CDM msihofu waachenihao CUF, TLP, NCCR waje kwenye hiyo kambi bali mkikutana kwenye kikao mawaziri wote KIVULI watatoka CHADEMA wakienda kulalamika jibu ni kuwa mlipiga kura na SIMPLE MAJORITY WALICHAGUA MAWAZIRI KIVULI!!
Mimi naona ni sahihi kwa maamuzi waliofanya CDM. CUF ni sawa na ndumila kuwili tu hawezi kuwa rafiki wa CDM vilevile CCM si atakuwa anachukua habri huku na kupeleka huku.
Ni point nzuri sana comrade,na kama simu yangu ingeweza ku'bold' ningeisisitiza hivyo.
CUF(bara),NCCR,TLP,UDP wanapaswa haswa watafute uhalali wa kuheshimiwa na wananchi kwa kutetea mustakabali sahihi wa taifa na kupigania haki za wananchi. Wanachojaribu kukifanya sasa, kukipiga vita CHADEMA na kujaribu kutumia mapenzi yao ya sasa na CCM ili kupora 'benefits' walizopata CHADEMA baada ya kupata ridhaa ya wananchi, haiwajengi, haiwaletei heshima.
Wanapaswa wajipange upya kimkakati na kiitikadi, wapiganie maslahi ya jamii pana zaidi ya Tanzania, waone kama watahitaji kupigania umaarufu kama wanavyofanya sasa akina Kafulila na Ahmad Rashid.