Sasa masomo ya sayansi lazima sekondari, utaratibu wa kuchagua masomo kidato cha tatu haupo tena

Kuna kitu cha msingi ya kwamba MOLA wetu katika uumbaji wake ametutunuku na biological diversity pamoja na social diversity. Hatuwezi wote tukafanana kwa uwezo wetu au mapenzi yetu kwenye haya masomo. Tuliosoma enzi hizo secondary tulikuwa na stream mbili tu (sayansi na arts) kijana anapoingia form 3. Hapa katikati wakaongeza ya biashara-kama kuna nyingine nifahamisheni.
Uhuru wa kuchagua ni haki ya kila mmoja wetu-ingawa kuna masomo kama taifa tunaweza kukubaliana kwamba ni vizuri kila kijana awe ameyasoma (e.g. hisabati, one international language na civics) baada ya hapo tutoe uchaguzi (kiuwezo na mapenzi) kama science, arts na commercial subjects. Tufundishe kwa viwango vya juu darasa la 1 hadi form 2 ili watoto wakifika hapo wanauwezo mzuri wa kuchagua au kuelekezwa na walimu tusiwalazimishe. Lakini serikali pia iweke mfumo mzuri na wenye uwiano ndani ya shule, mikondo hii iwepo na pia kuwe na career masters (shule nyingi hazina wala hazijawa na hii kitu). Facilities nazuri za masomo ya science (infrastructure na walimu) lazima ziwepo. Tukifanya hivi nina hakika vijana wengi wataipenda science na sio kulazimishana.
Namba ya masomo pia ni kitu muhimu. Ubongo wa binadamu una limited capability. Nikirudi enzi hizo tena wengi tulisoma masomo 8 na sio chini ya 6. Sasa yanatakiwa yasipungue 7 lakini yanafika 10. Ukilazimisha wote wachukue sayansi yatakuwa mangapi hasa kama kijana haoni kwamba anataka achukue sayansi. Shule zinazojengwa kwa msingi wa dini nao watataka vijana wasome somo la dini.
Mwisho tunaambiwa na wachumi kuwa kuna comparative advantage, na tija yetu kama taifa inakuwa kubwa kuzalisha kile ambacho umejaliwa nacho ulinganishwapo na wengine.
Kwa misingi hiyo ningependa kujua waziri ana mkakati gani wa kutekeleza adhma yake au ya serikali yake-lakini kimsingi simuungi mkono kitu anachotaka kukifanya hata kama nakubaliana nae kuwa tuna upungufu wa wanaochukua masomo ya science.
 
Hawa wasomi wetu ni shida kweli.

Viwanda na masomo ya sayansi wapi na wapi.

By 2020 hii serikari itakuwa imekasirisha kila raia vijana kwa wazee, vijijini na mijini. wasipojipanga hizo kura sijui watazitoa wapi it is if awatorudi kuomba kura.
 
Nchi hii!!! Unadhani kumforce mwanafunzi kusoma sayansi ndiyo kupata wataalamu ? Mwisho wa siku biology F, chemistry F, physics F, but History A, Commerce A, Bookiping A, Kiswahili A, n.k.umefanya nini sasa.
 
Masomo yanayotakiwa kufahamika na kila mtoto anayehitimu kidato cha 4 ni haya:
1.Kiingereza 2. Kiswahili 3. Geography
4. History 5. Mathematics 6.Information Science. 7. Chemistry 8. Physics 9. Biology

Plus one of the following options: 1. Additional Maths. 2. Religious Studies
3. French 4. Music 5 . Fine Art

Yaani kila mtoto anachukua masomo 10 kamili.
Civics??????????????????
 
