beparimkuu
Member
- Feb 25, 2014
- 17
- 0
Kutokuwako madawati sio kigezo cha kuwafanya wasivae yunifomu hujapitia darasa nini? Komaa watoto waende shule na sare sio unalewa tuuu halafu ukishindwa unalalama
Mkuu Kijakazi II,
Wengi wetu tupo hapa leo sio kwamba familia zetu zilikuwa na pesa nyingi za kutupa mahitaji Muhimu.
Isipokuwa wazee wetu walijitahidi kwa kadri ya uwezo wao kutupa kile walichopata ..wakawekeza kwene maisha yetu na huo ulikuwa mchango mkubwa sana. Mimi nafikiri sio sawa kusema watoto wasiende na uniform shuleni kisa mzazi hana pesa za kumnunulia. Nina uhakika wazazi Wengi wangekuwa na nidhamu ya maisha wasingeweza kukosa uniform. .kama ukisema mtoto hawezi kununua uniform..atawezaje kununua nguo za kushindia? Hivo kuna kipindi tutasema watoto waende uchi shule maana wazazi hawana pesa ya kununua nguo
hao ambao hawana masaada wa wazazi wapelekwe huko kulelewa na yatima hata serikali ikishindwa kuwasaidia sisi tutawasaidia kama yatima.wananchi watajitolea. lakini sio mtu ana wazazi wote ardhi kubwa,mifugo inafugika najua hawezi kuwa tajiri wala kujenga hela ya uniform kwa mwaka mzima ambayo pengne ni elfu 5?hili nakataa
Muwasilisha mada, wazazi wanakosa fedha za kununulia nguo ama sare?, iweje wapate za kununulia nguo za nyumbani wakose za kununulia sare? jaribu kutengeza hoja kamilifu idiyo kuwa na ombwe ndani yake. umesema
Sare za shule ni muhimu katika kujenga taifa moja na imara. Ikiruhusiwa kila mtoto aende shule na atakacho, basi kutakuwepo na watakaokwenda uchi kwani kuna wazazi ambao kwa ujumla hawataki kuwajibika kwa watoto wao na wale watakaokuwa wanabadilisha viwalo kila siku. Wanafunzi wengine, hata wale ambao wasingejengewa inferiority complex, huanza kukua nayo pole pole. Mwishoe ni psychological tourture na mtengano wa kitaifa kuanzia ngazi ya chini kabisa. Walioweka sare walikuwa na maana yake na mimi mwenyewe kwa kusoma shule ya sekondari ya aina hiyo miaka ya 80 najua madhara yake fika.
Kwa hiyo kwa maoni yako ni kwamba ni Bora Mtoto akae nyumbani mpake apate Sare ndiyo aende Shule?
Watanzania wengi wanapenda kufanyiwa kila kitu, hawataki kufanya kazi kujiletea maendeleo, in short wengi ni wavivu wakitegemea serikali iwafanyie ila kitu.Mzazi huwezi zaa mtoto halafu hata shati na kaptula ya shule ushindwe kumnunulia, ukisubiri serikali ipitishwe sharia ya kuondoa uniform. Ni kiongozi mwenye maono mafupi ndio anaweza kuja na sheria ya kipuuzi kama hivyo. Maeneo mengine nchi hii, kwa kuwa ni lazima mzazi amnunuie mtoto nguo ndizo hizo hizo zinakuwa nguo za kutokea. Sare ni lazima kwani ina implication zaidi ya unachofikiria. Nguo za shule n msaada pia w malezi ya mtoto kwani akifanyavisivyo anaweza pata msaada au malezi muafaka. Kwa kifupi hoja yako haina mashiko.
huo ni uzembe wa wazazi na walezi na sio vizuri kupenda sana vya bure wakati nguvu na uwezo wa kutafuta unao. ningeshauri hao walezi wakishindwa kumpa nwanafunzi mahitaji madogo kama hayo wakamatwe na kupewa vifungo vya nje hata kutengeneza barabara..mitaro na usafi wa mazingira. tusijushushe kiasu cha kupenda kusaidiwa kila kitu. nina uhakika kuna mambo flani ukimba kuwasaidia watakua wakali kweliNimekuwa nikijiuliza ni kwa nini Serikali inalazimisha Wanafunzi wavae Sare za Shule ambazo zinauzwa na huku ikijua wazi kwamba Wananchi wake wengi hawana hata pesa ya kununua Chakula, sembuse ya kununua nguo za Shule?
Kwa nini Serikali iseme Mtoto aende Shule na vazi lolote hata kama ni kanga lkn Bora apate Elimu ambao baadae itamkomboa?
Watotto wengi huko vijijini wanakosa Elimu kwa kuwa hawana Sare za shule, hawaruhusiwi kwenda Shule bila Viatu hivyo wanabaki Nyumbani, sasa Serikali haioni kama inakwamisha Maendeleo yao?
