Sasa masomo ya sayansi lazima sekondari, utaratibu wa kuchagua masomo kidato cha tatu haupo tena

Ukaridayo

JF-Expert Member
Oct 8, 2012
507
469
Mama Ndalichako asema nchi ya viwanda haiepukiki hivyo ule utaratibu wa wanafunzi kuchagua masomo wanapofika kidato cha III haupo tena!!!

Masomo ya sayansi ni ya lazima ili kufikia lengo.

Mjuze mwanao, dada yako, Kaka yako, binamu yako, Baba yako mdogo, Mama yako mdogo kama ndiyo wanaingia FIII ni lazima wayamudu masomo hayo.

---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
SERIKALI imetangaza mwongozo mpya kuwa kuanzia sasa masomo ya sayansi ni lazima kusomwa na wanafunzi wote wanaosoma elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. Kwa mujibu wa Sera ya Elimu iliyopo, wanafunzi wanaosoma elimu ya sekondari wanaweza kuchagua aina ya masomo watakayo wafikapo kidato cha tatu na kuacha mengine.

Uamuzi huo ulitangazwa jana mjini hapa na Waziri wa Elimu, Teknolojia, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza na mamia ya walimu wa elimu ya msingi kwenye mafunzo ya muda mfupi kuhusu mtaala mpya wa kufundishia wanafunzi wa darasa la tatu na nne.

Alisema hivi sasa nchi imedhamiria kuingia kwenye uchumi wa kati ambao ni wa viwanda, hivyo suala la sayansi haliwezi kuepukwa kwa sababu ni wakati sasa wa kuwa na wataalamu wengi wa fani za sayansi watakaoweza kutosheleza mahitaji ya sekta ya viwanda nchini.

Alisema kutokana na uhaba wa wataalamu wa sayansi nchini kwenye maeneo mengi, wizara imeamua kuanzia sasa wanafunzi wote wa elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, watalazimika kusoma masomo ya sayansi na kufanya mtihani wa masomo hayo, na kwamba baada ya matokeo kutoka ndipo watafanya uamuzi ama wa kuendelea nayo au la.

Hatua hii kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, itamlazimisha mwanafunzi kusoma kwa bidii ili kuhakikisha anafaulu masomo hayo ingawa hivi sasa wanafunzi walio wengi wanadai masomo hayo ni magumu, ndiyo maana wanachagua kusoma masomo ya sanaa.

Alisema ili kuhakikisha azma ya serikali ya wanafunzi wanapata vitendea kazi vya masomo hayo, Sh bilioni 12 zimetengwa kwenye bajeti ya fedha ya mwaka huu kwa ajili ya kununulia vifaa vya maabara kwenye shule zote za sekondari nchini ili kuwepo na zana za kufundishia kwa ajili ya masomo ya sayansi.

"Mafunzo ya vitendo sasa sio mbadala ni lazima, na yatafanywa kama sehemu ya masomo na wanafunzi wote watalazimika kuyafanya kwa vitendo ili wawe na uelewa wa walichosoma kwa manufaa ya taifa,” alisema Profesa Ndalichako.

Alisema Serikali ya Awamu ya tano imedhamiria kuona kiwango cha elimu kinachotolewa nchini kina hadhi sawa na elimu itolewayo na mataifa mengine ili kupata wataalamu wenye sifa zinazokidhi mahitaji ya soko hata kama sio wote wataajiriwa ila hata wale wasiopata ajira wajiajiri kupitia elimu waliyopata.

Aliwataka walimu waliohudhuria mafunzo hayo kuhakikisha wanatumia uwezo wao na elimu waliyopata kufanya kazi kwa mujibu wa maadili ya taaluma ya ualimu ili kuwajengea msingi mzuri wa elimu wanafunzi wa shule za msingi.

Akizungumzia kauli ya Profesa Ndalichako, Mwenyekiti wa Wamiliki wa Shule Binafsi Tanzania (TAMANGOSCO), Mahmoud Mringo alisema ni uamuzi mzuri ila umekuja kwa kuchelewa kwa sababu mahitaji ya wataalamu wa sayansi nchini ni makubwa kuliko idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo hayo.