Kwa hili ninakuunga mikono yoote professor ndalichako Congratulations kwa jambo hili. nakuunga mkono na faida zake na mifano yake ni kama ifuatavyo 1. Kila mtanzania atakuwa anawaza kujiajiri pindi ana knowladge ya sayansi 2. Masomo yanayotengeneza ajira za viwandani ni masomo ya sayansi kama pcb,pcm,pgm,EGM,ECA,CBG,nk Mtu akiwa na uwelewa wa masomo haya siku akimaliza kidato cha nne atakwenda Veta na kujua ufundi ambapo atakuwa na uwezo wa kuajiriwa kwenye sector ya viwanda kwa kuwa viwanda vingi watendaji wengi huwa daraja la chini na degree ni wasimamizi tu mfano mimi nina mpango wa kuanzisha kiwanda Cha ngozi pale shinyanga ninategemea kuajiri vijana 1000 na nitaajiri kwa asilimia kubwa vijana waliohitimu Form four na kwenda Veta waliosoma sayansi. 3.China wameendelea na wafanyakazi wengi viwandani wana Elimu ya college na kwa kuwa wana mfumo wa kusoma masomo yote ya hati na sayansi ni rahisi kuajirika kwa kuwa wana knowldge Kwa kuanzisha hili nakupongeza prof ndalichako. 4. A lieharibu elimu ya sayansi kuanzia shule ya msingi ni Mheshimiwa Mungai wazili aliefuta sayansi shule za msingi lakini lengo lake tunalijua hakuwa mtanzania na alitumwa na Kenya kuiua Elimu ya Tanzania ili kesho iendelee kwenye soko husika. 6.Kuhusu maabara hakuna shida kwa anaelalamika kwa kuws serikali ilishajenga maabara zote shule za sekondary. 7. waalimu wataajiriwa,tu no wasiwasi wa mleta habari kwani wale wanafunzi waliorudishwa UDOM wamepangiwa kusoma vyuo vya diploma ili wasidie kufundisha secondary. 8. ongezea na somo la kichina liwe compulsory kwa sababu wakenya kwa sasa wanakimbilia hilo soko na hatimae watakuja kuchukua hilo soko,sasa basi jitahidi kila mwaka peleka waalimu 100kila mwaka kusoma kichina kwa scholarship za wachina ambpo itasaidia kuboresha somo hilo. 9. Elimu ya form four kusoma science haimzuii mtoto wa mtu kusoma sheria,Kwa kuwa specialization inaanzia form six sio form four. 10. Kila mtoto mwambie faida ya kupenda masomo ya science, mfano hivi karibuni nilimhamasisha mtoto wa form four kusoma somo la kichina ambapo nilimwambia akijua kichina akimaliza shule form four ni rahisi kupata kazi ya translation ya kichina kwa kuwa jamii hiyo inaongezeka kuja Africa, Jana nimekutana nae anajua kuandika jina lake kwa kichina kafurahi na anajituma .Hongera saana mheshimiwa,usiogope maneno ya JF wewe chapa kazi hawa wengine hawataki kusikia maendeleo wamezoea varangati za maandamano.Ila mheshimiwa waambie wanafunzi kuwa ili fanikiwe awe na maendeleo SIASA za fujo hazitamsaidia,atakuwa maskini kwa kumjengea mtu umaarufu.
Una akili nyingi sana
 
ni kuwaongezea mzigo walimu tu kuwafundisha watua ambao hawaelewi au hawako tayari sawa na kumfundisha mbwa mzee kuwinda. kule sekondari kuna watoto wanawaowasomea wazee wao na walimu na si wao wenyewe ndo maana kuna utoro na uhuni mwingi walimu wanapata shida sana
suluhisho la sayansi ni vyuo vya ufundi waende huko wakue na kukomaa zaidi kwa vitendo tuache kuwajaza watt matheories huko mashuleni ambayo hawayaelewi
Wewe kweli mzalendo!!! Ubongo wako ni mgodi wa almasi
 
Juzi walituletea BRN leo wanaleta madudu mengine, mambo ya POLICY sio jambo la prof kijifungia na watu wake watano na kuamua mustakbali wa wananchi na maisha yao. Haya mtoto anafanya physics na hajawahi kuisoma tangia akiwa form one, hicho kiwanda chako kitasaidia nin?? kwani hivyo viwanda vimejengwa wapi ili tuambiwe kuwa havina wataalamu?? sasa huyu akusimamie Phd yako si utatamani dunia ipasuke uzame???

Kitu serikali isichokielewa nikwamba matatizo makubwa ya elimu yetu yapo ELIMU YA MSINGI, huku ndiko ambako mtoto atatoka na mwelekeo wa VIWANDA au VINYOZI, sio sekondari. Kwa mafano mwana funzi amemaliza darasa hajui hata longitude na latitude ni kitu gani, hiyo sayansi anayosoma shule ya msingi ipo kwa KISWAHILI akifika sekondari anakutana na ENGLISH, watoto wanataabika na kukariri tu hawajui kinachoondelea.

Ni jambo lakushangaza sana, mara nyingi tumesikia wanafunzi wanajiunga sekondari hawajui kusoma wakla kuandika, huyu anaweza kutafuta MOLARITY na MOLAR MASS?? kama hata jina lake mwenyewe hawezi kuliandika?? Huu uprofesa mnaenda kusomea jinsi yakugawa mali mnapotalikiwa na waume zenu au kitu gani??

Kuna shule nyingi sana hazina walimu wa sayansi hasa PHYSICS NA MATHS, wakati huohuo mwanafunzi ametoka shule ya msingi hajui kusoma wala kuandika, jamani hivi viwanda havianzii sekondari, viwanda vinaanzia kwenye shina la elimu yetu. Pia kuna shida ya watoto wengi kutotaka kusoma sio hayo ya sayansi tu bali hawataki kusoma hata hayo ya sanaa tofauti na zamani, serikali itafute suluhisho lakudumu na hakuna haja yakufanya haraka manake hata nishati ya uhakika hatuna, viwanda hivi vitatumia USHUZI?? swala lakuhamia dodoma hamjamaliza leo mnakuja na mengine. Mfumo wa elimu haubadilishwi kama mtu anavyobadilisha nguo ya ndani au soksi zake akavaa nyingine within 20 seconds, ni mchakato tegemezi na shirikishi wa sekta nyingi na kuwaandaa beneficiaries kwa kila eneo.