Nimekuwa nikijiuliza ni kwa nini Serikali inalazimisha Wanafunzi wavae Sare za Shule ambazo zinauzwa na huku ikijua wazi kwamba Wananchi wake wengi hawana hata pesa ya kununua Chakula, sembuse ya kununua nguo za Shule?
Kwa nini Serikali iseme Mtoto aende Shule na vazi lolote hata kama ni kanga lkn Bora apate Elimu ambao baadae itamkomboa?
Watotto wengi huko vijijini wanakosa Elimu kwa kuwa hawana Sare za shule, hawaruhusiwi kwenda Shule bila Viatu hivyo wanabaki Nyumbani, sasa Serikali haioni kama inakwamisha Maendeleo yao?
Nadhani elimu ni bora kuliko unifomu. Hii Tanzania ni kubwa sana, kuna watu Tanzania hii hawana uhakika wa hata mlo mmoja sembuse unifomu. Mshukuruni Mungu mmezaliwa katika familia ambazo japo zina uhakika wa mlo. Hakuna anaependa kuwa na maisha duni, mazingira hayaruhusu watu kujikwamua kutoka ktk lindi la umasikini.
huo ni uzembe wa wazazi na walezi na sio vizuri kupenda sana vya bure wakati nguvu na uwezo wa kutafuta unao. ningeshauri hao walezi wakishindwa kumpa nwanafunzi mahitaji madogo kama hayo wakamatwe na kupewa vifungo vya nje hata kutengeneza barabara..mitaro na usafi wa mazingira. tusijushushe kiasu cha kupenda kusaidiwa kila kitu. nina uhakika kuna mambo flani ukimba kuwasaidia watakua wakali kweli
Mleta hoja aweza kuwa na hoja hapa, ila ni lazima kuangalia pande zote.....wazazi na wajibu wao...na serikali na wajibu wake.
Mimi binafsi naunga mkono uvaaji wa uniforms...kwani hata kuvaa uniform kila anapoenda shule mwanafunzi ni sehemu ya elimu....si sawa na kumkuza mtoto anayekurupuka tu asubuhi na "masurupwete" kubeba madaftari na kukimbilia shuleni....lazima tujenge jamii itakayotofautisha shuleni na machungani (kuchunga ng'ombe, kondoo au mbuzi).
Na kama kweli shule zetu zinatimiza wajibu inavyotakiwa, huwa ni rahisi zaidi kusimamia usafi wa mwanafunzi akiwa na uniforms kuliko akija amevaa blangeti.....
Pia inajenga nidhamu kwa wazazi na watoto wao kwani huwapelekea kufanya juu chini kuhakikisha uniform ni safi kwa njia yoyote ili kufuata matakwa ya shule....bila hivyo hakutakuwa na ufuaji wa nguo aise.
Nasi wanainchi pia lazima tuangalie na upande wetu...nadhani tuepukane na kuongeza tuuu familia....kama mzazi unajiona huna uwezo epuka familia kubwa....watoto watano, sita au saba wa nini wote hao...
Nimekuwa nikijiuliza ni kwa nini Serikali inalazimisha Wanafunzi wavae Sare za Shule ambazo zinauzwa na huku ikijua wazi kwamba Wananchi wake wengi hawana hata pesa ya kununua Chakula, sembuse ya kununua nguo za Shule?
Kwa nini Serikali iseme Mtoto aende Shule na vazi lolote hata kama ni kanga lkn Bora apate Elimu ambao baadae itamkomboa?
Watotto wengi huko vijijini wanakosa Elimu kwa kuwa hawana Sare za shule, hawaruhusiwi kwenda Shule bila Viatu hivyo wanabaki Nyumbani, sasa Serikali haioni kama inakwamisha Maendeleo yao?
Haujajibu swali unaleta tu maelezo marefu. Nimekuuliza Je, kwa maoni yako unaona Ni bora mtoto abakie Nyumbani mpaka mzazi apate Fedha ya Kumnunulia Sare?
Unachoongelea wewe ni Matokeo ya mambo ambayo yameshatokea, watoto wameshazaliwa kama wazazi wao walifwata au hawakufwata Uzazi wa mpango hilo ni swala lingine, lkn hoja wapo tena wengi na wanazuiwa kwenda Shule kwa sababu hawana Sare, sasa Je ni sawa kumkosesha mtoto Elimu kwa sababu baba au mama au sijui Mlezi hana fedha ya kununua Sare ya Shule? Ndio Hoja yangu hapa! Haijalishi kama Baba au Mama ni mlevi ukweli unabaki kwamba Mtoto au Watoto hawasomi, sasa Je ni haki kwa huyu Mtoto? Yeye ana kosa Gani?