nchi hii, ifute matokeo yote ya urais na uchaguzi urudiwe upya.

Dk Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, alisema wamekuwa wakifuatilia matokeo ya nchi nzima kwa umakini mkubwa na wamegundua kuna wizi mkubwa wa kura kwenye nafasi za urais na ubunge.

"Kuna uchakachuaji mkubwa wa kura na kazi hiyo inafanywa na usalama wa taifa,"alisema Dk Slaa.
===============================

"Moringe wote ni wamasai lakini sio kila mmasai ni Moringe"
 

Forum statistics

Threads 1,237,332
Members 475,533
Posts 29,284,739