Je viwanda hivi havitahitaji WAHASIBU, watu wa ENVIRONMENTAL IMPACT ASSESSMENT??, watu wa PROCUREMENT?? Sasa huyu mwnafunzi atasoma masomo mangapi?? si yatafika 20?? au sisi tunajua viwanda vinahitaji Cemistry na Physics na Maths tu?? Kuna watu wa LABOUR RELATION?? COMMUNITY DEVELOPMENT, SPATIAL ORGANIZATION?? hawa wote watasoma masomo ya sayansi???
Ndiyo maana kipaumbele cha UKAWA kilikuwa elimu elimu elimu
 
Profesa ndalichako kwa hapo umekurupuka hao wanafunzi watafundishwa na madawati?lazima wakati unataka kufanya jambo ufanye tadhimini kwanza,unajua kabisa kuna uhaba wa walimu wa sayansi alafu unakurupuka tuu.why why
 
niwaambieni kitu
sector ya viwanda ina ndugu zake wakaribu ili viwanda vikamilike ambao ni
{1}miundombinu na usafirishaj
{2}elimu
{3}nishat
{4}kilimo
{5}masoko
hawa ni watu muhimu mno ktk, ukamilifu wa viwanda na uchumi wa kat
hivyo kuwekeza ktk sector moja pekee mfano kilimo kima cha chini ni zaid ya miaka10,
kumbuka kilimo hcho pia kinahitaj
-elimu
-miundombinu
-masoko
-viwanda
-nishat
je, umeona wanavyo tegemeana?
na je, ikiwa sector moja tu kufanikiwa huchukua zaid ya miaka10 vip sector 5 hizo zitachukua miaka mingap?
nchi kama japan,china, na marekan hazikuchua muda mfup ktk kuwekeza
na uwekezaji ktk kila sector upo systematic
kwana utaanza elimu na utapata experties ktk kada mbali mbali kwa ajil ya kutumikia hizo sector zilizobaki
mfano china walianza na elimu tena kwa mda mrefu sana kwa kuwapeleka marekan raia zao
vp tanzania inataka kuwekeza sector zote kwa mda mmoja tena kwa kipindi kifup?
hii huchangia kod pia zisizo na mpango kuongeza
hpo nisawa na mtu kapanda farasi wawili
 
Uwezi mlazimisha mtu kusoma sayansi wakati hakuna vyuo vingi vya udaktari,engineer waongeze na kuboresha vyuo vitoe kozi za sayansi kama udaktari na kuongeza mikopo
Uyo mama anatoa vitu from no where wange kua wa naitaji watu wa science wangefungia vyuo vya udactari na waliofaulu waka some wap
waandae mazingira mazuri tu watu watapenda sayansi automatikale sio shule nzima walimu wawili huku maabara zikichechemea kwa ukosefu wa vifaa mwalimu mwenyewe mshahara wake hata haumshawishi kufanya extra activities hapo tutakuw tunatwanga tikitimaji hali tukitegemea tupate walau pumba za kulisha kuku
 
Uwezi mlazimisha mtu kusoma sayansi wakati hakuna vyuo vingi vya udaktari,engineer waongeze na kuboresha vyuo vitoe kozi za sayansi kama udaktari na kuongeza mikopo
Mkuu umeenda mbali sana,leo hii kununua kemikali kwa ajili ya mafunzo ni mtihani achilia mbali kuwa na maabara zenye vifaa vya kujifunzia,jamani tunaweza kuwa na mawazo mazuri sana lakini tunataka kuwa na kenda wakati moja hatuna,tuanze kujenga maabara,tuweke vifaa,tuhakikishe waalimu wajuzi wa hiyo sayansi wapo na ndipo tuje na matamko,nachelea kusema hivi,,,wale wenye daraja la nne na sifuri watakua wengi mara dufu,asante.
 
Tanzania kuendelea bado sana aisee.. Hata tukiwa nchi masikini ni sawa
Hivi haya maamuzi ya kulazimisha yana faida kweli.? Mi nafikiri sera iliyopo iendelee.. Mtu atasoma hayo masomo kwa kishingo upande kwa kuwa amelazimishwa na hakuwa na msingi mzuri tangu elimu ya msingi sembuse sekondari??

Aibu aisee hata kama ni Tanzania ya viwanda sio kwa mtindo huu ambao mazingira ya shule mabovu, walimu hawapati stahiki zao, vifaa vya ufundishaji ni duni... Maabara hazitoshelezi... Elimu yetu yenyew ya kukariri ufaulu mtihani tu..... Tutegemee anguko kubwa la elimu kwa shule za serikali, la sivyo tutakuwa tukikimbizwa na shule binafsi ambazo ukimpeleka mwanafunzi huko anashawishika kusoma hayo masomo ukilinganisha na shule zetu hizi za kata....

WAZO NI ZURI SAWA.. ILA JE, TUMEJIANDAA AU NDIO TAMKO LIMETOKA LIFUATWE, HAKUNA MJADALA???
 
Civics??????????????????

I suppose CIVICS and similar derivatives of core subjects could be added into the list of optional subjects. But I must add that we should stress core subjects and leave the rest to specialized studies at higher levels of the education ladder. Civics, when devoid of indoctrination, can be taught within Political Science.
 
Back
Top Bottom