Mkuu hii tabia viongozi wengi wanayo na kama ni hivyo ni uzembe wa hali ya juu. Ninachofahamu ni kuwa Seriklai inafanya kazi kwa maadishi sio maelekezo ya mdomo, hata ukipewa maelekezo ya mdomo, unatakiwa uyaweke katika maandishi ili yaweze kutekelezeka na kuweka kumbukumbu. Kama alipokea tu kwa mdomo, basi ni kosa tena kubwa sana. Hata hvyo, kwa hadhi ya PM hawezi kuwa aliishia hapo, ni lazima baada ya hapo angempigia Rais au aende waongee kwa urefu kuhusu suala alilooona kuwa lilikuwa na utata. Ambacho mimi na wewe hatufahamu nikama alifanya yote hayo, na kama alifanya nini kilikuwa maelekezo ya Rais kwake, na ukumbuke kwa kuwa hawa watu ni marafiki na walishawahi sema kuwa hawakuktana njiani, huenda kuna maelekzo yalitolewa ambayo baadaye yalikuja kumgharimu mwingine kwa hiyo ndo maana ana hasira na kuamua kusema vile, aidha, anaweza kuwa ana mengine makubwa zaidi ambayo kwa hadhi yake asngeweza kuyasema katika hadhira ya aina ile ya siku alipokuwa anapokelewa CDM. Sasa ni wajubu wa upande wa "mamlaka ya juu" kukanusha kama kweli ni uwongo maana watu kwa sasa wanaamini vingine kuhusu Richmond na hii ndo agenda kubwa iliyotumika kumsafisha mtu.Kauli ya maelekezo kutoka ngazi ya juu ni ya kitoto sana kwani alidai kuwa eti kuna mtu alitoka nje akaongea na simu karibu saa nzima kisha akarudi na kutoa kauli kuwa ngazi za juu wanasema mchakato uenedelee.Huu ni utapeli wa kisiasa kwani yeye kama mtendaji mkuu wa serikali iweje atuambie kuwa kuna ngazi za juu tena kwa njia ya simu? Ivi inaingia akili kuwa PM hawezi kuongea na raisi wake mpaka mtu wa kati ndio ALETE taarifa tena ya mdomo kwa maswala muhimu yanayohusu hatima ya nchi. umakini wake unapatikana wapi ikiwa alishiriki kupitisha jambo asililiamini tena kwa maelezo ya mtu aliedai alipigiwa simu toka ngazi za juu? Kwanini leo? kama yeye ni mtu safi kwanini muda wote huu amekaa kimya mpaka alivokatwa jina na kuhamia ukawa ndio aanze kusema haya? kama asingekatwa inamaana angbaki kimya uku akijua kuwa alishiriki katika kuhujumu nchi? wapi uadilifu wake katika hili?