Alisema pamoja na uamuzi huo mzuri uliochukuliwa na serikali, lakini bado kutakuwa na changamoto ya uhaba wa walimu wa masomo hayo, maabara na maktaba na kwamba hali hiyo inaweza kusababisha mahitaji ya walimu hao kutoka nje yakaongezeka.

Katibu wa Tamangosco, Benjamin Mkonya alisema ni hatua nzuri ingawa utekelezaji wake utakuwa na changamoto nyingi kwa sababu hali halisi ya mazingira ilivyo nchini.

Alisema ikiwa serikali inadhamiria kutekeleza azma hiyo ni vyema kipengele cha vigezo vya shule kuwepo ambavyo vimeainishwa ndani ya sheria ya elimu nchini, vikaangaliwa ambavyo ni uwepo wa maabara ya kutosha, maktaba yenye vifaa na walimu wa kutosha.

Alisema iwapo vigezo hivyo vikiangaliwa shule ambazo hazijakidhi vigezo hivyo zikafutwa na vifaa vilivyopo kwenye maabara na maktaba hizo zikaongezwa kwenye shule zenye vifaa hivyo ili kusaidia utekelezaji wa azma hiyo ya kufundisha masomo ya sayansi kwa wanafunzi wote kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Walimu washiriki wameishukuru serikali kwa mafunzo hayo ambayo walisema ni mazuri na yameongeza kiwango chao cha uelewa na kuwaongezea mbinu za ufundishaji sambamba na kukuza morali ya kazi zao.

Pamoja na kushukuru, wameomba wizara hiyo iangalie jinsi ya kuweka posho kwa baadhi ya maeneo ya kazi, hususan kwenye vituo vya kazi vilivyopo pembezoni na kwenye mazingira magumu ili kuwajengea walimu motisha wa kufundisha maeneo hayo.

Walimu waliohudhuria mafunzo hayo ni 480 wanaotoka halmashauri za Bumbuli, Mji wa Handeni na Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.


Chanzo: Habari leo.
 
waandae mazingira mazuri tu watu watapenda sayansi automatikale sio shule nzima walimu wawili huku maabara zikichechemea kwa ukosefu wa vifaa mwalimu mwenyewe mshahara wake hata haumshawishi kufanya extra activities hapo tutakuw tunatwanga tikitimaji hali tukitegemea tupate walau pumba za kulisha kuku
 
Mie nadhani wangewekeza kwy vyuo vya ufundi zaidi(VETA,DIT,AR NA MBEYA TECH) na kuwapa fursa wanafunzi wengi kujiunga navyo,vifaa bora vya kisasa,kupanua wigo wa ufundi etc ila kwa kulazimisha eti secondary science lazima ni kukurupuka tu uko!sioni uhusiano wa science ya secondary na viwanda moja kwa moja!
 
Ina maana Mama Ndalichako anaamini kila form IV aliyehitimu akiwa anasoma pamoja na masomo ya sayansi ndo tayari nae ni mwanasayansi? Sawa, watu watalazimishwa kusoma sayansi kama wanavyolazimishwa kusoma maths lakini kwenye paper ya form iv; wanazungusha... then what?! Ndo umeshatengeneza hapo?
 
[QUOTE="_Iramba, post: 17116565, member: 359488"! i jambo jema,ila serikali haioni kuwa itapelekea kuua mizizi ya fani zingine kama sheria?[/QUOTE]
=====
Utakuwa mwanasheria lakini una basics za sayansi !
 
Naanza kuona kifo cha Facebook, tweets, instagram na kuchora vikatuni kwenye makaratasi ya majibu kimefika, Mungu Ibariki Tanzania
Yeeees. Nitakuwa wa kwanza kufurahi kuona hili likitimia
 
Hii ninaisuport serkal kwa mikono yote na miguuu. Hii ni kama uganda vile.

Na hya masomo yanabid yawe categorised katka group la Lugha, Math, Science, Bihshara na Art. Katika cuconsider GPA mwanafunz anabid awe amefaulu angalau somo moja kutoka kila category.
 
Huyu Mama nayeye anafikili wote wanafunzi ni watoto wake,dunia ya wapi hiyo JAPAN kwenye kwenye viwanda na sayansi iliyokomaa kitu kama hicho hakipo,hata hivyo ni kwa nini suala hilo lisipelekwe kwa wadau wajadili kwanza?
 
Back
Top Bottom